Sarakasi za bavicha zinaendelea - wagombea hawa kuenguliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sarakasi za bavicha zinaendelea - wagombea hawa kuenguliwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teh Teh Teh, May 18, 2011.

 1. T

  Teh Teh Teh Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wana JF:

  Kuna tetesi kuwa baadhi ya wagombea wa Uenyekiti, Umakamu na Unaibu wanaweza kuenguliwa kutokana na ushahidi kuwa wameanza kufanya kampeni mapema - wanaotajwa kuenguliwa ni John Heche, Habibu Mchange, Saanane, Joshua Nassari na Dady Igogo.

  Waraka kama huu wa Dady Igogo kwa wajumbe ni mojawapo ya evidence za kuenguliwa?

  KUGOMBEA KWANGU NAFASI YA UNAIBU KATIBU MKUU WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA [BAVICHA] – TANZANIA BARA.

  Kwa heshima na taadhima napenda kukutaarifu kwamba nimechukua fomu ya kugombea nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) – Tanzania Bara.

  Hatua hii ni baada ya tafakuri kubwa na kupata ushauri wa kina kutoka kwa wadau mbalimbali wa siasa za Tanzania. Hata hivyo msukumo wangu wa ndani wenye dhamira ya dhati na mchango ninaotaka kuutoa kwa vijana wenzangu imekuwa ni msukumo mkubwa ndani ya nafsi yangu.

  Ni dhahiri kuwa ninazo sifa, uzoefu, ujuzi na dhamira ya dhati katika kuongoza harakati za Vijana wa CHADEMA katika kipindi hiki muhimu cha kudai ukombozi wa Taifa hili. Katika kipindi muhimu tunapokaribia kuteka nyara dola ya mafisadi na kuirudisha kwa watanzania masikini mwaka 2015.

  Nimelelewa na kukuzwa kisiasa nikiwa kama Afisa wa Makao Makuu kwenye kurugenzi za Sheria na Haki za Binadamu chini ya Tundu Lissu; nikiwa kama Afisa wa Mafunzo na Oganaizesheni. Nikiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya wagombea wa udiwani, ubunge na urais kwa mwaka 2010; nikiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Logistiki chini ya Prof. Mwesiga Baregu kutokana na uteuzi wa kamati kuu ya chama.; msimamizi mkuu wa zoezi la utafutaji wa wadhamini wa mgombea Urais – Dr. Slaa (NEC) kwenye mikoa 10 ya Tanzania. Kama Katibu wa Vijana Arumeru Mashariki. Hivi sasa mimi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arusha nikiwa na umri wa miaka 26 tu na mlezi-mshauri wa matawi zaidi ya nane, ikiwemo tawi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha.

  Uzoefu wa mikikimikiki za harakati za kisiasa za vyuo vikuu nikiwa kiongozi wa DARUSO na siasa za nchi zinanipa tu sifa za ziada ya kuhitaji kuongoza Baraza hili muhimu kwa chama na Taifa. Ni wazi nimekuzwa na kukomazwa kisiasa, kiharakati na kitaasisi na Freeman Mbowe, Dr. W. Slaa, Zitto Kabwe, Tund Lissu, John Mnyika na wengine wengi; hali inayonipa sifa stahili za kuhitaji kuwa kiongozi wa Baraza hili muhimu na adimu.

  NIA YANGU ni kuunganisha nguvu na sauti ya vijana katika kudai ukombozi wa Taifa na kuleta haki na usawa kwa watanzania, kuifanya BAVICHA kuwa Taasisi imara, kuzidisha ushiriki wa vijana kwenye siasa hususani wanawake; kuwa chemchem ya ushauri kwa Chama katika masuala muhimu yahusuyo vijana; kuipa BAVICHA sura vutivu ya kitaasisi na kiharakati; kuandaa vijana kushika hatamu ya Chama na Serikali mwaka 2015, kufungua ofisi za BAVICHA angalau katika kiwango cha wilaya zote 113 za Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar; kutoa mafunzo ya kiuongozi kwa Wenyeviti/makatibu wa mikoa na wilaya/majimbo yote Tanzania nzima; kubaini na kukuza vipaji vya vijana na kuwaandaa kuwa viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi mbalimbali; kutafuta vyanzo vya fedha na kuziwezesha ofisi za wilaya.

