Sasa iwe Mwiko kutumia Quran na Biblia kuapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa iwe Mwiko kutumia Quran na Biblia kuapa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mzanganyika, Dec 11, 2009.

 1. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikitafakari kwa nini wanasiasa watumie vitabu vitakatifu kula viapo.

  Kiongozi anatakiwa aongozwe na katiba ya nchi na sheria za nchi sasa kwa nini ashike Biblia ama Quran kula kiapo-kwa nini asikamate Katiba anayoapa kuilinda na kama akikikuka ahadi hiyo atahukumiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi na sio Biblia wala Quran.

  Mwislamu ama mkristo unapokamata Quran ama Biblia na kuapa kwamba utailinda Katiba ambayo sheria zinaweza kugongana na kitabu chako kitakatifu unataka tukuelewe vipi?


  Pia naona ikomeshwe mara moja Bunge kuitwa Bunge tukufu-kwani wabunge wana utukufu gani? Kama wangekuwa watukufu wangetuacha sisi tulale na njaa wakati wao wanajilimbikizia vijisenti? wacha waitwe waheshimiwa na hiyo inawatosha lakini utukufu ukome mara moja.

  Nawakilisha.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hoja zako mujarabu.

  Vitabu vya dini sio muongozo wa kiserikali na wala havitumiki ktk kuendesha shughuli za kiserikali. Wazo zima la kutumia vitabu vya dini ktk kuapisha ni muflis na halina mantiki.
   
 3. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ni kwa sababu ya "Copy and Paste"
   
 4. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii natumaini makamba ameipata, Maana ndie aliyezoea kutumia vitabu vitukufu kutukana wanaoikosoa serekali!!
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  kama watu wangekuwa wanafata dini kwa dhati bac ilikuwa ni kitu kizuri sana, lakini kwa Tanzania wwengi ni wanafiki, hata kama mtu akiapa kwa hivyo vitabu still anafanya ushenzi kinyume na yanayompasa kufanya, hivyo inapoteza kabisa maana ya kapa
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii ni kuapa kuwa utakuwa na moyo mnyoofu hutaonea,kuiba,kudanganya n.k kama vitabu vitakatifu vinavyonena
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Hivi viapo wanavyokula kwa kutumia vitabu vya dini ni kiashirio cha unafiki wa watu. Utawasikia hao hao wanaoapa wakihubiri kwamba msichanganye dini na siasa huku wakiapa kwa vitabu vya dini. Pili wanaapa kwa mungu ambae nafsini mwao wanajua hawatawajibika kwa kumkiuka. Kwa watu wa dini kweli hasa wakristo wamekatazwa na Bwana wao Yesu kuapa na pia amesisitiza ole kwa atakaemwapiza nduguye kwani atastahili jehanamu ya moto. Sasa hii inawezekana kwa waamini waaminifu tu maana kamwe hutampata kwenye siasa kutakakomsababisha kuapishwa. Wala kumpeleka mwenzake kwenye mabaraza ya hukumu kutakakomlazimisha kula kia.
   
Loading...