Sare feki za jeshi zakamatwa kambi za wakimbizi Kigoma

NGolo Kante

Member
Feb 28, 2017
80
131
IMG_20190110_191814.png

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo mkoani hapa, imekamata nguo zinazofanana za sare za kijeshi katika makambi ya wakimbizi.

Akizungumza na waandishi na kamati hiyo mjini hapa leo Alhamisi Januari 10, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Samson Hanga, amesema nguo hizo zilikamatwa Desemba 31 mwaka jana kati saa tano asubuhi hadi sita mchana kwenye kwenye makambi ya wakimbizi.

“Jumla ya nguo zinazofanana na sare za kijeshi 1,947 zilikamatwa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli na Nduta zote za hapa hapa Kigoma.

“Katika Kambi ya Nduta zilikamatwa sare 1,325 na Mtendeli 622,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini walioingiza sare hizo na lengo lao.
 
January 13, 2019

Viongozi Wizara ya Mambo ya Ndani wasimamishwa kazi :

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Alphaxard Kangi Lugora ameamua kuwasimamisha viongozi mbalimbali waliopo ktk idara ya Huduma kwa Wakimbizi wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ya Tanzania. Bw. Kangi Lugora alisema viongozi wa idara hiyo ya Huduma za Wakimbizi walitegemewa kuwa macho na masikio ya serikali kubaini masuala yanayohusu usalama, lakini viongozi hao walishindwa kuzuia 'msaada' huo wenye mali haramu kufikia kambi hizo.

Bw. Kangi Lugora amebainisha kuwa wakimbizi ktk makambi hayo magharibi ya Tanzania walikuwa warudi makwao hivi karibuni. Hivyo uwepo wa sare za kijeshi miongoni mwa wakimbizi ungezua hali hasi kutoka serikali ya Burundi kuwa Tanzania inataka kuanzisha vurugu kwa siri kupitia wakimbizi hao wakifika Burundi. Mbali ya kuzua uhusiano hasi pia mavazi hayo yangewezesha serikali ya Burundi kuwakatalia wakimbizi hao kurudi nyumbani kwao Burundi.

Waziri Kangi Lugora akielezea kwa undani sakata la shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na kampuni ya kijapani UNIQLO ndiyo walioleta marobota ya nguo kama msaada kwa wakimbizi huku ktk marobota kukiwemo nguo za kijeshi.

Mgao huo wa nguo zikiwemo nguo 1,947 zinazofanana na sare za kijeshi kwa wakimbizi wilayani Kakonko na Kibondo mkoani Kigoma.

Source : Kwanza TV
 
Vigogo 5 idara ya Huduma ya Wakimbizi wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wasimamishwa kazi kutokana na sakata la sare za kijeshi zilizokutwa ktk kambi za Wakimbizi wa kutoka Burundi
  1. Harrison Mseke - Mkurugenzi Idara ya Huduma za Wakimbizi
  2. Deusdedit Masusu - Mkurugenzi msaidizi upande wa menejimenti ya makambi ya wakimbizi
  3. Selemani Mziray - mkurugenzi msaidizi usalama na operesheni kambi za wakimbizi
  4. Peter Bulugu - mkuu wa kambi la wakimbizi Nduta.
  5. John Mwita - mkuu wa kambi ya wakimbizi Kakonko.
  6. Tony Lazier - mratibu kambi za wakimbizi kanda ya Kigoma.
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo mkoani hapa, imekamata nguo zinazofanana za sare za kijeshi katika makambi ya wakimbizi.

Akizungumza na waandishi na kamati hiyo mjini hapa leo Alhamisi Januari 10, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Samson Hanga, amesema nguo hizo zilikamatwa Desemba 31 mwaka jana kati saa tano asubuhi hadi sita mchana kwenye kwenye makambi ya wakimbizi.

“Jumla ya nguo zinazofanana na sare za kijeshi 1,947 zilikamatwa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli na Nduta zote za hapa hapa Kigoma.

“Katika Kambi ya Nduta zilikamatwa sare 1,325 na Mtendeli 622,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini walioingiza sare hizo na lengo lao.

Kama Sare 1,947 kwa ujumla wake zimekamatwa unadhani ni ngapi labda zimeshaingia au kuna Watu wabaya wangapi wameshaingia nchini? Tafsiri ya hii ni pana sana ila ukiishia tu katika Sare hizo zilizokamatwa hutoweza Kuelewa lolote / chochote. Hiyo ni ' Ishara ' mbaya mno na inaonyesha kuna Taasisi kadhaa hapa nchini Tanzania hazifanyi Kazi zake vizuri na zinakula tu ' Mishahara ' ya bure.
 
Back
Top Bottom