Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana..
Sasa kundi la marehemu linatokana na nini huku mwenyewe hayupo?

Nina uhakika Ndugai yuko kundi hilo

Ushahidi huu hapa .

 
Magufuli ni nani asipingwe.

Watu wanampinga Mungu itakua magufuli.

Tatizo magufuli kawatenda wengi sana ndivyo sivyo ndo mana wengi wanampinga.
 
Ndugai kuna kitu anakitengeneza yeye ndio tatizo halafu anataka apate point kwa kutatua tatizo, kama ccm wako makini wamwondoe mapema vinginevyo huko mbele atawaletea madhara makubwa
Tatizo ni Mahera na ile tume! Saboofer ibaki hiyo, wademke weeee, mpaka wachoke! Mungu atawafanya kuwa mfano wote waliotenda dhuluma!
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.

Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli.
Sasa wanaitana caucus wapi na wapi wakati wenyewe humo humo ni caucus tupu mjengoni
 
Kila kilichokuja kiharamu kitaondoka.Ni suala la muda tu.Sioni mama akifika mbali na hili bunge la ajabu!Na linajimaliza lenyewe,na iwe hivyo haraka iwezekanavyo ili wasitucheleweshe kufanya reforms za msingi kwenye nchi yetu.Hatuna mda wa kukimbizana kidali po na watoto.Waende nje wakamalizie michezo yao kwanza.
Hata Urais wa Magu ulikuwa hramu
Ilikuwa zamu ya kutoka Zenji
 
She is right, kuna jitihada kubwa sana zinaendelea za kumchafua Magufuli
Kwa Magufuli wala haziitajiki jitihada kumchafua.

Alishajichafua enzi za utawala wake akiwa hai kwa mambo kadha wa kadha ya hovyo aliyoyafanya.

Nnachokiona ni mataga wanatafuta namna ya kufanya magu aonekane malaika.

Na akitokea mtu akisema mabaya yake ataambiwa anataka afute legacy ya mwendazake.

Legacy gani inalazimishwa hivyo?.
 
Lucy mayenga alikua chakula ya mwendazake apite hivi
Mbunge wa viti Maalum Lucy Mayenga amedai leo Bungeni kuwa kuna kundi la wabunge wengi ambao wanamepanga kuhujumu legacy ya Magufuli na kutaka kutenganisha Urais wa Samia na urais wa Magufuli

Amedai wabunge hao wanamsifia Samia Suluhu kwa lengo la kuonyesha kuwa Maguuli alikuwa akifanya vibaya na tangu awali wanafahamika kuwa walikuwa wakimpinga Magufuli.
Ameongezea watu hao kuwa wanamchonganisha Samia na watu wa Magufuli ambao alikuwa amewapanga na mikakati yao wanaijua

Zaidi unaweza kumsikiliza hapa

 
wabunge wa dizaini hii kwakweli tumepigwa yaani wanaendelea kudemka tu, ni hivi tu uchaguzi ni ghali mama alitakiwa avunje bunge kabisa
 
Unaleta habari ya upotoshaji inakusaidia nini? Sawa kuna makundi haya wewe inakusaidia nini?
Wewe Kawe acha hizo
Upotoshaji upi Huyo mama Mangenya na Spika hukuwaona na kuwasikia
Mataga Kawe alumini mpaka Id zenu mmezikimbia buku 7 kwishine nahivi mmembania Chakubanga nani atawalipa Imeumana
 
Alhamis sio mbali wao waendelee kudemka, kwa kuwa siku hiyo inaweza kuwa ni siku muhimu kwa Wabunge kufungasha virago vyao.
Wabunge hao hawana tofauti na wale vijana wa JKT, tena yawezekana wao wamezidi kwa kuwa wanatengeneza uasi ndani ya Bunge kwa kutumia kodi za Wananchi.
Hata hivyo mpangilio mzima wa shughuli za kibunge ujielekeze kwenye kufuata Katiba ya Nchi, wabunge ambao hawatambuliki na vyama vyao si busara kuendelea kuwa ndani ya Bunge.
Ili kuleta taswira nzuri ndani ya Bunge ni busara kwa Spika na Naibu wake wajiuzuru nafasi zao kwanza,hii itawasaidia na wao kutengeneza legacy nzuri ya uwajibikaji ndani ya Bunge hasa inapotokea Mkuu wa nchi kutokupendezwa na utendaji wa Bunge /Wabunge.
 
Sasa kusifia ni kosa? Au kupinga ni shida,?legacy kama ipo ipo tu!Hawa wanakera sana,ajili zao sijui huwa zinawaza nini yaani na hawawezi kamwe watu na namna hii kulisaidia taifa kwa kupitia bunge
 
Waache wamalizane wenyewe kenge hao si walitaka bunge la chama kimoja?? Waendelee na ushetani wao
Tatizo hawana hoja Hawa mataga.Hoja zao ilikuwa kutukana wapinzani. Sasa hawapo waya yaparulane
 
Bado WANADEMKA kwa ngoma inayopigwa mitandaoni.
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.


Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli.
 
Back
Top Bottom