Sasa mambo shwari!?....

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
....What about BoT's report? Would you make sure that Tanzania recovers $172 million that was paid to Richmond for nothing? What about the report from kamati ya madini? Would you be able to change all those fake contracts to make sure that Tanzania benefits from its natural resources? What about Ballali and all those responsible for BoT scandal are you planning to take any action against them?


Posted Date::2/13/2008
Rais Kikwete akiri nchi imetikisika baada ya kujiuzu Lowassa
* Asema sasa mambo shwari
* Ashukuru Pinda kukubali uteuzi

* CCM waandaa maandamano kumpongeza

Na Waandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa nchi ilitikisika kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri na kubainisha kuwa sasa hali imerejea kama kawaida.

Akihutubia wananchi Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana, Rais Kikwete alisema hali hiyo ilisababisha watu kukaa redioni na kuacha kufanya kazi na kusababisha wasiwasi mkubwa.

"Ni kipindi ambacho kilikuwa na shinikizo, wasiwasi mkubwa nchini, lakini sasa taifa limerudia hali yake kawaida," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Uamuzi ule ulileta mashaka makubwa sana, ulileta mtikisiko nchini. Makamu wa Rais (Dk Ali Mohamed Shein) alikuwa Tanga nikamwambia akatishe ziara yake na kuja hapa Dodoma..."

Alisema baada ya kuwasili kutoka Dodoma alikuta vumbi likitimka na kumfanya amwombe, kumwakilisha katika ufunguzi wa Kiwanda cha Chandarua cha A-Z, Arusha.

Rais Kikwete alisema, alipofuatilia mjadala wa bunge na kutafakari, vikao vya kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM na kamati ya wabunge wa chama hicho, walimuomba Lowassa kuwajibika.

Alimshukuru Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kukubali wadhifa huo na kwamba, angemkatalia ilikuwa ni kazi nzito na kuongeza kuwa, jinsi uteuzi wake ulivyopokelewa unaonyesha wananchi wana imani naye.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Pinda alisema upole wake atautumia kutekeleza matarajio ya Rais anayotegemea kutoka kwake ili yatimie na kwamba, imani ya bunge iliyoonyesha kwake anaamini ataweza.

Pinda alisema, baada ya kuthibitishwa bungeni ujumbe wa simu na simu zilizopigwa, ameamini kuwa wadhifa huo umetoka kwa Mungu.

Alitaja maagizo ambayo amepewa na Rais anayotakiwa kusimamia ni kutenganisha siasa na sughuli za biashara na kuangalia utaratibu mzuri wa jinsi ya kupata na kutumia fedha kwenye uchaguzi.

"Unakuwa na mgongano wa wasiwasi, kumbe ni hisia za wananchi…hili huwezi kulikwepa likitekelezwa vizuri litaleta heshima kwa chama chetu," alisema.

Pinda alisema, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bado ni tatizo katika utekelezaji wa Ilani ya CCM na kutangaza kuwa miaka miwili iliyosalia kuwa ni ya kufa na kupona.

"Huko ndo kuna fedha nyingi, na ndiko kuna matatizo na kero nyingi, huko ndiko kuna mtendaji wa kijiji anaona fahari kumchukua mzee asiye na hatia kumweka ndani, huko ndiko kuna mtendaji anajikopesha fedha za umma anavyotaka. Miaka miwili iliyosalia ni kufa na kupona kwa ajili ya kuibadilisha hali hiyo," alisema.

Kuhusu Richmond, alisema kama msaidizi wa Rais ameipokea kwa mtizamo chanya, huku akitaka serikalini kujihoji ili wasije wakaleta tena aibu, badala ya kuwaona walioandika ripoti kama maadui.

Katika hatua nyingine Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeandaa maandamano nchi nzima kuunga mkono jitihada za Bunge kufichua ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Taarifa ya Chama hicho iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari imesema kuwa CCM inampongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa kusimamia vizuri mchakato wa kujiuzulu Lowassa, kuvunja Baraza lake la Mawaziri na kuunda jipya.

"Ili kuunga mkono hatua ya Bunge ya kusimamia vema utendaji wa Serikali na pia kumwunga mkono Rais kwa mabadiliko aliyoyafanya ya uongozi serikalini, Chama Cha Mapinduzi kinaandaa maandamano katika mikoa yote," ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi, John Chiligati.

Taarifa hiyo imesema maandamano hayo yatafanyika katika mikoa yote nchini yakiwashirikisha wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwa Lowassa na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri ni dalili za kukua kwa demokrasia nchini jambo ambalo kila Mtanzania anapaswa kuliheshimu.

Katika hatua nyingine, CCM imempongeza Rais Kikwete kwa kuzingatia maoni ya wananchi kuhusu ukubwa wa Baraza lake la Mawaziri na kulipunguza kwa kiasi kikubwa katika uteuzi huo mpya.

Taarifa hiyo imesema kuwa CCM kimeridhika na uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri kwa kuwa umezingatia uadilifu, uchapakazi, uwiano wa kijinsia na pande zote za Muungano.

Chama pia kimetoa pongezi kwa Waziri Mkuu mpya Mizengo Pinda kikisema kuwa hakina wasiwasi juu ya uadilifu na utendaji wake wa kazi na kuwataka mawaziri wengine katika safu hiyo mpya kuiga mfano wake kwa maendeleo ya taifa.

"Tunawataka mawaziri walioteuliwa kuzingatia maadili ya taifa katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kutenda haki, kujali usawa, utawala bora, uzalendo na kujali maslahi ya wanyonge," ilisema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete leo saa 9:00 alasiri atazungumza na wazee wa Jiji la Dar es salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kuhusiana na mchakato mzima wa kujiuzuku kwa Lowassa pamoja na kuvunjwa kwa Baraza la Mawazili.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, John Barongo alisema Rais atazungumza na Wazee kama ilivyo kawaida kwa chama kunapokuwa na jambo lisilo la kawaida katika nchi.

Barongo alibainisha kuwa mazungumzo hayo hayatabagua itikadi za kisiasa na taarifa hizo zimesambazwa kwa wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam ili wawataarifu wazee walio nao katika wilaya zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom