Saratani ya tezi dume tishio Dar.................


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
Saratani ya tezi dume tishio Dar


na Ratifa Baranyikwa


amka2.gif
IMEELEZWA kuwa saratani ya tezi dume ambayo huwapata wanaume, umezidi kuwa tishio kutokana na inasababisha vifo vingi nchini, hususani jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dk. Emmanuel Kandusi, ambaye ni mratibu na mwanzilishi wa Tanzania 50Plus Campaign, alisema ugonjwa huo umezidi kuwa tishio kutokana na uhamasishaji mdogo.
Alisema kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo, Benki ya NMB, imetoa msaada wa vipeperushi zaidi ya 35,000 vyenye thamani ya sh milioni 7.5 kwa ajili ya kuhamasisha kupambana na ugonjwa huo.
Akielezea ukubwa wa tatizo hilo, Dk. Kandusi alisema Saratani ya tezi dume kama zilivyo saratani nyingine, imeua wanaume wengi ambao walishindwa kufika hospitali kwa wakati kupata matibabu mapema.
“Kati ya wanaume sita, mmoja atapata saratani ya tezi dume katika uhai wake…pamoja na yote hayo ifahamike bayana saratani ya tezi dume ikibainika mapema inatibika kwa urahisi zaidi,” alisema Dk. Kandusi.
Akielezea kuhusu saratani hiyo alisema, tezi dume inapatikana katika uume ambapo chembechembe za uhai katika tezi dume zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu na mfumo wa mwili na hapo huanza kutengeneza vivimbe vidogo vinavyosababisha saratani hiyo.
Alizitaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kujisaidia haja ndogo kwa shida na mkojo unapotoka hukatikakatika.
Dalili zingine ni kuhisi muwasho wakati wa haja ndogo, uume kusimama kwa shida, maumivu ya kiuno, miguu, mgongo na pia kuona damu katika mkojo na manii.
Akizungumzia ugonjwa huo kwa ukubwa wake, Dk. Kandusi alisema ripoti mpya ya Benki ya Dunia (WB), inaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2020 wagonjwa wa saratani watakuwa milioni 12 duniani kote wakati wagonjwa wa HIV watakuwa chini ya milioni mbili na malaria milioni moja.
Alisema kwa nchi zinazoendelea, Afrika ikiwemo wagonjwa wa saratani ifikapo mwaka huo watakuwa milioni tisa wakati katika nchi tajiri watakuwa milioni tatu tu.
 
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Messages
3,280
Likes
670
Points
280
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2007
3,280 670 280
Kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa wazee hasa kuanzia miaka 55 na kuendelea wengi tumeona wakifariki kila wakati hivyop kunifanya nifikiri je kuna tiba sahii ya ugonjwa huu??????? naomba unijulishwe maana nina mgonjwa amepimwa kwa kutumia PSA na kukugundulika ana ugonjwa wa Tezi dume naomba kujua ni wapi anaweza kupata tiba sahii hapa nchini??????
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,348
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,348 280
Prostate Treatment Methods
In addition to medical treatment for enlarged prostate in a natural way can be used.
Materials needed:

  • Parsley
  • Chickpeas,
  • Barley flour
  • Chamomile,
  • Couch grass,
  • Honey
PREPARATION AND APPLICATION FORMS:

  • Dried parsley, chickpeas boiled water, then filtered dem. Filtered from the mixture, sweetening and drink three cups a day during treatment.
  • Barley flour, kneaded with Melhem until consistency of honey. Chickpea paste is prepared by grit size pills.Prepared these pills, Inc. when daisy-flavored three-day, five ingested the receiver.
  • Dried split root, crushed, pounded. The prepared powder is boiled in water for five minutes. Filtered from the liquid, syrup until consistency of honey was added and mixed. Prepared in this syrup, a cup of after dinner drink.
 
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Messages
3,280
Likes
670
Points
280
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2007
3,280 670 280
Aksante sana tatizo langu ni kiingereza umeniacha mlango wazi,Naomba kama kuna uwezekano nitafsilie kwa kiswahili tafadhali sana.
 
