Sasa kushusha bei nyumba za NHC hasara ni ya nani?

Uhalisia wa ujenzi, makazi bora, na ujenzi wa miji ya kisasa chini ya NHC ndio suluhisho pekee ya kuondokana na makazi duni na ujenzi holela kwa watanzania..

NHC ikipewa nguvu na wananchi wakapewa elimu ili mwisho wa siku wote tununue nyumba kupitia NHC with reasonable price kwa loans nafuu za mpaka 20-30yrs... Hili likifanyika basi watanzania wengi wataweza kumiliki nyumba na kuachana na ujenzi holela na mbanano wenye athari kubwa kwenye jamii..

Bado miji yetu imejengwa kiholela, vijumba visivyo na hadhi kutokana na umasikini wa watu wetu..hali imeifanya miji kutovutia na kuonekana uchafu na hata kuipa shida serikali yenyewe kwenye mipango yake mbalimbali..

Katika hili NHC wanaweza kuongezewa nguvu kwenye miradi na NSSF na mifuko mingine + uwekezaji binafsi wa estate agencies lakini msimamizi mkuu anaendelea kubaki NHC kwa maana ya ramani,mifumo na payments process..
 
Tena sio kuuzwa hata chini ya 40m, tugaiwe hata bure ikibidi, maana sisi wengine hatujawahi kula hiyo inayoitwa keki ya taifa,tunaishia kuona wengine wakilipwa mishahara minono na kutembea na maVX ya umma. Mimi sio mshabiki wa Magufuli na wala sitarajii kuwa mshabiki wake kwa lolote, lakini hizo nyumba akishusha bei nitamuunga mkono, kama nilivyomuunnga mkono alivyoondoa ile tozo ya wizi ya TANESCO kila mwezi eti service charge. Ashushe hizo bei za nyumba hata iwe chini ya milioni kumi, tukae kwenye nyumba za kueleweka.
Kweli mku nasisi wengine ndo tutafaidi matunda ya nchi yetu. Wengine wameendesha ma VX mpaka wanatesa mitaani. Uko very right. Wewe unataka hata ziuzwe chini ya hapo? Lakini siunajua hawa watu walichukua na mikopo kwenye mabenki ili kuzijenga hizo nyumba?
 
Hasara ipi wakati inajiendesha kwa kodi yako.
Jana nilisikia nyumba za National Housing kushushwa bei kwa mfano nyumba iliyokuwa imepangwa kuuzwa Tsh. 60 Million itauzwa chini ya Tsh 40 Million.

Moyoni nkajiuliza hilo pengo hapo katikati ni hasara kwa nani?
 
Mku ni kwasabau bei iliyopangwa toka hapo awali imeshuka kutoka Tsh 60 Million mpaka Tsh 40 Million. Huoni kuna hasara kati kati hapo?

Ili kujua kitu kina faida au kina hasara kuna vitu vingi vya kuangalia. Kwenye hili la nyumba kikubwa kuliko vyote ni gharama ya kujenga nyumba hizo. Kama gharama ya kujenga itakuwa kubwa kuliko bei ya nyumba kuuza basi kutakuwa na hasara. Lakini hata hapo ni lazima uwe mwangalifu. Kwa mfano, mfanyabiashara anaweza kukubali kula hasara kwenye bidhaa moja lakini akapata faida kubwa kwenye bidhaa nyingine na bado kiujumla akawa amepata faida. Kinyume chake pia kinaweza kuwa kweli.

Jambo la pili ni muhimu kujua kitu kinachoitwa "wigo wa faida" au "margin of profit". Hii nayo unaweza kuigawa katika vipande vingine vidogo vidogo katika kuelewa dhana nzima ya faida katika biashara. Kwa mfano, "faida" inaweza kuwa ya bidhaa moja, kundi la bidhaa za aina moja, biashara moja, au kampuni nzima n.k Kwa hiyo ukisema "hasara" ni lazima uwe mwangalifu unamaanisha nini.

Katika mjadala huu tunachukulia tu unamaanisha kuwa kwa vile nyumba zimepunguzwa bei basi umedhania kuwa gharama yake ya kujenga na kila kitu inapita bei hii mpya ndio maana unaona kuna "pengo". Mojawapo ya mambo mabaya ambayo hata mimi naweza kuyadhania ni kuwa kuna watu wanataka kupata faida ya asilimia 100 ya gharama yao ili waone wamepata faida. Kwa mfano, mtu anajenga nyumba kwa gharama ya milioni 25, halafu baadaye akataka kuiuza na kupata milioni 50 au milioni 100. Mtu akitaka kununua nyumba hiyo kwa milioni 35 huyo mtu anaweza asione hiyo ni faida. Biashara nzuri kitalaamu inatakiwa iwe na faida ya angalau siyo juu sana ya asilimia 20 ya gharama yake au siyo chini sana ya asilimia 5. Hizi zote ni faida. Na sekta zinatofautiana n.k

Kwa hiyo, kama wengine walivyosema hatujui na hujatupa sababu ya kujua kuwa kuna uwezekano wa kuwepo hasara hadi tujue gharama ya ujenzi wa nyumba hizo moja moja na kwenye mradi mzima.
 
