Sasa ifike mahali wakaa kimya wachunguzwe

the truecaller

JF-Expert Member
May 8, 2019
809
940
Nawasalimia wote!

NAMPA POLE SANA "KUB"

Naenda kwenye mada straight.

Matukio haya ya utekaji, upigaji risasi na mengine ya uvunjwaji miguu nchini yamezidi kuendelea.

Kwangu mimi siwezi kukubaliana na hoja za kwamba hii serikali inaweza kujua kama anavyodai tundu lissu na kundi lake.

Hakuna wajinga wa aina hiyo wanaoweza kuwemo Serikalini huku wakijua kitendo hicho ni aidha kibaya kwa kuiweka serikali kwenye picha mbaya zaidi duniani.

Ninachoamini ni kwamba kuna kundi la watu fulani ambao ni wabobezi wa matukio kama haya na wanachofanya ni timing nzuri na wakati muafaka wa kuichafua serikali hii kwa sababu wanazozijua wao.

Kuna watu humu walikwishasema waguswe ili wanuke, ni wabobezi pia wa mambo haya ya taaluma ya kuviziana, lakini pia walikwishasema nchi hii inapoteza muelekeo ki diplomasia.
Lakini pia enzi zao wakiwa kwenye makali ndio utekaji ulipoanza na kungoana meno pia na macho.

Watu hawa maarufu walikwishawahi kuahidi wakati wao ukifika wabaya wao wajiandae pa kutimkia.

Sasa wako kando na wako harakati kimyakimya.

Je, kwanini vyombo vyetu makini visifanye kazi na kuisafisha serikali kutoka kwenye tuhuma hizi za kishetani.

Hata kama wako kwenye mfumo, je kwa nini wasichomolewe tuwajuwe na tumuache JPM aendelee kutimiza safari yetu ya mafanikio?

Nawasilisha.
 
Jiandae kisaikolojia.
Wazee wa kutoana akili wanakuja mda si mrefu.

Kutokana na huu uzi, watakujibu kama hivi....

" Acha ujinga wewe, hujui kama hivyo vyombo unavyosema kuwa ni makini ndio haohao wanaotoa vitisho dhidi ya upinzani tena hadharani.
Niwangapi wame potea kujeruhiwa na hakuna uchunguzi uliokamilika, au acha ujinga wewe.
Huyo JPM ashasema kuwa, upinzani lazima ufe."

Zingatia:
Hayo maneno sio yangu, ila nimajibu ambayo nimeyapata kutoka kwa jamaa mmoja ambaye aliulizwa maswali kama yako.
Nakusihi usiwe na jazba.
 
Mbowe kaanguka kwenye ngazi kwa ulevi wao wanasema kapigwa yani mtu apigwe asiwe hata na kanundu usoni
 
Mbowe kaanguka kwenye ngazi kwa ulevi wao wanasema kapigwa yani mtu apigwe asiwe hata na kanundu usoni
Asubuhi mlisema kimada wa maisha club haikulipa sasa hivi mmehamia kwenye ulevi duh!!
 
Mapimbi ya lumumba yanajaribu kwa kila namna kupotosha ukweli lkn cku zote ukweli unabakia kuwa ni ukweli tu ..tukianza kulipiza kisasi msije kulalamika...kuanzia tegeni sikio..amini nawaambia
 
Safari yako na Nani?
Muda ufike muache kutumia jina la Mzee wa Watu kwa maslahi yenu binafsi.. Kipindi kile alikua waziri mlikua hamumuoni?.. Sasa hivi kila kitu Mh.Raisi.. hamna mapya, Hakuna Sera wala Ubunifu.. Acheni kutembelea Nyota ya Raisi Magufuli

Anayoyafanya Hamkuweza kuyafanya kwa karibia miaka ishirini huko nyuma saizi mnaleta Unafiki kisa NJAA.. Nyinyi!!!!
 
Back
Top Bottom