Elections 2015 Sasa naanza kupata picha kwamba Apson Mwang'onda yupo kwa Lowassa kikazi zaidi...

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Nimeanza kuunganisha dots na kwa mbaali naiona picha kuwa kitendo cha Jasusi mkuu mstaafu wa nchi yetu kujiunga na kambi ya Lowasa kilikua ni cha kimkakati zaidi. Kwa wanaomfajamu Apson na utendaji wake tulijiuliza sana lakini tulikosa majibu.

Leo hii mara baada ya Edward kumaliza kufanya kampeni (Ninasisitiza kuwa ni kampeni na si kutangaza nia) yake pale uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ndipo nikazinduka na kutambua kuwa Apson alikua 'under cover' akiwa na jukumu maalum la kumdhoofisha Edward and Kingunge nailed it. Hili suala la magenge ya wasaka madaraka yaliyumbisha sana idara yetu ya usalama wa taifa kitu kilichopelekea idara hii kushutumiwa sana mitandaoni pia na makundi mbalimbali ya kijamii.

Ilikua si kazi rahisi kulimudu hili genge maana lilishajijenga vya kutosha na namna pekee ya kulisimamisha ilikua ni lazima the big man aingie in the war front and to begin with ilibidi ku step down then kujipenyeza ndani ya kambi hii ambapo na ku gain trust. Seems lengo la yeye kwenda front ilikua ni kulinda nguvu kazi ambazo idara hii ilikua ikizipoteza mara tu magenge haya yalipoona maslahi yao yanahatarishwa, (kujua zaidi unaweza ukarejea kingo za sakafu za mzee Kapinga na Daudi Mwakawago and others of a like zilipoishia).

Kwa kuwa magenge haya yanawakilisha maslahi mapana zaidi ya mataifa ya kigeni yanayoangalia namna ya kubena rasilimali zetu na yenye mitandao ya nguvu ya kijasusi, seems yali smell something fishy with Apson na hapo ndipo tukatangaziwa the return of The Kingmaker ambapo tukasikia kuwa Apson anawekwa kando (thou it was too late) kimtindo and the Kingmaker took over.

Kwa speech ya Edward na kila kitu kilichoendelea pale na kinachoendelea ndani ya kambi yake I can draw the conclusion kwamba the Game is Over. Ninaanza kupata hisia kuwa kutakuwa na transition kubwa zaidi mwaka huu.

Tanzania inarudi katika ubora wake, this is my country, I belong here. Hakika moyo wangu una furaha sana kuliko wakati wowote ndani ya miaka hii kumi. Si jambo dogo kuachia nafasi kubwa kama ile katika ofisi nyeti wakati muda ukiwa unamruhusu na kuamua kwenda under cover, hakika napata hisia idara yetu bado ingaki hai na nguvu na makali yake.

NB: Hizi ni hisia zangu baada ya kuunganisha dots kadhaa. Hazina uhusiano na taarifa yoyote rasmi. Unaweza ukawaza tofauti na kuwasilisha au kuchangia kwa namna yako mimi sitakuwa na cha kuongeza wala kupunguza.
 
Mmmmh mkuu nimekuelewa ila sijaelewa huez ukakaa na nyoka kisha ukaendelea kumpa unga
 
Natamani sana Lowasa akataliwe CCM lkn sioni kama itakuwa rahisi kwa sababu kundi lake linaweza kuimaliza CCM kirahisi. Hili kundi lina mafia ambao kila uchaguzi wanabadilisha matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Kundi hili linajua namna gani CCM imekuwa ikishinda hama kihalali au kwa wizi. Itakuwa ngumu kuwapiga chini. Wamewaachia muda mrefu na sasa wanalitafuna taifa. Na tutalia sana.
 
Unaweza kuwa sahihi kiongozi.kwa mkutano wa el leo na jinsi alivyoongea,tena speech ya maandishi ni vigumu kuamini mkutano uliratibiwa na wataalamu kama huyu jamaa retired officer wa usalama wa taifa.napata mashaka sana kuna mchezo wa ajabu anafanyiwa huyu mzee Lowasa bila kujijuwa.
 
Mie nshavuta kiti nipo mbele kabisa naangalia hii drama ila najua watarukaaaa kwa Ukawa tunawachinja tu tena mapemaaaa
 
Kwakweli Epsode 01 was well played..na ujumbe wa kazi yake tumeupata.Tanzania haiwezi kuchezewa kirahisi rahisi kama wanavyofikiria wao..a very tricky game will be played ili turudi kwenye ubora wetu kabla ya ukoloni..Yakuitaiji uone mbali ili kuuelewa uzi huu!!
 
Back
Top Bottom