S

Subira

Senior Member
Joined
Mar 7, 2009
Messages
167
Likes
11
Points
35
S

Subira

Senior Member
Joined Mar 7, 2009
167 11 35
kuna bidhaa inayoitwa" crusiferous plus" ya kampuni ya gnld ukichukua tembe tisa kwa sikuh tatizo linakwisha kabisa> Dr. fatma wa kenyatta hospital alitoa ushuhuda kuhusu babake aliyemtibu kwa tembe hizo, ni matunda mengina greens kwa wingizilizomondani ya crusiferous plus.
 
Nanren

Nanren

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2009
Messages
1,789
Likes
235
Points
160
Nanren

Nanren

JF-Expert Member
Joined May 11, 2009
1,789 235 160
Njia nzuri ni kuondoa Makende

Ikifanyika kwenye early stages, mgonjwa atapona kabisa na ataishi muda mrefu. Wataalam wanahusisha prostate cancer development na presence ya excessive estrogens kulinganisha na testerone, kitu ambacho hutokea umri ukienda mbali. Kwa hiyo dawa hapo ni kuondoa source ya estrogens ambayo ni makende. Note that Wakati wa ujana testerones inakuwa nyingi kuliko estrogen na ndio maana unakuwa na nguvu za aina zote.

Kwa kuzuia, Wanaume wanatakiwa kula nyanya pamoja na Broccoli plus other Cruciferous vegetables mara kwa mara. Na ngono zisiwe too much. Too much ngono poses a burden on prostate gland resulting into its enlargement (it needs to enlarge itself in order to cope with your excessive ngono) and this enlargement may end up into abnormal growth which is cancer.
 
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Messages
3,280
Likes
670
Points
280
Echolima

Echolima

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2007
3,280 670 280
Kwa kuondoa Makende je Mzee wa kaya ataweza kusimama bila shida??????
 
Higash

Higash

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
844
Likes
52
Points
45
Higash

Higash

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
844 52 45
Nakushauri mpeleke muhimbili amuone urologist siku ya clinic ni muhimu sana kansa sio ugonjwa wa kufanyia majaribio ya dawa, atafanyiwa uchunguz na kujua kama imesambaa au bado then watajua cha kufanya, ukiwahi ndo vzuri.
 
F

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Messages
2,117
Likes
859
Points
280
F

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2011
2,117 859 280
Sasa na umri wa miaka 50,toka nikiwa kijana nikikuwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara yaani mpaka inaudhi wakati huo nilikuwa wala sijaanza ngono.Nilipoanza ngono nikawa natoa mbegu za kiume kidogo sana na ni mara moja tu na inanibidi nisubiri siku 4 hivi ndipo nipate tena vinginevyo nikifanya kila siku basi mbegu hazitoki kabisa.Sasa nikimaliza tu ngono mkojo unakuwa umejee sana naenda kuutoa nikitoka chhoni nikifika sebuleni umejaa tena inabidi niende tena.Hali ikawa hihivi hadi nikafikisha miaka 28 nikaoa.Nikaanza kwenda hospitali nikaambiwa nimevimba prostate sasa nikaogopa sana nikawa nadunduliza mbegu namuingilia mrs mpaka tukapata watoto 5 nikarudi tena hosp dokta akaniambia anifanie TURP yaani trans ureter resection of prostate baada ya hapo nikawa sasa ngono nafanya ila hakuna mbegu kabisa hali ambayo ni sperm retrogration,sasa tatizo langu ni kwamba ile hali ya kukojoa ndio imezidi sana yaani nakojoa zaidi ya mara w0 kwa dk 1 na nikisema niubane nasikia maumivu makali,je sasa huu ni ugonjwa gani tena?maana nimepima kisukari nil na je nifanyeje?
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,821
Likes
8,582
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,821 8,582 280
Kwa kuondoa Makende je Mzee wa kaya ataweza kusimama bila shida??????
Kwanza kabisa sikubaliani na dhana ya kuondoa Kende, kama upo ushahidi wa kitaalamu naomba unielimishe. Prostate hutibiwa kulingana na stage. Kama ni changa huwa inatibiwa kwa dawa, lakini kama ni kubwa hufanyika operesheni inayoitwa Prostectomy yaana kuondoa hiyo Prostate. Hii inaweza kuwa Open procedure, lakini sikuhizi hasa nchi zilizoendelea hufanyika kwa ku crush prostate kwa njia ya kitaalamu bila kupasua (Open). Kwahiyo ni vema aende kumuona Urologist pale Muhimbili, Bugando au KCMC.

