Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
RASMI: BUNGE SASA NI IDARA YA IKULU
Zaidi ya asilimia 70 ya wabunge wote kwenye Bunge letu, wanatoka CCM. Kitendo cha MKATA UMEME kuwadhibiti wabunge hawa ni sawa na kudhibiti Bunge zima ili lisiwe na meno.
Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la leo, MKATA UMEME alikutana nao jana pale Ikulu ya Dom na kuwapiga mkwara mzito akiwataka wafanye kazi ya kulinda maslahi ya chama.
Amewaambia hawapaswi kuchangia kwa kuipinga serikali hata kama inaboronga.
Amewaambia marufuku kushirikiana wabunge wa upinzani.
Amewaambia ni marufuku mbunge wa CCM kumwachia muda wa kuchangia mbunge wa upinzani.
Amewathibithibitishia mbele ya Spika Ndugai kuwa yeye ndiye aliyezuia BUNGE LIVE kwa kuwa anakerwa na jinsi wapinzani walivyokuwa wakipata umaarufu kupitia Bunge live.
Amewapa Onyo wabunge waliokuwa wanapanga kwenda kumtembelea mbunge wa upinzani Godbless Lema gerezani,
Amemshtaki kwa baba yake mbunge mmoja binti ambaye inasemekana huwa anavujisha mambo yao kwa wapinzani.
Amewaonya wabunge waliokuwa wanapanga kuandaa hoja ya kumng'oa waziri mkuu,
Baadaye akawaambia waseme shida zao za majimboni kwao TU, wakazisema, akawaahidi kuzishughulikia (UBAGUZI)
Kimsingi MKATA UMEME anachokifanya ni kulitawala Bunge liwe KIBOGOYO kwa kuwapandikiza roho yake ya CHUKI, UBAGUZI na VISASI wabunge wote wa chama chake huku akitishia kulivunja Bunge ili wote warudi kwenye uchaguzi endapo wataenda kinyume na anachokitaka.
Je, hapo tuna BUNGE au IDARA YA IKULU?