Sasa namwelewa kwanini Mkapa hupenda sema Watanzania ni wapumbavu(ashakum si matusi)

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Mods naomba msiubanie huu uzi au kutaka ku edit. nina ushahidi wa audio Mkapa akitamka maneno hayo.sijamsingizia wala sijamkashifu na sijakashifu au watukana watanzania.

1. mtu anachukua pesa za wizi na zilipigiwa kelele miaka kadhaa baadaye baada ya kuwa amezifanyia kazi yake anarudisha tunafurahia sana na kusema ni mwanaume halafu tunamwacha aendelee kutembea akicheka alivyotufanyia. sisi tunamsifu na kumshangilia. MKAPA YUPO SAHIHI

2. kuna vichwa vya train vipo bandarini havijulikani vimetoka wapi ila inaonekana rais ndo kaenda kuvigundua maana vilikuwa havijulikani kama vipo. sasa issue inakuwa nani kavileta? haijulikani na tunashukuru rais kuvivumbua vile vichwa ila tunaishia hapo hapo. MKAPA YUPO SAHIHI

3. aliyekuwa rais kipindi kile ndugu kikwete alisema pesa za ESCROW ni halali kwake na kwa wengine waliopokea miaka michache ijayo tunawasumbua akina rugemarila na sigh wakati rais alihalalisha pesa zile na anadunda tu mtaani hatujamtaka naye aje ajieleze .MKAPA YUPO SAHIHI

4. yanayoendelea kibiti tunaambia ni chama flan cha upinzani... na waziri mwenye dhamana halafu haweki ushahidi wowote anaendelea tu kupokea salary na posho zetu. huko kibiti watu wanauawa na hao majambazi kila siku wanauawa badala ya kukamatwa kufanyiwa mahojiano ufahamike ukweli. hatujiulizi tunaendana na midundo ya nyimbo hizo na tunaitikia tu kwnye pambio. MKAPA YUPO SAHIHI

5. habari za makinikia/maboso zilivuuuuuuuuuma na mbwembwe kadhaa sasa.... aisee..tukaja kushangilia hapa n.k yameisha . MKAPA YUPO SAHIHI

6. MADAWA YA KULEVYA zikafanyika sanaa na uigizaji wa kiwango cha juu kwa kuchafuana na kukomoana. na sasa tumeshasahau . MKAPA YUPO SAHIHI.


HALAFU KUNA MTU ANATHUBUTU KULALAMIKA KUWA MKAPA ALITUKANA. ALIMTUKANA NANI? mtu akikwambia we mweusi na kweli we mweusi anakuwa amekutukana vipi wakati kakwambia sifa zako?

SASA NIMEMWELEWA MKAPA KWA NINI ANASEMA VILE. naamini na mgodi wake kule mbeya unaendelea kutema tu madini. apewe nini baba wa watu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom