Sasa naamini Chadema haiwezi kamwe kutokomea kama vile NCCR, na CUF.


Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,410
Likes
26
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,410 26 0
Baada ya matukio yote haya serikali ya CCM inayowafanyia CDm, bado chama kinazidi kuwa imara na kuzidi kupendwa. Nawaomba mashushushu wa TISS waweke masiko yao kwa wananchi katika migahawa, vijiwe, mabasi, maofisini nk nk wasikilize wananchi wa kawaida wanasema nini kuhusu CDM, au wanasema nini kuhusu CCM.

Mashshushushu hao wakaripoti kwa wakubwa wao kile cha ukweli na wanaweza kuiokoa nchi.

Kikubwa ambacho wanacho CDM tofauti na CUF na NCCR ni viongozi mahiri na fedha. Yes fedha wanazo Chadema na hili linawakera sana CCM ambayo daima hupenda kuona vyama vya upinzani vikiwa fukara na fedha wawe nazo wao tu. Nakumbuka kati kati ya miaka ya 90 pale mgogoro mkubwa ulipoibuka ndani ya NCCR, serikali ya CCM kupitia msajili wa vyama iliamua kutoa ruzuku yao kwa faction moja ambayo ilikuwa pinzani na ya ile ya Mrema.

Sasa hivi serikali ya CCM haiwezi kutumia silaha hiyo ya ruzuku kwa Chadema, kwani Chadema inaweza kujimudu bila hata ya ruzuku.

Lakini hata hivyo CCM bado wanajaribu sana, lakini hawataweza.
 

Forum statistics

Threads 1,274,531
Members 490,721
Posts 30,515,493