Kuhusu bwana aliyeuliza kama ukiondolewa kende mambo inakuwaje. Mambo yanakuwa kama kawaida ila mapungufu yataonekana kwasababu viungo hufanya kazi kwa kushirikiana. Fahamu kuwa hapo ndipo utakuwa umehitimisha uzazi. Nadhani umenielewa.
 
K

Karata

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2011
Messages
324
Likes
27
Points
45
K

Karata

JF-Expert Member
Joined May 1, 2011
324 27 45
SARATANI YA TEZI DUME(PROSTATE CANCER)


1.0 UTANGULIZI: Sisi katika picha ni waathirika, wahanga, manusura wa saratani ya tezi dume (prostate cancer).Tunawasalimu! Kwa waraka huu tunapenda kuwahabarisha juu ya gonjwa saratani. Gonjwa hili kwa sasa ni gonjwa tishio kwa maisha ya watu wengi duniani. Katika nchi zinazoendelea na hususani Afrika chini ya jangwa la Sahara Tanzania ikiwa miongoni hali ni mbaya sana. Mwaka 2010 takwimu duniani zinaonyesha kuwa malaria iliua watu laki 5, kifua kikuu 2.1 milioni, ukimwi 1.8 milioni na saratani 9.9 milioni. Asilimia 75 ya hao 9.9 milioni ambao ni 7.4 milioni walifariki toka nchi zinazoendelea. Inatarajiwa mwaka 2020 malaria itaua watu laki 2.5, kifua kikuu 2.2 milioni, ukimwi 1.5 milioni na saratani 12.2 milioni. Asilimia 75 ya hao 12.2 milioni ambao ni 9.15 milioni watafariki toka nchi zinazoendelea.Waraka huu unawahabarisha umuhimu wa kuliangalia gonjwa la saratani na hasa saratani ya tezi dume ambao sisi ni wahanga. Tunawaomba WaTanzania muliangalie na kuliwekea uzito, mjielimishe juu ya gonjwa hili - saratani. Pamoja na kwamba saratani inauwa watu wengi duniani kuliko magonjwa ya kuambukiza kama malaria, kifua kikuu na ukimwi, lakini tunaona elimu ya saratani haijapewa uzito unaostahiki. Katika hotuba ya kuahirisha bunge la Jamhuri ya Muungano, Mkutano wa Tatu, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo K. P. Pinda (Mb) aliongelea kwa msisitizo juu ya saratani na hasa saratani ya tezi dume (prostate cancer) na magonjwa mengine sugu. Wa-Tanzania tuendeleze mkazo huu kwenye jamii tunazoishi. Wa-Tanzania tujielimishe juu ya hali hatarishi, dalili za saratani na umuhimu wa kujichunguza angalau mara moja kwa mwaka. Sisi tumelipata joto la jiwe la saratani ya tezi dume. Tunajua madhara ya saratani. Tusingependa watu wengine wapate mateso kama tunayoyapata kwa kuchelewa kugundulika gonjwa mapema. Hii ni sababu tosha iliyotusukuma kuanzisha Tanzania 50 Plus Campaign inayotoa elimu, utetezi na msaada wa saratani ya tezi dume kwa jamii nzima. Wachina wana methali isemayo, ‘Ukitaka kujua unakoelekea, muulize anayerudi’. Sisi tumerudi na tunakuhabarisha.

2.0 JEE SARATANI NI GONJWA GANI? Neno saratani ni jina la gonjwa ambao hutokea wakati chembe chembe za uhai katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu na mfumo wa mwili - zinaasi na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida chembe chembe za uhai mwilini huwa zinajigawa, zinapevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini chembe chembe za uhai za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe zinaishi muda mrefu kuliko chembe chembe za uhai za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza chembe chembe za uhai asi zingine na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo - saratani.
3.0 SARATANI YA TEZI DUME NI GONJWA GANI? Tezi dume linapatikana katika mwili wa kiumbe mamalia dume tu (angalia mchoro – normal prostate). Chembe chembe za uhai katika tezi dume zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili - zinaasi na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo, hapo mtu anakuwa ameathirika na saratani ya tezi dume. Zipo aina nyingi za saratani. Zipo zinazowapata watoto tu, vijana, wanawake na wanaume. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiacha saratani ya mapafu kwa vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS:2010) na cha Afrika Kusini (CANSA) vimebaini kuwa,“mwanaume mmoja kati ya sita atapata saratani ya tezi dume katika uhai wake”. Na kama wanaume mia moja watakutwa na saratani ya tezi dume. “Saratani hii haina mipaka ya kitabaka” asema Askofu Mkuu Desmond Tutu. Askofu Mkuu Tutu, sisi binafsi na Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela ni baadhi ya waathirika wa gonjwa hili ambao bila ya kujinyanyapaa na wala hofu ya kunyanyapaliwa, tumevunja ukimya na kuwa wawazi katika jamii. Pamoja na yote hayo, ifahamike bayana, saratani ya tezi dume ikigundulika mapema inatibika kwa urahisi zaidi.

4.0 HALI HATARISHI:

Kuna hali hatarishi nyingi zinazochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Zifuatazo ni baadhi tu:-

Umri: Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume inaongezeka sana hasa ukifikia umri wa takribani miaka 50 na kuendelea; Nasaba: Kama katika ukoo kuna historia ya ugonjwa wa saratani ya tezi dume suala na nasaba linachangia kumweka mwanamume kuwa hatarini kuathirika na saratani ya tezi dume kwa misingi ya nasaba (genetic); Lishe: wanaume wanaopenda kula nyama (red meat) yenye mafuta mengi na aina ya maziwa yenye mafuta mengi (high-fat diet) wako katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume; Mazoezi: Wanaume wasiopenda kufanya mazoezi; Unene (obesity). Upungufu: Virutubisho E.

5.0 DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME:

Swali linakuja: Jee mwanamume ataziona dalili zipi zinazoashiria saratani ya tezi dume? Zipo dalili nyingi na hapa nazitaja baadhi tu:

Udhaifu katika kujisaidia haja ndogo na unapotoka unakatizakatiza; Kushindwa kukojoa na kushindwa kuanza pata haja ndogo; Unapohisi haja ndogo unapata shida kuzuia haja ndogo isijitokee yenyewe; Hisia ya kutaka kupata haja ndogo kila wakati hasa nyakati za usiku; hata kukojoa kitandani; Mkojo kujitokea wenyewe; Maumivu au kuhisi mwasho wakati wa haja ndogo; Mbabaa kusimama kwa shida; Maumivu wakati unapotoa manii wakati wa kujamiana; Damu damu katika mkojo na katika manii; Maumivu viungoni – kiunoni, miguu, mgongo nk. Kukosa hamu ya kula na kupungua uzito / kukonda.

Pamoja na kuorodhesha dalili hizo napenda msomaji ujue kwamba mwanaume anapoanza kuziona na kuzihisi kati ya dalili hizo, basi ajue chembe chembe za uhai asi katika tezi dume lake zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.

