Sasa nahama CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa nahama CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akashube, Nov 18, 2010.

 1. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa mwanachama mfu wa CCM kwa muda mrefu, hasa baada ya kuchoka kuishi katikati ya uozo wa kisiasa ndani ya chama hicho. Nimekuwa nikisita sita kwa kuwa sikuwa na uhakika kama kweli vyama vya upinzani viko 'serious'.

  Nilikuwa nasubiri kuvipima kwenye matukio mazito maana bila matukio mazito kila kimoja kilionekana chama cha upinzani. Leo hii baada ya matukio mazito ikiambatana na baadhi ya vyama kupewa rushwa ya madaraka na CCM, ndipo imethibitika kuwa kuna chama kimoja makini cha upinzani nchi hii.

  Baada ya leo hii CHADEMA kufanya tukio la kishujaa bila kujali kwamba watakosa madaraka haya au yale bali kwa kuweka maslahi ya haki ya wapiga kura wa Tanzania mbele, sasa nimeamua rasmi kuhama CCM na uanachama wangu mfu na sasa nahamia CHADEMA.

  Ninahama na kundi la wapiganaji zaidi ya hamsini tulio kwenye maeneo nyeti sana katika nchi hii.

  Buriani CCM, Buriani CUF, Buriani wasaliti wote.


  NIMERUDI CCM

  Ni kwa sababu ya kuridhika na Team iliyochaguliwa kuongoza CCM 2012 - 2017. Na hasa Philip Mangula. CCM OYEEEEEE!!!!!!!

  CCM ni chama sikivu, Mwenyekiti na viongozi wenzake wamesikiliza vilio vya wananchi, CCM imerudishwa kwa wananchi, wajumbe wa NEC tumewachagua tokea vijijini kwetu, kwenye matawi yetu, hata wanyonge tumeshirikishwa kuongoza nchi. Na sasa wakulima wenzetu kina Mangula wako kwenye uongozi. Kwa hekima ya ajabu ya mwenyekiti, ufisadi umebomolewa kabisa, na sikutegemea kabisa kama Jakaya Kikwete angeweza lakini ameweza.

  Nyinyi mnaobisha ni kwa sababu mnasimuliwa mambo, mimi nayaona kwa macho yangu. Mimi kamwe sitaingia kwenye uongozi wa siasa na hivyo sina tabia ya kujipendekeza kwa kutaka uongozi. Mimi nina kazi yangu binafsi isiyohitaji kubebwa na mtu na inanitosha, ila sikuzaliwa mtanzania ili kukodolea macho watu wanaoharibu Taifa hili. Hilo siwezi kulikubali kamwe.

  Ukweli ni kuwa chini ya uongozi wa Jakaya Kikwete, nilifika mahala nikadhani amekuwa msaliti, sikujua kuwa mbinu zake za kuipigania nchi hii zilikuwa za hali ya juu mno. JK ni kama mchora picha mahiri ambaye anapoanza kuchora unaweza kudhani kuwa anaharibu lakini akimaliza ndiyo unaona picha kamili, picha nzuri, picha iliyojaa ushindi kwa watanzania.

  Kwa kweli umahiri wa JK umenifanya nirudi CCM huku nikiona aibu kubwa kwa kumhukumu kiasi cha kumtukana na kumtakia mabaya na kumbe yeye alikuwa akifanya mema kwa ajili ya nchi hii. Furaha niliyo nayo inaizidi aibu niliyo nayo kwa kumchukia bure mtetezi wa kweli wa Taifa langu.

  CCM ni chama sikivu, ni chama cha wanyonge. CHADEMA ni chama cha siasa kali, fikira mgando. Ndani ya CHADEMA namewaona watu wachache sana wa maana, mfano Zito Kabwe na Shibuda . Wengine wote ni watu ambao hawataki kufikiri; yaani hata jambo likiwa kwa manufaa ya taifa ili muradi linatoka CCM wao wanalipinga tena hata bila kuboresha.

  CHADEMA hawana uwezo wa kutoa hoja bila kuchonganisha wananchi na serikali yao. Kuna watu CHADEMA wanatamani kuhamia Syria au Somalia kwa sababu ya kupenda vita. CHADEMA wanatamani kuingia Ikulu kwa uongo na kwa wale wanaodhani kuwa CHADEMA ni chama cha wakatoliki hiyo siyo kweli, hawa wengi wao ni freemasons, wazee wa ma'casino', watoa kafara mikutanoni wakihakikisha damu inamwagika ili wananchi waone polisi wanaua kumbe wao wametoa kafara kwa mashetani.

