Sasa kushusha bei nyumba za NHC hasara ni ya nani?

Kikiwo

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,734
2,000
Jana nilisikia nyumba za National Housing kushushwa bei kwa mfano nyumba iliyokuwa imepangwa kuuzwa Tsh. 60 Million itauzwa chini ya Tsh 40 Million.

Moyoni nkajiuliza hilo pengo hapo katikati ni hasara kwa nani?
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,937
2,000
Zishushwe bei na ziuzwe kwa namna sahihi ili zinunuliwe kweli na wenye haki ya kuzinunua..
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
27,827
2,000
Tanzania Kwasasa Ipo Vema Maendeleo Hayana Chama
Uchumi Wa Kati
 

nalb

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
431
1,000
Kuna msemo "bora nusu shari kuliko shari kamili" sasa kama nyumba umepanga kuuza mil 60 na miaka inakwenda nyumba hazinunuliwi na zinazidi kuchakaa, wakati huo shirika halipati chochote kutokana na uwekezaji huo sasa si bora ushushe bei angaau upate hata hicho kidogo.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,240
2,000
..bei ya nyumba sawa na bidhaa yoyote inaweza kupanda au kushuka.

..na hali ya kupanda au kushuka kwa bei kunatokana na demand vs supply.

..inawezekana sasa hivi, kutokana na HALI NGUMU YA UCHUMI / KIPATO demand ya nyumba iko chini, wakati NHC wana nyumba nyingi[ supply] ambazo wameshindwa kuziuza kwa bei ya awali.

..Katika mazingira kama hayo, bei ya nyumba lazima ishuke, vinginevyo NHC wanaweza kuingia hasara kubwa na kushindwa kulipa MIKOPO waliyochukua ili kujenga nyumba hizo.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,539
2,000
Jana nilisikia nyumba za National Housing kushushwa bei kwa mfano nyumba iliyokuwa imepangwa kuuzwa Tsh. 60 Million itauzwa chini ya Tsh 40 Million. Moyoni nkajiuliza hilo pengo hapo katikati ni hasara kwa nani?
Kwanini unasema ni hasara? Unajua gharama za kujenga hizo nyumba zilikuwa kiasi gani?
 

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
5,977
2,000
Wana ccm watazigawana kama walivyogawana serikali za mitaa, kama huna connection sahau kuzipata.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,240
2,000
Nyumba zikiwa bei juu tabu, zikishushwa bei tabu, Watu kama wewe inatakiwa mpigwe risasi hadharani.

..usimlaumu.

..huenda yeye ni muwekezaji aliyekuwa ktk biashara ya kujenga na kuuza nyumba.

..kilichotokea ktk soko la nyumba Mabeberu huita " buyers market " yaani ni wakati mzuri kwa wanunuzi wa nyumba, na mbaya kwa wauzaji wa nyumba.
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,431
2,000
Nehemia ndiye aliyekuwa mkurugenzi na wakati huohuo mhasibu,na wakati huohuo Mwekezaji,,magu alitutonya kuwa kwenye kila eneo la mradi la Nhc,pembeni hakukukosekana mradi mwingine wa jamaa(asiyejulikanika)
Kwanini unasema ni hasara? Unajua gharama za kujenga hizo nyumba zilikuwa kiasi gani?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,961
2,000
Tena sio kuuzwa hata chini ya 40m, tugaiwe hata bure ikibidi, maana sisi wengine hatujawahi kula hiyo inayoitwa keki ya taifa,tunaishia kuona wengine wakilipwa mishahara minono na kutembea na maVX ya umma. Mimi sio mshabiki wa Magufuli na wala sitarajii kuwa mshabiki wake kwa lolote, lakini hizo nyumba akishusha bei nitamuunga mkono, kama nilivyomuunnga mkono alivyoondoa ile tozo ya wizi ya TANESCO kila mwezi eti service charge. Ashushe hizo bei za nyumba hata iwe chini ya milioni kumi, tukae kwenye nyumba za kueleweka.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,571
2,000
Ujawahi kuona abandoned housing projects au watu kuachana na mortgages zao kutokana na sababu za kiuchumi kama kushuka kwa bei za nyumba, low number of buyers and popular economic phrase ‘demand and supply’ at certain asking price.

Mfano wakati dunia ilipoyumba kiuchumi kuna wawekezaji waliacha investment za majengo nusu kisa bei za nyumba zilishuka ivyo ilikuwa ni bora kuingia hiyo hasara ya kuachana na nusu mradi kuliko kumalizia na kujiongezea hasara kwa sababu kwa bei waliyopanga kuuza hao wateja waliyeyuka ghafla.

NHC ishaingia hasara sio kwa sababu za uchumi bali CEO mmbovu aliyekuwepo anajenga bila ya kufanya marketing research kama hizo bidhaa zinawateja.

Hivi sehemu kama Kongwa ambapo millioni 1 unapata kiwanja kikubwa zaidi ya nyumba size walizojenga NHC na millioni 30 unajenga nyumba kubwa kutosha kabisa ni tutusa tu atakaeenda kununua nyumba ya NHC kwa millioni 40 Kongwa.

Kuuza hizo nyumba kwa bei che ndio solution ya ku-salvage kinachowezekana kulipa madeni na interest zake aliyowaachia yule CEO wao bogus ambaye watu walikuwa wanasifia safari yake ya kuitengenezea NHC madeni ambayo wengine walikuwa wakisema serikari itayalipa tu mbeleni kutokana uwekezaji mmbovu unaofanywa.

When it comes to government investment it is very easy to predict what will happen, siku ATCL wakitoa external audited financial statement ndio watu wataamka ata wale wanaosifia hizo ndege. Huo uwekezaji ni mmbovu na kuwatia umaskini watanzania hizo hela zinahitajika kwenye huduma muhimu za jamii haswa kwa wale wenye kipato kidogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom