Sasa imedhihirika wazi kuwa mtaji wa CCM siyo tena wananchi bali vyomba vya dola.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatamka wazi ya kuwa chanzo cha mamlaka yote hapa nchini ni wananchi. Hivyo panapojitokeza jambo lolote lenye utata chombo chenye madaraka yamwisho katika kumaliza utata huo ni wananchi wenyewe. Katika siku za hivi karibuni kulifanyika njama zenye lengo la kukinyima fursa chama cha CDM kutekeleza majukumu yake bungeni; kufuatia njama hizo CDM ikaamua kuwasikiana moja kwa moja na wananchi. Sasa tunaanza kusikia kelele kutoka kwa viongozi mbali mbali wa CCM wanaotaka vyombo vya dola kutumika ili kudhibiti CDM hisiwe na mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi. Jambo hilo likifanyika itakuwa ni matumizi mabaya ya vyombo vya dola, kwakuwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya vyama vya siasa na wananchi ni haki ya kila chama.
 
umeoona eeh wafuasi wao ni vyombo vya dola na baadhi ya vyama vya upinzani kama viongozi wa hivyo vyama nao walivyolaumu maandamano instead ya kujoin power ili pia wananchi wajue vyao na sera zao sasa tunawajua kwa upande mwingine kabisa kwamba ni reserve team ya CCM wakati wananchi washaichoka ccm
 
ccm huwaona wananchi wa maana kidogo wakati wa kura tuu!kura ikipita hawana jukumu la kumtumikia mwajiri wao bali ni kumkandamiza kwa kutumia dola
 
umeoona eeh wafuasi wao ni vyombo vya dola na baadhi ya vyama vya upinzani kama viongozi wa hivyo vyama nao walivyolaumu maandamano instead ya kujoin power ili pia wananchi wajue vyao na sera zao sasa tunawajua kwa upande mwingine kabisa kwamba ni reserve team ya CCM wakati wananchi washaichoka ccm
Vilio vya baadhi ya viongozi wajuu wa CCm na baadhi ya vyama vya upinzani vinanikumbusha bwana mmoja aliye hua wazazi wake wote wawili kikatili, na alipokuwa anahukumiwa kwa kusababisha vifo hivyo akamtaka jaji amsamehe ete kwakuwa ni yatima. Hayo ndiyo yanatokea kwa wakina Wasira na Cheyo; kimbunga cha maandamano ya CDm kimepitia majimboni kwao na kikakuta nyumba zao si imara, sasa wanahaha, na kutafuta visingizio badala ya kujilahumu wenyewe kwa kuwa mbali na wananchi
 
Back
Top Bottom