Sasa ndio nimeelewa kauli ya kusema nimesacrifice maisha yangu kwaajili ya Watanzania maskini

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
5,975
7,731
Ndugu zangu

Sasa ndio nimeelewa kauli ya kusema nimesacrifice maisha yangu kwaajili ya watanzania maskini.

Nimeelewa hivi kiongozi kusacrifice maisha yake kwaajili ya watanzania ni kitendo cha kutumia fedha zote za umma kuijenga Tanzania na kukataa kushirikiana na viongozi wenzake wenye nia ya kuiba, kudhulumu, kuhujumu na kufisadi mali na fedha za umma.

Mtanzania mwenzangu wewe unaelewaje.

Tafadhali toa maana yako.
Huu uzi sio kwaajili ya kuwasema watu bali ni uzi, tunataka tupate maana ya kusacrifice maisha maana yake nini. Kila mmoja ajikite kwenye kutoa maana badala ya kuwasema watu.
 
Ni mapema sana kuja na hitimisho hilo.
Madam President SSH alikuwa VP wa JPM kwa miaka 5 na miezi 5,
Waziri Mkuu bado ni yule yule na hata baraza la mawaziri kuna mabadiliko sio kivile.

Madama SSH alisema yeye na JPM ni kitu kile kile, huenda mode of operation zikabailika maana anatumia ilani ile ile, na katiba ni ile ile.

Japo Madam alisema viatu vya JPM havimtoshi, bila shaka akatumia rungu lake ili kuwadhibiti panya buku wasipige madili.

Ila kwa inavyoonekana yale mambo ya kujenga kibanda cha mlinzi kwa mamilioni ya shilingi mpaka waziri mkuu anashtuka siku ya uzinduzi nchi hii yanatisha.
Au wale washua wa hazina waliokuwa wana-saini vocha za malipo ya kujilipa mamilioni siku moja tu (mei mosi ya 2021); mambo hayo yanaonekana kuwa ni ajabu ila yanafanyika Tanzania hii hii.

Mungu atusaidie, ni nchi hii

Ni nchi hii Rais JK alishuhudia "kutia saini' na kuweka jiwe la msingi, baadae waziri anakuja na kusema haukuwa mkataba ili yalikuwa mazungumzo/makualiano.

Hapo napo sijui kuna madili au ni mkanganyiko wa lugha gongana kwa waziri wa sasa ambae alikuwa DC awamu ya 5, akawa boss wa kituo cha uwekezaji awamu ya tano, akawa waziri awamo ya tano, leo awamu ya sita anasema... (naomba nisiendelee).

Hapa chini kuna rejea ya mambo ya zamani. Tusiwe na hasira sana, ni mambo ya zamani na labda ilikuwa "rehesal"; au ahh, nchi hii ngumu sana.

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BANDARI YA MBEGANI BAGAMOYO

MICHUZI BLOG AT FRIDAY, OCTOBER 16, 2015

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Usultani wa Oman Hon.Dr.Ahmed Mohamed Al Furaisi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya China Merchants Group Dkt. Hu Jianhua wakichanganya kokoto kuzindua rasmi ujenzi wa Bandari ya Mbegani iliyopo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani leo.Bandari hiyo kubwa inajengwa kwa ubia kati ya serikali ya Tanzania, China na Oman.(Picha na Freddy Maro).

Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Kusaini mikataba.

Wakionyesha mikataba iliyosainiwa.
 
Ndugu zangu

Sasa ndio nimeelewa kauli ya kusema nimesacrifice maisha yangu kwaajili ya watanzania maskini.

Nimeelewa hivi kiongozi kusacrifice maisha yake kwaajili ya watanzania ni kitendo cha kutumia fedha zote za umma kuijenga Tanzania na kukataa kushirikiana na viongozi wenzake wenye nia ya kuiba, kudhulumu, kuhujumu na kufisadi mali na fedha za umma.

Mtanzania mwenzangu wewe unaelewaje.

Tafadhali toa maana yako.
Kabla ya kupongeza tueleze trilioni 1.5 ziko wapi?
 
Lile jizi lilijenga kwao tu. Kwingine liligoma kujenga eti kisa hawampendi
Ndugu zangu

Sasa ndio nimeelewa kauli ya kusema nimesacrifice maisha yangu kwaajili ya watanzania maskini.

Nimeelewa hivi kiongozi kusacrifice maisha yake kwaajili ya watanzania ni kitendo cha kutumia fedha zote za umma kuijenga Tanzania na kukataa kushirikiana na viongozi wenzake wenye nia ya kuiba, kudhulumu, kuhujumu na kufisadi mali na fedha za umma.

Mtanzania mwenzangu wewe unaelewaje.

Tafadhali toa maana yako.
 
Biased statement.
CAG alipohoji matumizi yasiyoeleweka ya shilingi 1.5 trilioni aliishia kupokwa kibarua chake kinyume na taratibu za uteuzi wake. Mpaka kesho hatujui zilielekezwa wapi zile pesa.
Kama kulikuwa na ufisadi unadhani hawa wanaochafua legacy ya mzee wangemnyamazia.... acheni kuokota maneno ya mtaani... ni siku tu utaambiwa ulipie hiyo hewa unayovuta ndo utaelewa kuwa upo kwenye sayari gani...

He was the true Son of Africa, the Hero
 
Kabla ya kupongeza tueleze trilioni 1.5 ziko wapi?
Pia ungeuliza mamilioni ya pesa alizokula anagawa njiani kwa wananchi maskini alitoa wapi?

Nyoka wa makengeza aliwahi kusema..kosa gani kuchukua pesa serikalini na kujenga barabara Bariadi?

Utakuwa umenielewa.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom