Sasa nataka kuoa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa nataka kuoa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mayenga, May 7, 2010.

 1. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa mtazamaji na mchangiaji katika jukwaa kwa muda sasa.Lakini ombi langu kwa leo nadhani umefika muda niseme kwamba nahitaji mke.Sifa zifuatazo zinahitajika.Mzuri wa haja,mweusi(si kama Idd Amini),mwenye urefu wa wasitani,asiyependelea vileo,mwenye kiu ya maendeleo, MCHA MUNGU,asiwe ni ndiyo mzee(she must be critical),awe mfanyakazi kwa kujiajiri au kuajiriwa (lakini si mwanasheria),Umri walau kuanzia miaka 23 mpaka 25.La muhimu zaidi asiwe mwanasiasa.Karibuni.
   
 2. kobonde

  kobonde Senior Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Jan 6, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  punguza masharti utampata
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Nipunguze lipi mdau?
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  All the best lakini unachagua sana....hivi hapo ulipo hakuna mabinti?
   
 5. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mshkaji utachemsha, mwanamke wa kuoa siku zote si external features ni moyo wake ukoje kwako. Ila kama uataka wa kupita nae kwenye red carpet OK go ahead!!
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  All the best kaka, lakini haya mambo huwa yanatokea automatically, unaweza kukutana naye tu na roho yako ikakwambia she is the one, so you dont need all that.
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  akitokea mweupe hutamuangalia hata kama ana sifa nyengine ulizotaja? na jee kama ana miaka 30?

  kaka punguza masharti kisha omba mungu akuletee mke bora tu, akiwa na sura ya kukuridhisha kidogo tu inatosha
   
 8. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Y excluding wanasheria and wanasiasa? Hakuna wife materials miongoni mwao? En yz, kila la kheri ktk harakati zako
   
 9. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  iish....mimi niko tayari lakini mwaka huu nagombea udiwani kwa tikiti ya mbayuwayu upo tayari?
   
 10. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  she must be critical - lakini angalia asije kucritisize kila kitu mpaka ukajiona hovyo,
  kwann asiwe mwanasheria au wewe fisadi?
  asiwe mwanasiasa - hutaki kuja kuwa mume wa raisi cku moja?

  lakini penzi halichagui elimu wala uzuri au bado hujapenda?
   
 11. M

  Mchili JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa masharti hayo hata asipokupenda utamuoa?? Anaweza jitokeza muigizaji wa ndoa.
   
 12. Bright

  Bright Member

  #12
  May 7, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ni vizuri na wewe ukatoa sifa zako naye atakaye endana na hivyo vyako afanye maamuzi. In pyschology it is said "human beings are very complex"; that is, they can behave unexpectedly in a good or bad manner.
   
 13. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kaka mbona masharti kibao? Je akiwa na sifa zote ila akawa mwanasheria bado humtaki? Hebu tupe ishu kwa nini usingependa kuoa mwanasheria?
   
 14. M

  Mchili JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwani Girl friend wako amekupiga kibuti?
   
 15. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #15
  May 7, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila la kheri ila mh! kwa masharti hayo!wataogopa!!
   
 16. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kaka naona kama we mkuda fulani hvi... masharti mbona magumu! labda hilo la kumcha Mungu. Na ukipata wa kumcha Mungu huonji kitu hadi siku ya ndoa!
   
 17. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua mi sijaweza kuelewa hii staili ya kutafuta wachumba kwenye mitandao mi nadhani kama muda wa kuoa au kuolewa unafika pale unapompata mtu mnaanza urafiki uchumba then unaoa lakini usikurupuke tuu kwa kutangaza unataka kuoa unaoa nini sasa maneno! muombe mungu wako akupe mke mume mwema...naboreka sana kuona thread watu wanatoa humu na kuweka masharti ya nataka hiki nataka kile...kwa hiyo wasio na hizo sifa hawataolewa au kuoa achen hizo bana...muda wako ukifika hutakuw na hata haja ya kuesma ni hayo tuu kwa leo...
   
 18. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kizazi kipya yoyo nyiiiiiiiiingi
   
 19. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waache wakupige vijembe,but at least unajua unachokitaka.....

  hata kwa fundi wa nguo tunaenda tunamwambia nishonee hivi au vile,hatumwambiiii tu nishonee utakavyo!
   
 20. T

  Tall JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kwenye rangi NYEUSI: BAADA YA NDOA HALAFU AKAFUKUZWA KAZI UTAMWACHA?....KWENYE RANGI YA BLUU:unampango wa kumuonea/kumdhurumu mkeo mtarajiwa? kuna jirani yangu hapa ana binti yake ni mfanyakazi nasikia anafanya kazi pale kwa macheni,...tukuunganishie mzeeee?
   
Loading...