Sasa nasema Bw. Bernard Membe wacha domo weye! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa nasema Bw. Bernard Membe wacha domo weye!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 8, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280


  Waziri wa Mambo ya Kigeni, Bernard Membe hasemi ukweli hata kidogo alipojigamba ya kuwa serikali ya CCM itahakikisha uchaguzi huu unakuwa huru na haki.
  Kauli hii aliitoa kwenye mkutano wa kuwakaribisha UNDP na waangalizi wa uchaguzi kutoka nje. Hata hivyo, njama za JK na CCM yake zifuatazo zaashiria ya kuwa CCM imekwisha kuyachakachua na yaendelea kuyachakachua matokeo:-

  a)[FONT=&quot] [/FONT]NEC kutokuwa huru kuajiri watumishi wa kudumu na badala yake kuazima watumishi kutoka serikali za mitaa ambao hawawajibiki kwao. Serikali ya CCM ambayo ndiyo mwajiri mkuu wa watumishi hao ni dhahiri yasubiri kivuno kikubwa cha kuchakachua matokeo hapo 31st Oktoba 2010.


  b)[FONT=&quot] [/FONT]NEC kutuzuia wapigakura kuweko mita 200 kutoka katika vituo vya kupiga kura ili kudhibiti mashushushu ambao watataka kujipenyeza na kuwarubuni mawakala hususani wa Chadema.


  c)[FONT=&quot] [/FONT]JWTZ kututisha wapigakura kinyume na majukumu yao yaliyobainishwa kwenye Ibara ya 148 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.


  d)[FONT=&quot] [/FONT]Vyombo vya habari vya serikali haswa TBC1, Daily News na habari leo kukipendelea kwa uwazi chama tawala.


  e)[FONT=&quot] [/FONT]REDET na SYNOVATE aidha kuficha au kuchakachua ukweli wa kura za maoni ambao ulipaswa kuonyesha ya kuwa JK na CCM yake ni hoi bin taabani.


  f)[FONT=&quot] [/FONT]Matumizi ya rasilimali za nchi katika kukibeba chama tawala.


  Hizi hoja hazina majibu na kwa hiyo Bw. Membe ninamwamuru kufunga bakuli lake na siyo kuendelea kujidhalilisha machoni pa umma wa dunia kuwa hajui asemalo.
   
 2. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Huyu Membe tunamfahamu nilisema naye Mlimani degree ya kwanza Political Science and Public Administration. Tuligraduate pamoja mwaka 1984. Ni mwongo sana, hiyo ni silika yake. Binafsi nilishangaa na kupigwa butwaa kusikia amepewa wadhifa huo wa Waziri wa Mambo ya Nje badala ya Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro. Lakini vyeo Tanzania yetu hususan serikali ya Awamu ya Nne vimekuwa vikitolewa kiholela bila kuangalia competence ya watu wenyewe. Ndiyo sababu tunapata mtu kama huyu mwenye kudiriki kuwaambia watu wa UNDP na wasimamizi wa uchaguzi (election observers) kutoka nje kuwa watahakikisha uchaguzi utakuwa wa haki. Uchaguzi utakuwaje wa haki wakati watu walio madarakani wankazana kuchakachua matokeo ili waweze ku 'maintain status quo'? Uchaguzi utakuwa wa haki kama kila chama kitapewa haki sawa kwenye kampeni, kutakuwa na mdahalo wa wazi, na chama tawala kitakubali kuwa tulikosea pale na pale, na tukipata nafasi ya kuongoza nchi kwa mara ya pili, tutarekebisha hili na lile. Uchaguzi ambao tayari tumeshaonywa na baadhi ya viongozi wa jeshi, na kuambiwa kuwaccm lazima ishinde tena kwa kishindo utakuwaje wa haki? Uchaguzi ambao mpaka REDET na SYNOVATE wamediriki kuchakachua kura za maoni ili kuonyesha matokeo yasiyo ya ukweli utakuwaje wa haki? Grow up Membe, hii siyo Mlimani ya 1981-1984 ambapo ulikuwa unaweza kutunga uongo ukakubalika. Kama uliweza kudanganya wachache Chuo Kikuu, usifikiri watanzania zaidi ya milioni 40 wa mwaka 2010 utatudanganya.

  Tutakutoa kwenye madaraka wewe na vibaraka wenzako, mkatafute wengine wa kuwadanganya.

  Mungu Ibariki Tanzania!
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeongea na Membe sasa hivi kumueleza ulichoandika kuhusu yeye. Kaniambia wewe tatizo lako ni chuki binafsi isiyofutika tokea enzi za chuo alipokuchukulia demu wako hapo chuoni. Yaani Bw. Kiwi mambo ya mahusiano na ngono unayaendelea tokea miaka ya 80s? Vipi wewe mutu? :wink2:
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Membe nae kazungunzia suala la Shimbo eti hajakosea. Wakati huo huo Shimbo anaonekana kwenye makabidhiano sijui ya matrekta mabovu --Power tillers amabayo ni tender yake kupitia JWTZ.

  Toka lini JW wakawa ni maagent wa bidhaa kama matrekta Tanzania? Membe ..membe ..uza sura tu lakini 31/10/201 haiko mbali.
   
 5. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na mimi nikijadili matendo ya Membe na ukampigia simu atasemaje?
   
 6. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Membe ni mtu wa system (shushushu). Na sifa mojawapo ya kuwa shushushu ni kwamba lazima uwe mwongo
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  TUNATAWALIWA kijeshi period.
  anaye bisha asimame hapa apewe clues
   
 8. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi sana. Kuna moja alikuja kwangu na longo longo zake CCM this CCM that kupima upepo. Nilipombana maswali akaingia mitini na maneno kibao. Unajidai unajua sana na liCHADEMA lenu halishiki nchi ng'o. Nikamwambia kuhoji matendo ya CCM au wana CCM si kwamba lazima uwe CHADEMA au CUF unaweza ukawa mwananchi wa kawaida tu
   
 9. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,448
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Membe anajaribu kulinda mkate wake kwani anajua fika kuwa mabingwa halisi wa nafasi anayoshikilia wako wengi wa kumwaga.
   
 10. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Membe nae kazungunzia suala la Shimbo eti hajakosea. Wakati huo huo Shimbo anaonekana kwenye makabidhiano sijui ya matrekta mabovu --Power tillers amabayo ni tender yake kupitia JWTZ.

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]


  [FONT=&quot]ONYO la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vyombo vingine vya usalama limeibua mjadala mpana na mzito nchini. Ni mjadala unaohusu weledi wa mijeledi. Wengine katika vyombo vya habari wanapigia kelele wakisema si weledi kumbe wanaogopa mijeledi!

  Baada ya Luteni Jenerali Abdulraham Shimbo kutoa onyo, wapo waliostuka na wakidhani JWTZ imetangaza hali ya hatari, wengine wakidiriki kusema imedhamiria kuinusuru CCM huku wengine wakisema ilikuwa ni kazi ya jeshi la polisi.

  Niliposikia hayo wakati nikiwa katika ndege, niliogopa nikidhani wajomba wamechukua hatamu sasa. Hawataki upuuzi na wanataka Jakaya Kikwete aongoze nchi vyema hadi matokeo ya uchaguzi mkuu yatakapotangazwa.

  Lakini baada ya kukaa na kutulia, nilitafuta kauli sahihi iliyorekodiwa na kisha nilipata taarifa sahihi kwamba kumbe JWTZ haijatoka kambini kama ilivyokuwa imeripotiwa na wanasiasa na wadau wengine!

  Kumbe ilichokuwa imekifanya JWTZ ni kujaribu kuonya vyama (ikiwemo CCM) kwamba hakuna damu itakayomwagika; kwani uchaguzi utafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

  Ila, kilichonistua na kuonyesha watu hawajaelewa mantiki ya onyo la JWTZ ambalo ni jeshi lenye historia ya utiifu, ni pale wanasiasa wa Upinzani walipoibuka na nadharia kwamba jeshi limelenga kuinusuru CCM.

  Nilipaswa kurejea onyo la Luteni Jenerali Shimbo, lakini bado nilipata ukakasi kuoanisha na kile kilichozungumzwa na Upinzani asubuhi yake. Wapinzani ambao baadhi tunafikiri ni wanasiasa wasomi, wakajikuta katika lindi la ujinga.

  JWTZ ilisema, kwa niaba ya vyombo vya ulinzi na usalama: "Hakuna umwagaji damu utakaofanyika. Uchaguzi utafanyika kwa amani na kwamba vyombo hivyo viko tayari kupambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani."

  Hapa ukifanya uchambuzi wa kimaduhui, huoni hata sehemu moja ambayo JWTZ inasema imepanga kuibebea mbereko CCM kama ilivyodaiwa na vyama vingine vya Upinzani.

  Jambo la ajabu kabisa ni kwamba, hata mwanangu wa chekechea alimwelewa Shimbo. Alichokisema ni kwamba, wao wa vyombo vya ulinzi na usalama watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani ya nchi.

  Lakini, nilistuka kusikia eti JWTZ imepanga kuinusuru CCM! JWTZ haikusema kwamba vyama vya Upinzani vikubali matokeo yoyote ambayo yatatangazwa kwamba CCM imeshinda. Ilichosema ni kwamba vyama vya siasa, ikiwemo CCM, vikubali matokeo yoyote.

  Sasa unaweza kuona jinsi uwezo wa kufikiri wa baadhi ya wanasiasa wetu ulivyo mdogo au kuchanganyikiwa na mambo mengi ya maisha. Ni wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia.

  Wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia, kifamilia na jamii, ndiyo ambao huweza kutamka na kurupoka kile walichoota jana usiku kwamba, kuna njama za kutaka kumuua. Inawezekana jana usiku mwanasiasa aliota kakabwa na jinamizi la usingizini, basi, anaamka asubuhi na kuambia umma yuko tayari kuuawa!

