konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,666
- 8,582
Leo nimempeleka wife kumfanyia vipimo na matibabu nikidhani labda kwa sababu ni dispensary ya serikali huduma itakuwa bure lakini cha kushangaza kila kitu unalipia. Kuanzia kumwona daktari unalipia. Vipimo vyote unalipia, dawa zote unalipia. Kiufupi kila kitu unalipia kwa 100%.
Sasa nimeshindwa kuelewa serikali inaposema tunalipa kodi na tozo ili kuboresha huduma za afya. Huduma gani wanaboresha kama kila kitu tunalipia? Hii nchi sijui imelogwa na nani?
Sasa nimeshindwa kuelewa serikali inaposema tunalipa kodi na tozo ili kuboresha huduma za afya. Huduma gani wanaboresha kama kila kitu tunalipia? Hii nchi sijui imelogwa na nani?