Sasa naanza kumuelewa marehemu Ibrahim Saidi "Sultan"

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
6,893
2,000
Jumanne ya March 10 mwaka 2009 kijana Ibrahim Saidi (pichani) maarufu kama "Sultani" alimzaba kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, wakati wa baraza la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee, tukio lililoibua taharuki kubwa ukumbini hapo na nchi nzima kwa ujumla.

Baada ya tukio hilo Mzee Mwinyi alisema amemsamehe kijana huyo, lakini Polisi walimkamata na kumfungulia mashtaka ya shambulio la kudhuru mwili. March 11 alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, ambapo alikiri kosa na kufanya shauri hilo kusikilizwa kwa siku moja tu kabla ya kutolewa hukumu.

Ibrahim alisema sababu ya kumtandika kibao Mzee Mwinyi ni kutokana na kuzungumzia masuala ya kondomu kwenye baraza la Maulidi kinyume na mafundisho ya dini yake. March 13 mwaka 2009 Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Neema Chusi, alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo alipewa nafasi ya kuiomba mahakama impunguzie adhabu lakini alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kumpunguzia adhabu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.
_
“Mimi ni kiumbe dhaifu, hakimu ni kiumbe dhaifu, na sote ni viumbe dhaifu mbele ya Mwenyezi Mungu. Siwezi kuiomba mahakama inipunguzie adhabu, ila namuomba Mwenyezi Mungu anipunguzie adhabu ya kaburi. Na kama akitaka nipunguziwe adhabu mnayotaka kunipa hakuna wa kuzuia” alisema Ibrahim.

Baada ya kutumikia adhabu yake kwa miezi 8 alipata msamaha wa Rais na kuachiwa huru, lakini June 02 mwaka 2019 alifariki dunia nyumbani kwake Mabibo Loyola jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.! #RIP_Ibra

Kutoka kwa Malisa GJ
FB_IMG_1594498807601.jpg
 
mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
11,092

Kutoka kwa Malisa GJ View attachment 1504098
Baadhi ya "testimonials" kuhusu Ibrahim Saidi (Sultani) aliyemzaba kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, March 10, 2009 wakati wa baraza la Maulid ktk ukumbi wa Diamond Jubilee.
___
Nimesoma nae Ilboru Sekondari, tulikua tukimuita "Man Ibra" enzi hizo. Alikuwa mwanaharakati thabiti wa dini ya kiislam na mara kadhaa amewahi kuadhibiwa kwa kilichoitwa utovu wa nidhamu kutokana na misimamo yake katika maswala ya mengi hususani ya kidini. Dr chriss Cyrilo
_____
Nimesoma naye Tabora Boys 2005/07 yeye akiwa PCM, mimi PCB. Alikuwa mtu wa utani na mcheshi. Kila muda anatabasamu na kibaragashia kichwani hata kama amevaa uniform. Alikua anashinda kwenye chumba msikitini, anasomea huko huko na akichukua chakula bwenini hakai na makundi ye fasta anarudi zake chemba iliyokuwa ndani ya msikiti wa shule. Parade kwake mwiko labda kama ataenda kufumushwa na mwalimu wa zamu huko msikitimi. Alikuwa anatembea na kitabu cha U.P (university physcics mda wote mkononi) na kazi yake ilikuwa kusolve maswali magumu. Na alifaulu vizuri kwa kupata division one. Dr.Semeni Nyerere
_____
Pale Tabora Boys kuna msikiti. Ulijengwa zamani sana wakati akina Lipumba wanasoma pale. Mwaka 2007 wakati Sultan akiwa form six alikua mmoja wa viongozi wa msikiti huo. Na alichukua hatua ya kutambua form 5 waislamu na kuwalazimisha kwenda msikitini kila ijumaa. Na alikua akipita mabwenini na kiboko kukagua kama kuna muislamu hajaenda msikitini, akikukuta unakucharaza bakora. @annonymous
___
Nimesoma nae IFM na alikua muumini mzuri wa dini ya kiislamu. Ilikua kila swala lazima ahudhurie pale msikiti wa Ocean riad. Alitakiwa amalize mwaka 2016 pale IFM. Lakini wiki moja kabla ya mitihani ya mwisho alikua ameanza kupata shida ya akili. Alikuja chuoni na akawafanyia fujo walinzi pale getini. Mvua ilikua inanyesha akavua baadhi ya nguo zake na kuanza kuzunguka maeneo ya Ocean Road akiigiza kama Traiffic barabarani. Since that day he became lunatic mpaka alipofariki. @ilolesezary
____
Namfahamu Ibra walikua majirani zetu Mabibo. Alikua mtu smart sana na mwenye misimamo. Inawezekana tatizo la akili lilimpata baada ya tukio la Mwinyi maana askari walipiga sana hasa maeneo ya kichwani. @annonymous
 
Sirdirashy

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
2,488

Nimeskitika tu hapo mwisho rest in peace Ibrahim
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,284
2,000
Acheni ujinga...huwezi kumpiga mzee vibao ujione shujaa upumbavu tu

Aache sasa na yeye kuongea pumba mbele ya hadhara! Wewe unaalikwa kwenye Baraza la Maulid unaongelea mambo ya condom! Wapi na wapi!!

Unaalikwa kwenye Mkutano wa Chama chako ili utoe neno, wewe unaleta masuala tata ya kuongeza mhula wa Urais kinyume kabisa na Katiba!

Kwa nini usichapwe vibao?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom