Saratani ya Matiti: Fahamu viashiria muhimu vya Ugonjwa huo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Saratani ya Matiti ni ugonjwa maarufu sana katika kuwapata Wanawake japokuwa unaweza kutokea kwa Wanaume ila ni nadra sana ikilinganishwa na Wanawake

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa vifo 42,260 (Wanawake 41,760 na Wanaume 500) vinatokea kwasababu ya Ugonjwa huo kila mwaka na 62% ya Wanawake wanafariki kutokana na kishindwa kupima afya zao mara kwa mara

Idadi kubwa ya Wanawake hawajui viashiria vya mwanzo vya Saratani ya Matiti na kwa mujibu wa gazeti la Independent, 42% wanajua ni mabadiliko gani ya kuangalia kwenye matiti yao huku robo ya Wanawake wakidhani kiashiria pekee ni uvimbe

Wanawake wanashauriwa kukagua matiti yao kila baada ya mwaka na kuangalia viashiria vifuatavyo; Uvimbe, Badiliko la Ukubwa au Muundo wa titi, Kutokwa na vipele vidogo au Ngozi kukakamaa na Chuchu kutoa majimaji

Aidha, viashiria vingine ni Ngozi kutokurudi katika hali ya kawaida baada ya kubonyezwa/kugandamizwa, Maumivu ya mara kwa mara, Mabadiliko katika mguso wa Ngozi, Kuvimba maeneo ya kwapa na Mabadiliko katika muonekano wa Chuchu(Kuingia ndani au kuchomoza)

Inashauriwa unapoona dalili kama hizi, ni vizuri kwenye kumuona daktari atakaye fanya uchunguzi zaidi na baadaye kukupeleka kwa bingwa wa magonjwa hayo kwa ushauri na tiba zaidi
*****

Breast Cancer is one of the most common cancer diagnosed in women, though it can occur in men but it is most common in women.

According to World Health Organization it is estimated that 42,260 deaths (41,760 women and 500 men) from breast cancer will occur this year.

About 62% of women die of cancer because they fail to go for regular cancer check ups.

According to Cancer Net, breast cancer is the second most common cause of death from cancer in women in the United States, after lung cancer.

However, since 1989, the number of women who have died of breast cancer has steadily decreased due to early detection and treatment improvements.

Currently, there are more than 3 million women who have been diagnosed with breast cancer in the United States.

Avon launched a campaign to educate the women about breast cancer and it discovered that a large number of women do not know the early stages of breast cancer.

According to the Independent, 42% knew what changes to look for in their breasts while a quarter of women thought that a lump was the only sign.


“Early detection is crucial to fighting breast cancer, yet our survey found that women don’t know their risks or what signs to look for,” said Sheri McCoy, chief executive of Avon.

Women are advised to check their breasts each month. Warning signs include:
  • A lump
  • Change in breast size or shape
  • Rash or skin sores
  • Nipple discharge
  • Skin indentation
  • Constant pain
  • Change in skin texture
  • Swelling around the armpit or collarbone could be an indicator
  • Growing vein
  • Inverted nipple (any change in nipple position, such as your nipple being pulled in or pointing differently)
When one notices any of these signs, it is advisable to visit a General Practitioner who will perform some examinations and later refer you to a specialized doctor.

According to Breast Cancer Now, one in eight women in the UK develop breast cancer at some point in their lifetime, despite this a large number of women do no check their breasts for the symptoms.

According to National Health Service, another sign to watch out is bleeding from the nipple.
 
Asante kwa elimu hii, kitu cha kuzingatia ni kwenda kucheki afya mara kwa mara kama inavyoelezwa na wataalamu wa afya ili kudhibiti tatzo kama hili. Maana likitokea ni shughuli ingine.
 
Asante kwa elimu mkuu,ila inasikitisha comments chache sana za watu ,ila ungeweka udaku au picha fulani fulani hapa,comments zingekua zinakaribia elf 10.

Ndiyo tulipofika
 
Tunashukuru kwa elimu. Je kama mtu anadevelop kitu kama kukauka ngozi kwenye titi lakini haliumi ni nini? Mimi nafanya mammogram kila mwaka ila naona titi moja linakuwa kavu kwenye chuchu.
 
Back
Top Bottom