Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Baada ya ushahidi wa Cohen, aliyekuwa mwanasheria binafsi wa Trump, sasa ni wazi kwamba Congress ya Marekani ambayo ina Democrats wengi zaidi itachukua uamuzi wa kum-impeach raisi Trump ili aondolewe kutoka madaraka ya Uraisi wa Marekani. Ni wazi Democrats wanasubiri ripoti ya Mueller anaechunguza kama Trump alishirikiana na Urusi ili kufanikisha kuchaguliwa kwake kuwa raisi. Kuna kila dalili kwamba ripoti ya Mueller itazidi kupigilia misumari kwenye jeneza la Trump, hivyo Democrats wanaisubiri ili kulipa suala la impeachment uzito unaostahili, zaidi ya ushahidi wa Cohen dhidi ya Trump.
Hadi sasa ushahidi wa Cohen kwa kamati ya Congress umeonyesha kwamba Trump amekuwa akidanganya na ana makosa ya jinai kutia ndani yanayohusu kodi na matumizi ya fedha kinyume cha sheria kipindi cha kampeni. Na pia kumekuwa na tuhuma za kutisha watu au taasisi mbalimbali ili wasitoe taarifa mbaya dhidi yake.
Kimsingi, Raisi wa Marekani hawezi kushitakiwa kwa makosa ya jinai akiwa bado raisi. Linalotakiwa kufanywa ni Congress kumuondoa madarakani kwanza kwa impeachment. Congress ikisha muondoa kwa impeachment, suala lake litapelekwa Senate ambapo kamati ya Senate itakaa na kupendekeza kwamba Senate ikae kama mahakama ili kuamua juu ya tuhuma zilizosababisha awe impeached na Congress. Ikiwa Senate itamtia hatiani Trump kutokana na sababu zilizofanya Congress imu-impeach, basi huo ndio utakuwa mwisho wa urais wa Trump.
Hata hivyo, ikumbukwe kwamba Congress inatawaliwa na Democrats, kwa hiyo suala la impeachment ya Trump ni rahisi sana. Senate inatawaliwa na Republicans kwa hiyo kuidhinishwa kwa impeachment ya Congress kwa kumtia hatiani Trump itakuwa sio rahisi.
Ikumbukwe kwamba Raisi Trump akiondolewa madarakani, Makamu wa raisi Mike Pence atachukua uraisi ili kumalizia awamu iliyopo. Na baada ya hapo anaweza kugombea uraisi awamu mbili zijazo, kwa kuwa hii aliyochukua uraisi toka kwa Trump haitahesabika kama ni awamu yake.
Kwa jinsi hiyo basi, Republicans wanaweza kuamua Trump aondoke ili kujipa nafasi za kushika uraisi kwa awamu tatu, hasa wakijua kwamba sio rahisi kwa Trump kushinda uchaguzi ujao kama asipoondolewa madarakani kwa impeachment.
Kwa jinsi hiyo, watakaofaidika na impeachment ya Trump ni Republicans! Democrats wakijua hilo wanaweza wasichukue hatua kum-impeach Trump ili wajitahii kumshinda uchaguzi ujao.
Source: Mimi mwenyewe kwa uelewa wangu wa siasa za USA