  CCM pekee ndiyo chama chenye kuweka maslahi ya Taifa mbele.

  CCM DAIMA!!!!!!!
   
 2. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  We did not even notice you existed. Its better to die in CCM than being alive in CHADEMA.

  Umekosa madaraka and now you are crossing over, uchaguzi umepita unafuata nini huko?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Akashube,
  Hauko peke yako. Katika matanuzi yangu bongo hivi karibuni nimekutana na wana CCM wengi tu ambao wako disillusioned na chama chao.
  Wengi wametoa mchango wa hali na mali kwa CHADEMA na baadhi wanaendelea kutoa mchango wa mawazo na ushauri. CHADEMA is a growing party. CCM is Titanic na wote waliomo kuna wakati watatambua kuwa wamekwaa meli inayozama.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwagalie huyu naye. Atakufa na Titanic yake.
   
 5. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Wanafki wanasubiri vyeo....hawaangalii maslahi ya nchi, udini na tamaa ya vyeo umewajaa.
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135

  Sasa mtu asibadiri msimamo?
  Kosa lake ni lazima liwe kukosa Cheo?

  Acha zako wewe!
   
 7. W

  We know next JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Akashube, ombi langu, wewe na kundi lako la watu 50 toka maeneo nyeti, kila mmoja wenu atoke na watu wengine 50 toka ktk maeneo hayo nyeti, najua mnaweza mkishawaonyesha njia. Historia ya nchi hii itakuja kuwaenzi.
   
 8. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Please JF could do you start a contest for "the most stupid statement of the month"? I submit the red coloured bit from Ninja for November 2010.
   
 9. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAMENI NYOTE, KWANI MLILAZIMISHWA KUKAA CCM?? OPPORTUNISTS WAKUBWA NYIE.:nono:
   
 10. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  karibu tujenge chama
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  I have come to a conclusion that "Many people are alive only because it is illegal to shoot them"
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hongera sana ila angalizo; Usihame na uanachama wako mfu, uanachama mfu uache hukohuko ccm na ingia CHADEMA na uanachama hai na wenye kutegemewa kujenga chama imara zaidi.
   
 13. c

  chipegwa Member

  #13
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unahama baada ya uchaguzi, chadema ni kuti kavu hilo maneno mengi matendo sifuri, mbona kenya waliwasha moto mpk dunia iliwasikia. TUNATAKA MATENDO SI MANENO.
   
 14. M

  Mkerio Member

  #14
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2006
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo wewe huijui siasa. Kushinikiza katiba mpya na tume huru ya uchaguzi si lazima uingie barabarani. Unaweza kutumia shinikizo kama la kutoka nje ya ukumbi kama walivyofanya chadema, mabalozi watajua kuna tatizo, watanzania watajua yote si shwari. Shinikizo litafanya CCM wakubali tume huru. Bila tume huru na vyombo huru kama jeshi, polisi, TAKUKURU, msajili wa vyama nk upinzani hauwezi kushinda milele.
   
 15. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unataka vitendo gani zaidi ya ulivyoanza kuona jana. Utopia!!!!
   
 16. Mpelijr

  Mpelijr Member

  #16
  Nov 19, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  hongera sana ndugu yangu...sasa hivi siyo enzi za kudanganyana kwa maneno.......1 down 22million to go....way long!!!!!
   
 17. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli incentive ya CCM ni madaraka au ufisadi. SIDANGANYIKI Akashube unachokifanya ndicho unachokiamini endelea hongera sana usigeuke nyuma
   
 18. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  CCM mnachoangalia ni uchaguzi tu, ndio maana mnaiba kura. Mimi sasa nimeondoka huko kwa kuwa nataka kutazama masuala ya muhimu kuhusu mustakabali wa taifa hili.
   
 19. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  karibu milango ipo wazi kwa wanachama makini, wanaokuponda wote ni wanasisiemu hata uwezo wao wa kufikiri ni kama ulivyousoma hapo juu
   
 20. M

  Musia Member

  #20
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  nawaunga mkono CHADEMA kuhusu kudai katiba na tume huru ya uchaguzi, wanaopinga hilo aidha ni mafisadi au watoto wa mafisadi
   
Loading...