Jana nilisikia nyumba za National Housing kushushwa bei kwa mfano nyumba iliyokuwa imepangwa kuuzwa Tsh. 60 Million itauzwa chini ya Tsh 40 Million.

Moyoni nkajiuliza hilo pengo hapo katikati ni hasara kwa nani?
Biashara ni ushindani hata hivyo zilikuwa zinauzwa aghali kuna makampuni mengi sasahivi yanayo uza nyumba
 
Je kama bei ya awali ilikuwa ni kubwa sana na faida kubwa mno?
Nafikiri hata hiyo 40m bado wana faida na sio hasara
Wao ndio wanajua zaidi
 
Kweli mku nasisi wengine ndo tutafaidi matunda ya nchi yetu. Wengine wameendesha ma VX mpaka wanatesa mitaani. Uko very right. Wewe unataka hata ziuzwe chini ya hapo? Lakini siunajua hawa watu walichukua na mikopo kwenye mabenki ili kuzijenga hizo nyumba?

Mkuu hii nchi ni tajiri italipa hilo deni la bank. Fuatilia zile nyumba za umma watu waliuziwa bei gani na ukubwa wa zile nyumba, na kumbukumbu wale waliouziwa kwa bei za kutupwa walikuwa na mishahara na marupurupu yanayowawezesha kujenga nyumba zao. Sasa ukitaka kujifanya mzalendo utaishia kukaa kwenye double room, kisha mkeo akikupa unyumba watoto wawe wanasikia maujuzi.
 
Watanzania sijui mnataka nini kipindi cha nyuma mlisema nyumba zipo juu, zimeshuka mnataka zipande wakati mnalia maisha magumu.
Kumbe zinashushwa bei kwavile maisha magumu! Kwanini hali imekuwa ngumu hivyo? Nilimsikia Majaliwa akishauri wahusika wa mradi wa nyumba za Kigamboni waangalie namna ya kupangisha nyumba hizo kwa wanafunzi wa vyuo.
 
Jana nilisikia nyumba za National Housing kushushwa bei kwa mfano nyumba iliyokuwa imepangwa kuuzwa Tsh. 60 Million itauzwa chini ya Tsh 40 Million.

Moyoni nkajiuliza hilo pengo hapo katikati ni hasara kwa nani?
Hakuna hasara wanapata faida kidogo tofauti na ilivyopangwa
 
Mku ni kwasabau bei iliyopangwa toka hapo awali imeshuka kutoka Tsh 60 Million mpaka Tsh 40 Million. Huoni kuna hasara kati kati hapo?

Amekwambia nani kama bei ikipangwa then ikashushwa ndio hasara?

What if Mwanzo hao NHC wali Over-priced hizo nyumba ili watengeneze Faida ya haraka
 
Mku ni kwasabau bei iliyopangwa toka hapo awali imeshuka kutoka Tsh 60 Million mpaka Tsh 40 Million. Huoni kuna hasara kati kati hapo?
chinga anaweza nunua kitu mia 500 na kupanga kuula 1000 ila badae bidhaa ikawa haitoki akaamua kuuza 800
kwan hiyo ni hasara mkuu?
 
Nasimama na mkurugenzi alietimuliwa, akijua bei lazima itashuka tu kama sio leo bas kwa wajukuu wetu. Dawa kwa wanasiasa wa enzi hiz ni kuyaporomosha tu majengo. Wakishindwa kutunga sera wezeshi kwa bei nafuu ni wao. Wajao watashusha. Bila hivyo hakungekuwa na jengo jipya hata moja la kuongelea.
Nikiingia madarakani nitamludisha Msechu NHC.
 
Jana nilisikia nyumba za National Housing kushushwa bei kwa mfano nyumba iliyokuwa imepangwa kuuzwa Tsh. 60 Million itauzwa chini ya Tsh 40 Million.

Moyoni nkajiuliza hilo pengo hapo katikati ni hasara kwa nani?

Hakuna hasara kodi ya 18% serikali wakitoa inatosha nyumba kushuka bei sijui kama umenielewa. Hizi nyumba zina kodi ya 18% ndani.
 
Back
Top Bottom