  Huu ndiyo ujumbe tuliopata baada ya JWTZ kutoa onyo. Jeshi lina dhima ya kulinda nchi kutoka maadui wa ndani na nje, Jeshi lina intelejensi yake (Military Intelligence), kwa mantiki hiyo, linapozungumza kuna njama za watu kuvuruga amani, huwa halikurupuki.

  Nilitegemea wananchi walipongeze jeshi kwa kuonyesha msimamo mapema na kutoa onyo kwa watu wanaotaka kuivuruga nchi. Unashangaa unaona wanasiasa wenye kuangalia madaraka badala ya Tanzania wanakurupuka na kulihusisha jeshi na mbeleko kwa CCM.

  Wapo wanaosema JWTZ imeenda mbali zaidi kwani hilo lilikuwa jukumu la jeshi la polisi, lakini wamesahau kwamba hatua ya jeshi kuchelewa kuchukua hatua ndiko kunakofanya nchi kuvurugika na damu kumwagika.

  Leo hii, watu wanalalamika uzembe katika kudhibiti mauaji ya halaiki ya Rwanda, kwa sababu Dk. Kofi Annan akiwa mkuu wa Ulinzi na Usalama wa UN, alishindwa kushauri umoja huo haraka kuzuia mauaji nchini humo.

  Kwa mantiki hiyo, JWTZ iko sahihi kuhakikisha amani ya nchi haivurugwi na maadui wa ndani au nje. Jeshi limekuwa sahihi kutoa onyo mapema kwa sababu hatuwezi kuruhusu umwagaji damu wa kutisha ndipo tuombe nguvu za jeshi.

  Amani na usalama wa nchi haufanyiwi majaribio. Amani, uhuru na umoja wa kitaifa unalindwa kwa nguvu. JWTZ imekaa katika nafasi yake husika.

  Nimestushwa kusikia kauli ya JWTZ ikihusishwa na mbereko dhidi ya CCM. Hili ni jambo la kipumbavu. Kwa nini CCM ikae kando wakati nacho ni chama cha siasa kinachopaswa kutii matokeo kama kikishindwa?

  Uropokaji huu wa wapinzani umezidi kuifanya CCM ionekane kama ni chama makini, kilichobobea katika siasa na kisichokurupuka. Ndiyo maana, ingawa chenyewe ni chama cha siasa, hakikutaka kukurupuka na kuirukia JWTZ.

  Kwani kinajua jeshi letu lina nidhamu ya hali ya juu, halijihusishi na mambo ya siasa za majitaka, lina nidhamu, utiifu na uzalendo.

  Hivyo, kudhani kauli ya JWTZ ni mbereko kwa CCM ni mawazo yasiyosadikika, na ni dhana tu isiyo na mashiko. Ni vema vyama vikaiga ukimya wa CCM.

  [/FONT][FONT=&quot](Source: RAIA MWEMA NEWSPAPER)[/FONT]
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Halafu umati huo wa waajiriwa wa NEC (unaotaka waajiriwe)watafanya kazi gani mara baada ya uchaguzi mkuu kupita?! Yaani walipwe mshahara wa bure kwa kipindi kizima cha miaka mitano?!
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Nahisi unataka kutuambia kwamba kumbe hata wana CHADEMA nao wananunulika (TAFSIRI NYEPESI NI KWAMBA WANAWEZA KUWA MAFISADI) otherwise usingekuwa na hofu ya kwamba mashushushu wanaweza kujipenyeza na kuwarubuni mawakala wenu! Katika mtiti wa uchaguzi kama huu, na hofu mliyonayo juu ya kuibiwa kura, basi sina shaka yoyote kwamba mawakala mtakaowateua ni wale walio royal to the chama! Sasa kama hata walio royal mna mashaka nao, so who should we trust?! Siamini kama mngekuwa na hofu ya mashushu endapo mawakala wenu (WANA-CHADEMA MNAOWAAMINI) wangekuwa ni aina ya Baba wa Taifa mnayehubiri kufuata nyendo zake!
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  A black cat may be bad luck only if you are mouse!
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Nazani sio vibaya mkijipoza na utafiti wa JF kwavile ndio pekee unaoaminika na wana-CHADEMA!!
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  CONCLUSSION: Sasa ikiwa mnaamini kabisa kwamba uchaguzi hautakuwa huru na haki, ya nini kupoteza raslimali zenu kushiriki wakati mnafahamu fika kwamba hautakuwa huru na haki?! Kwanini msisusie kama wanavyofanya wenzenu pale wanapohisi kwamba uchaguzi hautakuwa huru na haki?! Ili halina haja ya kujifunza toka mbali kwani hata CUF walishawahi kususia kushiriki! I hope mnafahamu fika kwamba utakuwa huru na haki lakini hamtakuwa tayari kukubali matokeo
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Unajuaje kama Kiwi ni mwanamume? Acha kutuletea comedy hapa!
   
Loading...