Sasa hivi Magufuli hata ukimsimamisha na Pierre Liquid lazima Magufuli ashindwe kwenye sanduku la kupigia kura.

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Waungwana hamjambo!
Ukweli lazima niuseme daima, Magufuli hapendwi na makundi karibia yote.

Mimi kwetu kusini mkoa wa Lindi, kila ninayemuhoji hana mpango naye, Mbeya ninalima viazi, hivyo nakwenda mara kwa mara kuliko hata nyumbani Lindi, nako wakulima hatumpendi, maisha magumu.

Dar nafanya kazi, ukiondoa BOSS karibu watumishi wenzangu wote hatumpendi Magufuli, boss ni siri yake. Sijui kama anampenda au la.

Nimefilisika kaduka kangu cha bidhaa mchanganyiko hapa dar kwakukosa wateja. Wafanyabiashara wadogo Dar hatumpendi, sijajua hao wafanyabiashara wakubwa kama wanamkubali au la.

Kama kura ndio ingekuwa mwamuzi hapa Afrika 2020 hata 30% Magufuli haiokoti.

Anaonekana anakubalika kwa propaganda za wachache ambao wanatumia media kumsifia. Na media zote sasa wanajikomba kwake ili waendelee Kusurvive.

Hata ukiweka dongo hapa na baba Jesca pale Mimi nitalipigia kura dongo.
 
Back
Top Bottom