6.0 MWITO KUFANYIWA UCHUNGUZI WA TEZI DUME:

Kwa kuzipitia dalili hizi, imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi huwa na soni kwenda kumwona daktari kwa uchunguzi. Wengi huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina – “kuna mkono wa mtu, nimelogwa”. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuliita gonjwa la mabasha na wengine kuurahisisha kama ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni haki yake kuugua mwanaume mwenye umri wa utu uzima. Mambo kama hayo huleteleza wanaume kujinyanyapaa na kujikuta wengine wakijitibia chochoroni au kwa waganga wababaishaji mpaka pale wanapokuwa hoi bin taabani, mambo yamekuwa mabaya ndipo wanapopelekwa hospitalini. Hapa tunatoa wito kwa wanaume kuweka kipaumbele kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla na ujumuishe uchunguzi wa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.

Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kukupima mara moja ofisini kwake: Vipimo hivyo ni “Digital Rectal Exam (DRE)” na cha pili ni “Prostate Specific Antigen (PSA)”. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine vya uhakiki kama transrectal ultrasound au na prostatic needle biopsy. Kuwahi kugundua saratani mapema, kabla ya dalili, ni faida kubwa kwa mwaathirika. Maana saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.

7.0 SARATANI NA MATIBABU:
Pamoja na yote hayo, katika zama hizi, matibabu ya saratani ya tezi dume yanapatikana. Ukigunduliwa una saratani hiyo unashauriwa ushauriane na daktari wako kuamua aina ya tiba itakayokufaa. Kuna tiba za uangalizi (active surveillance), upasuaji (surgery), mionzi (radiotherapy) vichocheo (hormone therapy) na kemikali (chemotherapy).

8.0 TUOMBWA KUUNGWA MKONO:

Katika mpango kazi wa kampeini hii tuna mahitaji mengi. Tumekusudia kuwafikia Watanzania wengi zaidi mwaka huu. Tunapenda kutumia nafasi hii kukuomba mchango wako na toka marafiki zako kwa ajili ya kampeini hii. Mwaka huu kati ya miradi tuliojipangia ni pamoja na kuchapicha vipeperushi vya Kiswahili vya saratani ya tezi dume milioni moja na kuvitawanya nchi nzima! Kipeperushi kimoja kinagharimu takribani Tshs. 250 hadi 300 kufuatana na wingi wa nakala. Vipeperushi vimekuwa vya msaada sana katika kutoa elimu ya gonjwa saratani. Kwa kuanzia mchango katika eneo hili utashukuriwa sana.

8.0 HITIMISHO: BAADA YA MAELEZO HAYO TUNAPENDA KUTOA WITO:

8.1 Kwa wanaume wote wenye umri takribani miaka 50 na kuendelea, tafadhali mwone daktari wako kwa uchunguzi wa afya ukijumuisha uchunguzi wa tezi dume;

8.2 Elimu hii itolewe pia kwa akina mama wote katika jamii mnayoishi. Wakinamama wakipata uelewa wa saratani ya tezi dume, wanaweza kuwaelimisha na kuwasaidia waume zao, baba, kaka, wajomba nk. Pia nao wahimizwe kujua juu ya saratani za wanawake kama za matiti na shingo ya uzazi nk.

8.3 Tunawaomba madaktari wote, mnapopata wagonjwa wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea washaurini pamoja na matibabu mengine, wafanyiwe uchunguzi wa tezi dume.

UKWELI KUHUSU SARATANI:

“Saratani zote na hususani saratani ya tezi dume ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.”

Kwa mawasiliano zaidi: Mratibu, Tanzania 50 Plus Campaign, P. O. Box 1854 Dar es Salaam
au barua pepe : tanzania50plus@yahoo.com, info@tanzania50plus.org Simu: +255 754 402033.

KUCHANGIA KAMPEINI :
Weka katika tawi lolote la CRDB. Jina la akaunti : Centre for Human Rights Promotion – CHRP;
Namba ya akaunti: 01 J 1027311100 au kupitia M-Pesa: 0754 402033

TUPIGE VITA SARATANI! TUPIGE VITA SARATANI YA TEZI DUME! PAMOJA TUNAWEZA!

Kimetayarishwa na kutawanywa na:

Tanzania 50 Plus CampaignNaomba kuwasilisha.
​
 

Forum statistics

Threads 1,237,198
Members 475,497
Posts 29,281,157