Sasa COSOTA yatia aibu kwa njaa kali mtaani

Alagwa

Member
May 30, 2012
95
85
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa Mwenyekiti wa chama cha haki za wasanii (COSOTA) akishirikana na jeshi la polisi wamevamia stationari zilizopo wilayani Mbulu Mkoanai Manyara na kukusanya Computer zote zilizo kuwa zinatoa huduma mbalimbali ndani ya wilaya bila hata ya kujali huduma inayo tolewa katika eneo husika.
Kwa kifupi ni kwamba mwanamke huyo anatembea na zaidi ya askari 5 wakiwa na bunduki na wanachokifanya wakifika mahali wakiona computer wanasema hii computer inakazi zetu bila hata ya kuhakikisha au kukagua wanamlazimisha aliyoko ofisini kubeba computer wanaichukuwa sasa wamechukua hadi za shule ya computer iliyopo hapa wilayani.
Kilichotokea baada ya hapo wamezipeleka kituo cha polisi nilipo fuatilia kwa undani wahusika walichukuliwa na computer zao wametishiwa kuwa walipe laki tano kila mmoja au wafikishe mahakamani huku mwanamke huyo nilipo jaribu kumhoji kiundani alionekana kutojiamni kwa anacho kifanya.
Wana jamii Ivi ni kosa kimiliki computer ?
Ivi COSOTA wanaruhusiwa kufunga kazi za watu bila ya uhakika wa hizo wanazo ziita haki zao?

Je jeshi la polisi linatambua kazi wanayo fanya?

Bado sakata linaendelea nitawajuza zaidi
 
Pamoja na kwamba unalalamikia zoezi hilo, wakikukuta hata na wimbo mmoja tu katika PC yako ambao huna maelezo ya jinsi ulivyoupata, nadhani wataanzia hapo kukushikisha adabu. Najua wengi tuna nyimbo kwenye PC zetu, ambazo hatujazipata kihalali. Naomba uje na jibu la kitakachofuatia hapo. Copyright ni ishu kubwa sana, sio malalamiko tu. Anachokifanya huyo jamaa ni kile kile anachokifanya Alex Msama pale Dar. Kumbuka kwamba hata kupiga kopi vitabu ni makosa ya kukiuka copyright.
 
Back
Top Bottom