Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,869
- 16,916
Pamoja na wazee kukuusia uliacha yao mema
Alokuroga yu wapi alifanya yake kenda?
Unajifaragua kama kuku huku watimua vumbi
Leo kila mtu akucheka ngoma yako haikukesha
Omba yaishe salama Binti Mzingeri wa Leo
Mwanaisha Binti Mkambi mbona umezua Janga?
Angalia ulofanya kwa kuchanganya mabwana
Kama ungelijua hili mapema si ungewauliza wana?
Ona maisha uliyoachagua Una rafiki mmoja
Na kama wazazi hawakukufunza hii dunia hadaa
Daima tengeneza Maisha mema
Mwanaisha Binti Mkambi kila Kaya wachafua?
We si ulianza rusha mawe kwa jirani
Ulisahau wenzako wanaweza washa moto
Nyumba yako ya miti juu umezeka majani
Tulikwambia hapa mjini nenda taratibu
Ulitembea ukigagaruka kila kona mtaani