Uchaguzi 2020 Sasa & Baadae: Pigia kura chama chenye sera inayogusa maisha yako

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
769
1,000
Habari Tanzania!

Kura & Uhusika: Hii ni kwako wewe ndugu mtanzania na kwa wale wote wanaohusika na upigaji kura. Nakuomba kwa kukuwekea msisitizo ewe mpiga kura na Mtanzania tafadhali sana, hakikisha unakwenda kukipigia chama chenye mgombea mzuri, makini na ambaye mwenye sera safi inayogusa na kuakisi maisha na mahitaji yako; jiepushe na ushabiki; kumbuka hayo ni maisha yako na taifa lako ulipendalo.

Sasa: Wananchi tumebahatika kwa usawa na pamoja kusikiliza sera na ahadi juu ya nini vyama vitatutendea tukivipa nafasi kupitia kura. Kazi ni kwako. Jiangalie wewe, jirani, ndugu na jamaa yako kuhusu mahitaji na maisha yenu ya kidunia.

Mwisho: Nawatakia watanzania wote amani, upendo na usawa sahihi katika upigaji kura nchi nzima. Mungu awatangulie kila mmoja kwa namna itakavyompendeza Mungu katika mapenzi yake.

"Tanzania ni nchi nzuri sana; Tanzania inapendeza sana kwa mambo yote; Tanzania ni tulizo la moyo wako".

Bye.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,582
2,000
Bima ya afya kwa wote

Kurudisha FAO la kujitoa

Kuondoa kikokotoo cha Magufuli

Kura kwa Chadema

Viva Lissu
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
5,584
2,000
Ni yeye 2020.

Nani kama yeye? Utamlinganisha na asiyejua haki za wanawake nazo ni human rights?

Haki, uhuru na maendeleo.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
5,584
2,000
Ni yeye 2020.

Nani kama yeye? Utamlinganisha na asiyejua haki za wanawake nazo ni human rights?

Haki, uhuru na maendeleo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom