Sarakasi za CCM, Usanii wa Operation Vua Magamba na kuzaliwa kwa Zuma wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sarakasi za CCM, Usanii wa Operation Vua Magamba na kuzaliwa kwa Zuma wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keil, Apr 25, 2011.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Awali ya yote naomba niseme kwamba siweki hili bandiko kwa lengo la kuwatetea mafisadi, bali ninajaribu kufikiria nje ya sanduku kwa mapana na marefu ili kuona hila ya CCM katika kughilibu waTanzania wenzangu.

  Nimeipitia document ya KANUNI ZA UONGOZI NA MAADILI ya CCM (Toleo la 2002) ambazo ndio zinaelezea makosa mbalimbali ambayo mwanachama anaweza kuyafanya na pia ni adhabu gani ambayo anaweza kuchukuliwa kulingana na makosa yake. Document hiyo inapatikana hapa: http://www.ccmtz.org/nyaraka/kanunimaadili.pdf

  Kulingana na document hiyo, kipengele cha 8 kinaongelea makosa mbalimbali na adhabu zake. Mpaka sasa ninaona wazi kwamba Secretariat Mpya pamoja na Mwenyekiti wao hawajui wanachokifanya, maana wako kinyume na Kanuni zao za Uongozi.

  Kitendo cha Nape Nnauye kutangaza kwamba watuhumiwa wa ufisadi wanatakiwa kujiuzulu, ni kukwepa responsibility ya Chama kuchukua hatua. Dhana ya kumtaka mtuhumiwa ajiuzulu bila kuthibitisha tuhuma hizo ni sawa na kumuonea. Kulingana na Kanuni za Uongozi, tuhuma za kukipaka matope chama lazima zichunguzwe na baada ya hapo hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo hupeleka mapendekezo yake kwa Kamati Kuu na hatimaye kwenye NEC.

  Kwanza, tuhuma hizo hazijafikishwa kwa Kamati ya Maadili, mbili hazijachunguzwa na kuthibitishwa na mwisho, Kikao cha NEC kilifanyika baada ya CC na Secretariat kujiuzulu. Je, hizo za Agenda kuwataka mafisadi wajiuzulu ziliandaliwa na CC ipi na ilihali CC ilishajiuzulu? Ukienda hatua moja moja, kulikuwa na pendekezo kwamba wanaokipaka matope chama watoswe, lakini hakukuwa na makubaliano.

  Kitakachofanyika: Nape Nnauye na Chiligati watasema kwamba barua zimeandikwa na baada ya hapo watuhumiwa watagoma kuondoka mpaka taratibu zote zifuatwe kwa kuchunguza tuhuma zao na baada ya kuchunguza tuhuma na kuthibitika, ndipo sasa Kamati ya Maadili inaweza kukaa na kupendekeza hatua za kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa ambapo CC nao watajadili na kupendekeza kwa NEC kwa ajili ya utekelezaji. Katika hili sakata, hakuna kilichofanyika mpaka sasa zaidi ya ngojera za kwenye majukwaa tu.

  Uchunguzi wa tuhuma hizo, Kanuni za Uongozi hazisemi kwamba ni nani mwenye jukumu la kuchunguza. Kwa kuwa watuhumiwa wanatuhumiwa kufanya ufisadi wa mali ya umma, ina maana kwamba Jeshi la Polisi na PCCB ndio wenye jukumu la kufanya uchunguzi huo. Je, kuna mtu ana imani na Jeshi letu la Polisi au PCCB? Kesi ngapi ambazo PCCB imezisimamia na ikashindwa kuwafunga watuhumiwa hata pale ambapo ushahidi ulikuwa wazi?

  Dr. Hoseah alichunguza Richmond na kusema ilikuwa ni deal halali na hakukuwa na harufu ya rushwa. Leo hii akipewa jukumu kama hili la kuwachunguza Chenge, Lowassa na Rostam, ataweza kutoa majibu tofauti na yale yaliyotolewa awali? Je, IGP Said Mwema na DCI Bwana Manumba wana ubavu wa kufunua kila kitu kwenye hizo tuhuma za ufisadi?

  As long as kuna hatari ya kufungua Pandora Box, uchunguzi wowote utakaofanyika unaweza kuishia kumsafisha Lowassa, Rostam na Chenge na hivyo watakuja ku-bounce back kwa nguvu kubwa sana. Ninachokiona mbele yetu ni kuzaliwa kwa Zuma wa Tanzania japo sina hakika na tuhuma za Mzee Jacob Zuma wa Sauzi kama zilikuwa na ukweli wowote.

