Sasa bunge la jamhuri limeteza uhalali kama hata mambo ya msingi kama katiba yatafanywa kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa bunge la jamhuri limeteza uhalali kama hata mambo ya msingi kama katiba yatafanywa kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibori, Nov 16, 2011.

 1. K

  Kibori Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wanzangu Tumekwisha.

  Imani yangu ni kwamba Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa limepoteza/litapoteza hadhi na heshima kama jambo kubwa sana kama hili la kikatiba linapelekwa kisiasa zaidi kama ambavyo tangu juzi sote tulivyoona. Sisi nashindwa kaamini kwamba lakini zaidi nimeshangazwa na mambo makuu yafuatayo;

  1. Majina ya wabunge waliopo kwenye kama ya kudumu ya bunge ya sheria, bila shaka kuna washeria waliobobea na wapambanaji wazuri tu, lakini cha kushangaza ni kwamba ripoti yao haifananii hata kidogo ni madudu kwa lugha nyingi. Kwanza kuelendela kuisupport serikali kwa mswada ule mmbovu ni hatari sana kwa nchi.

  2. Repoti ya Kambi ya upinzani kwa kweli imeandikwa kwa ustadi mkubwa wa kisheria, kiufundi na kimaudhui. Kila point alinamshiko mkubwa sana kisheria lakini cha kushangaza ni kwamba hakuna hata mbunge hata mmoja aliyechangia mpaka sasa kwa kutoa mchango unaojikita katiba points aidha za kukosoa au kuikubali chochote kilichoandikwa na kampi ya upinzani. NO BODY kwanini ? ni siasa tu . Hii ni hatari sana kwa nchi na kwa amani na utulivu wa nchi yetu.


  Naomba kutoa hoja kwamba kwa mtindo huu wa kisiasa ambayo imedhihiridhwa wazi na bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni hatari sana kwa nchi na kwa taifa katika siku za usoni. Kwa njia hii nachelea kusema kwamba bunge sasa limekosa uhalali na halistahili tena kuaminiwa kama chombo huru cha kuwaakilisha watanzania wenye nia na kiu kubwa ya kupata katiba mpya. Naomba kutoa hoja !!!


  TUFANYE NINI KWA SASA NDILO SWALI KUBWA


  Mimi binafsi napendekeza yafuatayo
  1. Wataanzania sasa tusimame imara na kwa pamoja kupinga kuburuzwa katika zoezi hili muhimusana la katiba mpya; tushikamane na wanaharakati kupinga serikali kupitisha mswada ambao bado haijakidhi matarajio na matakwa yetu kama Taifa. Tupinge Bunge letu kwa kupoteza uhalali wa kusimamia serikali na kuwaakilisha watanzania. Bunge ambalo baadala ya kushughulikia mambo ya msingi yenye tija kwa watanzania; wanaendeleza na kuendekeza siasa zao za vyama. CCM vs. CHADEMA. Katiba ya Tanzania ni juu ya vyama vya siasa lakini zaidi WATANZANIA ni muhimu zaidi kuliko vyama vya SIASA. Siasa za vyama katika swala la KATIBA ya NCHI-SHERIA MAMA hazina na hazitakuwa na nafasi kubwa katika zoezi kubwa kama hili bali ni WATANZANIA wenyewe. Hapa tusimame tuseme HAPANA.
  2. CCM waliendeleza ubabe na wingi wao na mshikamano wao, (ndoa yao) )katika swala la katiba ni sisi kama WANANCHI TUSIMAME TUSEME HAPANA....WABUNGE WA CCM NA WASHIRIKA WAO NI KWELI NI WENGI KATIKA BUNGE NA WANAWEZA KABISA KWA ULEVI TU...WA USHABIKI WA SIASA ...WAKAPITISHA JAMBO HILI. MIMI NAAMINI KWAMBA SIO WENGI KULIO WATANZANIA, TUKISEMA HAPANA NI HAPANA.
  3. NAJUA POLISI NA VYOMBO VYA ULIZI PENGINE VITATUMIKA LAKINI TUSIMAMA SOTE KWA PAMOJA KAMA " UMMA" POLISI NA RISASI NA MABOMU YAO HATASAIDIA SANA ...HATUTAKI WALA SIOMBI HILI LITOKEE LAKINI KAMA WENYE MADARAKA WANGALIJUAHILI MAPEMA HAKUNA ULAZIMA TUFIKE HUKO. NI BUSARA ZAO. SERIKALI IKIAMUA KUWAPIGA WANANCHI WAKE KWA KUWAZUIA KUPINGA JAMBO LAO SERIKALI ITAKUWA IMEKOSA UHALALI WA KUONGOZA WATU .....NI SHAKA WAKAE PEMBENI ...MADARAKA YANATOKA KWA WATU/WANANCHI KAZI WALIZOOMBA NA KUAPA KULINDA NI KUFANYA YALE TUNAYOTAKA SISI WATANZANIA.
  4. MSIMOMO WETU KAMA WANANCHI NDIO TU KITAKACHO TULETEA KATIBA TUNAYOITAKA, SAA YOYOTE NA MUDA WOWOTE; SIO BUNGE, WALA CCM WALA SERIKALI WALA VYAMA VYA SIASA AMBAVYO WAKATI WOTE NI SIASA TU BALI NI WATANZANIA WENYEWE.
  NAOMBA KUTOA HOJA !!!

  i STAND TO BE CORRECTED !!!
   
 2. V

  Vatoi Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi itabidi Cv za kila mmoja zichunguzwe labda tutajua undani kwa nini mambo hayaendi. Tatizo ni elimu ndogo au.....
   
 3. V

  Vatoi Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila nina wasiwasi na CV ya Mnyika na.....
   
Loading...