Sasa hizi Pikipiki Toyo ni janga hapa A Town! Ni janga kubwa jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa hizi Pikipiki Toyo ni janga hapa A Town! Ni janga kubwa jamani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LiverpoolFC, Jan 27, 2012.

 1. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Jana majira ya saa mbili kasoro usiku pale Sanawari kwenye taa.
  Palitokea ajali ya pikipiki Toyo kuikatizia gari aina ya Fuso na dereva toyo kufa palepale na isitoshe ile pikipiki kukanyagwa na kuwa kama chapati vile.

  Na ndipo washikaji wakaanza kumfukuzia jamaa wa fuso aliyeelekea barabara ya Moshi bila ya mafanikio.
  Ikiwa hilo halitoshi,majira ya saa nne kasoro dk kidogo,Gari aina ya landcruiser ilimkatizia mwendesha toyo mwingine na kumwua hapo hapo kwenye mataa Sanawari.

  Na ndipo wadau wa Toyo wakaanza kumfukuzia jamaa na landcruiser yake na wakafukuza mpk kule Ngaramtoni ya juu na walipofika pale Sauti ya Injili Dereva wa Cruiser akaamua kugeuza na ndipo akalipeka mpaka central police ya Arusha kusudi ajinusuru na madereva toyo waliokuwa na hasira mithili ya Mbogo aliyejeruhiwa.
  Lakini ukiangalia gari yenyewe imepasuliwa vioo hakuna hata moja.

  Na ndipo police wakawa na kazi ya ziada ya kuwapooza hao washikaji na wakawa wamepoa.
  Sasa Mi najiuliza hawa wajamaa wa Toyo wataelimika lini?
  Ukiangalia hapa A town hakuna siku inapita bila ya ajali ya Toyo.

  Hakika imewapunguza vijana hapa town kbs!
  Sasa sijui dawa itakuwa ni nini.

  Nawasilisha!!
   
 2. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwengine juzi kati kaangukiwa na tawi la mti barabara ya mahakamani.
  Kitendo cha kusubiri dakika 1 mti ukatwe, yeye kajipitisha kwa kiburi.
  Ndio ikawa mwisho wake.
   
 3. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  ndugu ndo unajua leo?nilivyokua mt.meru hospital ukikaa zamu usiku lazima upate wagonjwa zaidi ya kumi wa toyo na lazima polisi wakuletee maiti kama tatu kwa siku kutokana na ajali za toyo....its a disaster
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa nao wamezidi na TOYO zao, hafuati sheria kabisa
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Siyo sheria tu!

  Wamekuwa vile vile ni kama desturi ya wao kusababisha ajali!
  Tuwaonee huruma hawa vijana wajamen!
   
 6. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amen.
  Mkuu LiverpoolFC ni jambo la kushitua na kushangaza...kwa usiku mmoja watu wawili tena toyo wamepoteza maisha sehemu hiyo hiyo? ni makosa ya hao waendesha TOYO au ni makosa ya waendesha magari? au ni miundo mbinu ya uwekaji wa hizo taa ndo umekosewa? Hizi toyo zitawamaliza vijana na kuwaachia wengi vilema vya maisha. utoaji wa leseni kwa waendesha toyo nadhani ufanyiwe uchunguzi ikiwa sambamba na elimu kwa waendesha TOYO wajue sheria za barabarini na wazifuate
   
 7. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Madereva wa toyo huwa wanakula sana vijiti vya A - Town ambavyo ni vikali sana na hupelekea kupoteza uwezo wa kuona vizuri; let them try Kitu cha Mara bana.
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa!

  Inaweza ikawa ndiyo chanzo kuu kweli?
  Maana kama ni kula hakika wanaipeleka haswa!
   
 9. E

  ENGINE CONTROL Senior Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha kusikitisha hapo waacheni wafe tuu wakibanwa na kupewa mwongozo watu wanang'aka na kuona kama wanaonewa.

  Hawa jamaa wengi wao wakiweza kuipeleka mbele tu ndani ya dk 2 unawakuta barabaran tena wamepakiza abiria.
  Hawa madereva wa toyo ni wapuuzi sana na sema waachen wafe ili wajifunze.
   
 10. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Makumira pale kwa ngai juzi kagongwa mwingine, hatima yake sikuifaham japo aliumia sana
   
 11. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inawezekana maana ya TOYO ikawa ni KIFO
  Anayefahamu maana yake tafadhali iweke hapa.
   
Loading...