  Hii Operation Vua Magamba itaishia kwa Lowassa, RA na Chenge kupelekwa mahakamani na ushahidi ambao uko weak na baada ya hapo watashinda kesi zao na kurudi ndani ya Chama. Lowassa pamoja na uchafu wake mwingi sana ana wafuasi wengi sana ndani ya CCM kuanzia ngazi za wilaya mpaka NEC Taifa. Kwa kiyo ili kummaliza lazima wavuruge kila kitu kwenye mfumo mzima wa CCM, vinginevyo the guy will bounce back na atakuja kuwashangaza sana. Na Kikwete huyu huyu atakuja akicheka cheka kwamba jamani huyu mtu alituhumiwa tu, baada ya uchunguzi na kesi kupelekwa mahakamani amesafishwa na sasa yuko clean. So, kama wanachama mnamtaka mpeni kura ili apeperushe bendera ya Chama kwenye Urais. Hakuna mchapakazi kama Lowassa!

  WanaCCM kama kawaida yao watalipuka kwa shangwe na vigelegele na kuanza kushangilia kwamba Lowassa ndo chaguo lao.

  Angalizo: Kesi za Ufisadi ambazo zinamgusa Mkapa mpaka sasa zinasua sua mahakamani na kuna dalili zote za hao jamaa kushinda. Nina hakika kwamba tuhuma za ufisadi za Lowassa, Chenge na Rostam zinawagusa pia Mkapa na JK mwenyewe. Kwa hiyo ni ngumu kupata concrete evidence ya kuwatia hatiani kwa kuwa kuna baadhi ya ushahidi inabidi ufichwe ili Mkapa na JK wasije wakaguswa na ndio maana naona kwamba wakipelekwa mahakamani watashinda kirahisi sana na hivyo kusafishwa kwa sabuni yenye marashi na wanapuliziwa na perfume kabisa.
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Asante, wewe ni mtabiri gani? unauhusiano wa kiofisi na sheikh yahaya?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mazingaombwe ni sanaa ya kutumia ujanja ujanja na kuhadaa hadhira kufikiria kiini macho kinachofanyika kina ukweli. Sisi wengine tunajua CCM inajaribu kucheza Mazingaobwe, Kama ni kujivua kweli hayo magamba sioni wa Kusimama kuanzia Kikwete mwenyewe, Mkapa na hata wale walionufaika na fedha za Jeetu Patel.
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Keil niliwahi kusema zamani Ccm wanachokifanya ni sarakasi na kubadilisha mwelekeo. Sasa hivi mtazamo Wa Tanzania upo kwenye magamba wameshasahau Dowans, Richmond , IPTL, makanisa (zile bilioni 600) , stimulus package, etc. Mwishowe akina Lowassa, Rostam, na Chenge watasafishwa na kutawazwa kuwa watakatifu hawana doa. Nchi imeuzwa hii!!!
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Keil,
  Mkuu shukran kwa kutuwekea hii link.
  Nimeitazama na hasa kifungu cha TUHUMA kinasema hivi:-


  7.4
  Tuhuma

  7.4.1 Mtu ye yote anayetuhumiwa mbele ya Kamati ya Usalama na Maadili ya Ngazi yo yote, kwa kosa lo lote linalohusiana na Maadili au Nidhamu ya Chama atasomewa na kuzijibu Tuhuma hizo mbele ya Wajumbe wa
  Kamati hiyo kwanza yeye mwenyewe, ama kwa kauli yake ama kwa maandishi; lakini hataambiwa nani aliyezileta Tuhuma hizo, isipokuwa kama imekwisha julikana mapema kutokana na mijadala ya Vikao,
  Vyombo vya Sheria, au Vyombo vya Habari.  7.4.2 Uchambuzi wa Tuhuma hizo utafanywa kwa kutumia njia mbali mbali, pamoja na mashahidi watakaoweza kupatikana. Uchunguzi utakapokamilika, na endapo itadhihirika kwamba Tuhuma zina uzito,
  Mtuhumiwa ataitwa mbele ya Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Ngazi inayohusika, kama ni lazima, ili apate kuhojiwa ana kwa ana.  7.4.3 Kamati ya Usalama na Maadili ya Ngazi inayohusika itatoa Mapendekezo yake kuhusu suala hilo, kwenye kikao cha Maamuzi kinachohusika. Mtuhumiwa atapewa nakala ya Maamuzi kwa maandishi.  Kwa hiyo ni vizuri tukawatoa makosa CCM kulingana na kifungu hiki hata kama tutajua au kufikiria kwamba CCM wanafanya usanii mtupu. Binafsi naamini kweli JK atafanya lakini kwa nia ya kuwalinda hawa Mafisadi hawa dhidi ya sheria ya miiko na maadili ya Kitaifa..


   
Loading...