  Tunapokaribia kuingo’a dola ya mafisadi iliyotawala kwa miaka 50 BAVICHA inahitaji viongozi majasiri wasiogopa kufa kwa ajili ya Taifa. Uzoefu wangu wa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka na jamhuri na kushinda kesi kutokana na kudai haki za vijana wa kitanzania, kukamatawa zaidi ya mara 6 na jeshi la Polisi kwa kutetea na kupaza sauti kwa vijana wa kitanzania ni miongoni mwa sifa zidishi tu kwangu ya kukusudia kugombea nafasi hii. Hivi sasa ni mtuhumiwa namba 10 katika kesi ya maandamano ya Arusha Mjini.

  Napenda kuchukua fursa hii kukuomba uniunge mkono wa haki ambayo kwangu ni ukombozi mkubwa. Najua zipo propaganda za udini, ukanda, ukabila au ujinsia. Kumbuka kuwa tunakwenda kuunda BAVICHA ya KIHARAKATI kwenye siasa na siyo ya “KISIASA”.

  Inawezekana kukawa na fedha nyingi, propaganda nyingi, uzushi mwingi zikatumika dhidi yangu! Lakini napenda kukwambia ya kwamba MUNGU YUPO UPANDE WA WAPIGANIA HAKI!

  Ingawa elimu yangu ni kiwango cha digrii mbili; lakini naamini kuwa hatuchagui Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA kwa elimu yake tu maana BAVICHA siyo sekondari au chuo; wala kwa dini yake maana BAVICHA siyo kanisa wala msikiti; kwa umbile kubwa maana BAVICHA siyo sehemu ya mieleka; BAVICHA ni Taasisi ya Kiharakati kwenye siasa!

  Kwa ridhaa yako nakusudia kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA – Tanzania Bara wala siyo kwa kanda fulani au mkoa fulani.

  Ni Heri kufa katika harakati za kutafuta Haki na Usawa kwa watanzania kuliko kuendelea kuishi katika manyanyaso na dhuluma kwa watanzania.

  Naamini kwamba tumekusudia KUSHINDA kwa maana TUMECHAGUA KUSHINDA!

  VIJANA! Nguvu ya Mabadiliko!

  Wako katika ujenzi wa Demokrasia na Maendeleo.  Dady Igogo.
  Mgombea – Unaibu Katibu Mkuu – BARA.
  0713 – 616096
  dady@chadema.or.tz
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hapana....
  endelea na maswali...
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwani mtu kujitambulisha kuwa wewe ni mgombea au umechukua fomu ni kampeni nafikiri hujui maana ya kampeni kwa hiyo wanaotangaza kugombea urais mwaka 2015 nao waenguliwe kwa vile wameanza kampeni mapema haiingii akilini.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Eeh! Huku kuna makubwa

  Mimi sijapiga kampeni na wala sifikirii kukiuka kanuni za uchaguzi.Siku zote mimi ni mtu wa kanuni,sasa nitashangaza kama nitakiuka kanuni.Nilitangaza dhamira ya kugombea basi.Demokrasia makini ni lazima iendani na uhuru wa kutoa au kupokea habari

  Nje ya hapo kama ikithibitika pasipo na shaka kwamba kuna mtu ambaye anakiuka kanuni za uchaguzi inabidi awajibishwe hata kama ni mimi mwenyewe na sitanung'unika kwani chama kitakuwa kimenikumbusha wajibu wangu.Si hata sisi tunaipinga CCM kwa kupindisha kanuni?Lazima tuwajibike .Otherwise nimeona niwe clear kwa hili ingawa ni Tetesi.Thanks,Have a good Day!
   
Loading...