Sarakasi za ma-DC: DC Shinyanga amsweka ndani muhandisi manispaa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amemsweka rumande Muhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simoni Ngagani, baada ya kupuuza agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua kokoto na Saruji kwa ajili ya kusimika mapipa 50 ya kutunzia uchafu kwenye mitaa mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga ikiwemo eneo kituo cha mabasi yaendayo wilayani.

Tukio hilo limetokea April hii mjini Shinyanga wakati Mkuu huyo wa wilaya akiwa na msafara wake alipowasili katika eneo la stendi ya mabasi yaendayo wilayani kwa lengo la kufanya uzinduzi wa kusimikwa kwa mapipa hayo na kukuta maandalizi hayajakamilika.

Matiro alimuagiza Mhandisi huyo kufanya maandalizi hayo mapema mbele ya Mkurugenzi wake wa manispaa ya Shinyanga, Kalinjuna Lewis, kuwa ataandaa vifaa hivyo majira ya saa moja asubuhi ili zoezi kusimika mapipa hayo likamilike haraka, na baada ya hapo wafanye usafi wa mazingira lakini agizo lake mhandisi huyo akapuuza.

Mkuu huyo alipomhoji mhandisi huyo kwanini alipuuzia agizo lake la kufanya maandalizi mapema, mhandisi huyo alianza kujikanyaga kanyaga akidai sababu iliyomkwamisha ni kukosekana kwa pesa za kununua kokoto na saruji kwani mvua kubwa ilinyesha na kushindwa kwenda benki, na alivyoamka asubuhi ndipo atakafuta zana hizo.

Hata hivyo Mkuu huyo hakuridhika na majibu hayo ndipo DC alipochukua uamuzi ya kumsweka rumande kwa kumuagiza mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Shinyanga kumkamata na kumuweka ndani mhandisi huyo wa ujenzi manispaa hiyo Samson Ngagani kwa kosa la kuchelewesha maandalizi ya vifaa vya ujenzi vilivyopangwa kutumika kusimika mapipa ya taka.

“Hawezekani tukubaliane tuamke mapema ili tufanye kazi hii haraka na pia tuingie Mitaani kufanya usafi, ambapo mimi nimeamka saa 11 nikajiandaa harafu wewe una kuja saa mbili tena bila ya kufanya maandalizi yeyote hii si kunidharau hivyo naagiza OCD mkamate akakae Rumande kwanza ili liwe fundisho kwa wengine” ,alisema Matiro.

Katika uzinduzi huo Matiro alisema mapipa hayo ya taka ambayo idadi yake ni zaidi ya 50 yatawekwa katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya Shinyanga na wananchi wanatakiwa kuyalinda.

Kuna haja ya hawa wakuu wa Wilaya kufuata sheria za utumishi, wamegeuka miungu watu

Source: Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga amkamua jipu Mhandisi wa manispaa, amsweka rumande huku Mkurugenzi wake akishuhudia | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Hata ningelikuwa mimi ningelikuwa hivyo kutetea ugali cheo chenyewe kimeandikwa kwa chaki boss akikosea akaegemea ubaoni unafutika kwanini usijipendekeza, vyeo vitamu bhana asikwambie mtu.
 
Hata ningelikuwa mimi ningelikuwa hivyo kutetea ugali cheo chenyewe kimeandikwa kwa chaki boss akikosea akaegemea ubaoni unafutika kwanini usijipendekeza, vyeo vitamu bhana asikwambie mtu.
teh teh teh
sasa mkuu ndo iwe kusweka watu ndani kwa kosa dogo hivyo aiseee
 
teh teh teh
sasa mkuu ndo iwe kusweka watu ndani kwa kosa dogo hivyo aiseee

Hata kuwekwa ndani ni adhabu ndogo pia maana mnatetea uzembe badala ya kumsapoti Dc Mhandisi ana gari ya manispaa mvua inakwamisha vipi kuchukua fedha benki?
 
Tena akitakiwa amsweke above 48hrs, uzembe mkubwa sana
 
Rais anapaswa kuongea na hawa na DC wake haraka sana!Wanaipaka mno matope serikali yake na kuonekana ni serikali ya hovyo hovyo tu

DC Kasesera Iringa kawaweka mahabusu watangazaji walio iga sauti yake,kule Kyela DC kamuweka mahabusu Diwani ambaye kata yake alikutwa mgonjwa wa kipindupindu

DC na RC vyeo hivi vifutwe!
 
Ma DC wa mkoloni walikuwa wanatembea na walugaluga akikukamata haujapalilia pamba unakula mijeledi mbele ya mkeo kwanza ndio unaenda ndani, usijekuta hizo hela alishanywea pombe.
 
Engineer ni wapili kutoka kushoto na mkuu wa wilaya ni huyo alueshika kiuno
 

Attachments

  • 1459737456063.jpg
    1459737456063.jpg
    79.8 KB · Views: 85
Tatizo kazi za mazoea hata ukipewa maagizo na mkuu ilikua hiyari kutekeleza kwa wakati au utakapojisikia kisa kunamtu juu yake anamilinda ndo madhara yake haya
 
Back
Top Bottom