Sasa hivi dispensary za kata za Serikali unalipia kila kitu. Hakuna tofauti na hospitali binafsi. Tozo tunazokatwa za kazi gani sasa?

BIMA, BIMA, BIMA ndio jibu. Sasa hivi iko bima ya kila saizi na ya uwezo wako kwa wananchi wote. Waziri Ummy alipokuwa Afya alimaliza mzizi wa Fitina katika kufanikisha mpango wa BIMA kwa watanzania wote. Ni uamuzi wako tu kama unataka kulipa kila ukiienda zahanati au unalipa bima mara moja kwa mwaka.

Kuna bima za aina nyingi, kwa mfano ya Mwanafunzi, Familia, mtu mmoja pekee ya vikundi n.k. Ya mwanafunzi ni 50 elfu kwa mwaka. Wahi kakate BIMA.
Hivi jamani bima ya tanzania ina operate vyenginevyo? Maana kwa nchi nyingi nyengine, kila ukitumia bima yako unapofika muda wa ku renew bei yake hupanda, sasa nashangaa kuona watu wanashauri wenzao wawe wakitumia bima zao za afya kilaini kabisa.
 
Sasa kaka. Acha tuwahurumie viongozi wetu waendeshe V8 za 500,000,000.
Na ikifika wakati wa uchaguzi tuhakikishe tunawachagua hao hao tena bila kujali maumivu tunayoyapata juu ya namna wanavyoongoza nchi na kututungia sheria zisizo na kichwa wala mguu!
 
Zerikali za Kiafrika zina laana.
Kodi wanakusanya
Misaada wanapewa
Mikopo rahisi wanapewa
Rasilimali lukuki
** Wananchi wanaishi kama ndege**
SHULE, SHULE, SHULE ndugu yangu. Umande usitutishe. Pesa ya Kodi, inajenga majengo, inanunua vifaa, inalipa mishahara na kukarabati vifaa na majengo. Mkopo hata ukiwa wa masharti nafuu lazima ulipwe kupitia kodi yako, Misaada- hao watoaji wanaelekeza wenyewe iende wapi, huwezi kuwapangia- kwamfano, ukuzaji wa demokrasia, kuinua uchumi wa wanawake, maji n.k.

Ngosha unayeumwa huko haupo kwenye pesa ya msaada ulie tu. Rasilimali zinajenga barabara, madaraja, vifuko n.k
 
Hivi jamani bima ya tanzania ina operate vyenginevyo? Maana kwa nchi nyingi nyengine, kila ukitumia bima yako unapofika muda wa ku renew bei yake hupanda, sasa nashangaa kuona watu wanashauri wenzao wawe wakitumia bima zao za afya kilaini kabisa.
Kila nchi inautaratibu wake. Hapa haipandi unakata kwa pesa ile ile. Msiogope BIMA ndio habari ya mjini kwa sasa.
 
SHULE, SHULE, SHULE ndugu yangu. Umande usitutishe. Pesa ya Kodi, inajenga majengo, inanunua vifaa, inalipa mishahara na kukarabati vifaa na majengo. Mkopo hata ukiwa wa masharti nafuu lazima ulipwe kupitia kodi yako, Misaada- hao watoaji wanaelekeza wenyewe iende wapi, huwezi kuwapangia- kwamfano, ukuzaji wa demokrasia, kuinua uchumi wa wanawake, maji n.k.

Ngosha unayeumwa huko haupo kwenye pesa ya msaada ulie tu. Rasilimali zinajenga barabara, madaraja, vifuko n.k
Ni sahihi kwenye zahanati za serikali mwananchi kutozwa sawia na kuwango ambacho angetozwa kwenye zahanati za binafsi?
Kumbuka huyu mwekezaji wa private dispensary analipa Kodi, analipa mishahara, ananunua dawa , hana misaada, tozo n.k analipa
 
Tatizo wewe kichwani huna akili. Kwa hiyo kazi ya serikali ni nini sasa?
Wewe upo dunia gani? Hadi leo unataka serikali ikutibie mkeo!!! Hii nchi bado tunasafari ndefu, ila kama kazi yako ni sawa na hilo jina lako siwezi kukulaumu
 
Ni sahihi kwenye zahanati za serikali mwananchi kutozwa sawia na kuwango ambacho angetozwa kwenye zahanati za binafsi?
Kumbuka huyu mwekezaji wa private dispensary analipa Kodi, analipa mishahara, ananunua dawa , hana misaada, tozo n.k analipa
Mkuu achana naye huyo jamaa atakuchosha tu.
 
Kwa hiyo serikali inadanganya inaposema tulipe kodi na tozo ili iboreshe huduma za afya?
Unaelewaje hilo neno KUBORESHA. Hilo neno halimaanishi BURE.

Kwa msaadatu, hapa serikali ilimaanisha:
  • Kusogeza huduma karibu na mwananchi (ujenzi wa vituo vya afya)
  • Ukarabati wa majengo na ununua wa vifaa
  • kuwaelisha wafanyakazi ili watoe huduma bora zaidi
 
Wewe upo dunia gani? Hadi leo unataka serikali ikutibie mkeo!!! Hii nchi bado tunasafari ndefu, ila kama kazi yako ni sawa na hilo jina lako siwezi kukulaumu
Natumaini boss una mkwanja mrefu sana maana si kwa dharau hizo. Hongera.
 
Unaelewaje hilo neno KUBORESHA. Hilo neno halimaanishi BURE.

Kwa msaadatu, hapa serikali ilimaanisha:
  • Kusogeza huduma karibu na mwananchi (ujenzi wa vituo vya afya)
  • Ukarabati wa majengo na ununua wa vifaa
  • kuwaelisha wafanyakazi ili watoe huduma bora zaidi
Tumia akili hata kidogo basi. Unaponisogezea huduma karibu ilihali sina uwezo wa kuzinunua inasaidia nini? Si bora niende hospital binafsi.
 
Basi haina haja ya kwenda kwenye hosptali za serikali. Bora uende private hospital tu kule kunakojulikana huduma ni ya kulipia.
Hakuna sherti eti lazima ukatibiwe serikalini. Hili ni swala la uamuzi wako na familia yako, kama unavyoamua kumpeleka mtoto wako shule binafsi japo kafaulu na kachaguliwa kujiunga shule ya serikali.

Ila nakuhakikishia kuwa hospitali/dispensary za serikali bado zitajaa tu.
 
Kwa hiyo ni halali kwa viongozi kununua magari ya 500,000,000 badala ya kutoa huduma za afya bure?
 
Kila nchi inautaratibu wake. Hapa haipandi unakata kwa pesa ile ile. Msiogope BIMA ndio habari ya mjini kwa sasa.
Wow huo ni mfumo mzuri bali ni wa kushangaza, maana Bima ni biashara, sasa sijui ni vipi wemye kuendesha bima wanajipatia faida ikiwa kila siku kazi yao ni kuwalipia wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu kila siku na kupindukia na walicholipa kwenye bima.
 
Back
Top Bottom