Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Huu Ni uzi maalum wa kukushana uhalifu mbalimbali uliotokea Tanzania 🇹🇿 kwa nyakati mbalimbali.
Matukio haya hayako kwenye mtiririko maalum wa kikalenda.

SARAH SIMBAULANGA NA WIZI MKUBWA NBC 1987
The case of Sarah Simbaulanga, a National Bank of Commerce (NBC) employee who stole Shs 31.0 million in foreign exchange (mostly travellers cheques) astonished Tanzanians because of the sum of money involved in the theft, the apparent ease with which it was carried out and, the biggest surprise of all, the immediate admission of guilt after the lady had been arrested. The accused looked very calm in the dock. �Yes� she said �it is true� to the five counts she was facing. The Principal Resident Magistrate asked her twice if she really understood the charges against her. She confirmed her plea of guilty.

The evidence presented to a packed court in Dar es Salaam was, in abbreviated form, as follows:

Between October 19th and 29th 1987 Simbaulanga and an accomplice named Toroha (whose extradition from Kenya is being demanded by the Tanzanian authorities) stole from the NBC 1,100 travellers cheques worth US$ 390,000 and 200 travellers cheques worth £20,000.

Simbaulanga and Toroha had been friends since the early seventies when she had been at Kisutu Secondary school in Dar es Salaam. She and Toroha hired two rooms at the Skyway Hotel on the night of October 29-30. Simbaulanga had managed to obtain four passports for herself and her three children. They travelled on an Air Tanzania plane to Nairobi on October 31st.

They then used some of the travellers cheques to buy five KLM tickets to London. On November 1st and 2nd they made twelve different transactions using $246,000, The Police are still trying to trace the remaining travellers cheques.

The accused then bought five tickets to Nairobi on November 5th, and in Nairobi they carried out further transactions with new travellers cheques they had bought in London. Toroha bought four mini-buses and a pick-up and registered them under the name of his wife Elizabeth. Later three other suspected accomplices were arrested Simbaulanga�s NEC Controller, a KLM Sales Manager and a businessman.

On February 10th Simbaulanga was sentenced to 35 years imprisonment, seven years on each count, to run concurrently. But, on February 16th, the Prosecution appealed the case and asked the High Court to issue an order for the sentence to run consecutively. Subsequently, Simbaulanga was sentenced to 28 years in prison. The case was one of many referred to later by SHIHATA under the heading �Tanzania�s thriving theft industry� in which it quoted a whole spate of thefts by servants of the NBC from branches all over the country. It estimated the total loss at over Shs 60.0 million

============

Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40).

Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha!.

Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, makambini, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha hizo. Kwa wengi, ilikuwa ni simanzi kubwa sana na haikushangaza basi pale Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la Vijana uliokuwa ukifanyika Singida kutoa wito kuwa uongozi wote wa juu wa NBC "Ufyekelewe mbali"!.

Ofisi ya DCI, mara moja, ilituma taarifa (Interpol) nchi mbalimbali ili zisaidie kuwakamata "mabandido" hao.

Hatimaye, majira ya saa 9 alasiri, siku ya Ijumaa, tarehe 13.11.1987, Bw. TOROHA akabambwa kwenye ofisi ya magari ya Toyota jijini Nairobi, Kenya akiwa kwenye mishemishe ya ununuzi wa magari.
"Mandata" walipombana aeleze kuhusu aliko Bi. SARAH, Bw. TOROHA hakuwa na namna zaidi ya kuwapeleka chumba na. 322 cha hotel maarufu ya Jacaranda. "Mandata" hao, wakiwa na TOROHA, waliingia chumba hicho kininja na kumkamata Bi. SARAH kiulaiiini!.

Jijini Dar Es Salaam, NBC ilimfukuza kazi Bi. SARAH kwa kutoonekana kazini kwa siku 5 mfululizi. Aidha, kamatakamata ilianza ambapo wafuatao walikamatwa na kuhusishwa na wizi huo:

Bw. ROMANIUS PETER NDANZI(43), Mdhibiti wa Fedha za Kigeni, NBC "Foreign Branch", Bw. ERNEST JOHN MWENEWANDA(40), Meneja mauzo KLM, HAROON DAUD(35), Mfanyabiashara. Washtakiwa hawa, tarehe 19.11.1987, walifikishwa Kisutu kwa "Pilato" Mh. JUMA MUSTAPHA JIBREA. Waliomba dhamana wakanyimwa. Wakakata rufaa Mahakama Kuu. Tarehe 5.1.1987, Jaji LUHEKELO KYANDO, aliwanyima dhamana na kueleza, kwa uchungu na uzalendo, kwamba:

*"Kiini cha kesi hii ni moja ya matukio ambayo yameshtua sana umma kuona kwamba mamilioni ya fedha yanaibwa. Ni maoni yangu kuwa itakuwa kinyume na hisia za jamii ikiwa mahakama itachukua msimamo tofauti na usiokuwa na mwelekeo wa hisia sahihi kuhusu vitendo hivi"*.

Msimamo huu uliakisi kilichoelezwa na aliyekuwa Waziri wa sheria, Mama JULLIE MANNING, tarehe 17.1.1976, kwamba: *"Ingawa Mahakama hazipendelei upande wowote, hiyo haina maana kwamba zisijali nini kinatokea nchini"*.

Serikali ilituma Kenya Hati ya kuomba SARAH na TOROHA warudishwe nchini(Extradition) kwani nchi hizi zina makubaliano hayo ya aina hiyo. Hati hiyo iliwasilishwa na SP PETER MWANGI mahakamani saa 2.30 asubuhi ijumaa, tarehe 15.1.1988 mbele ya Hakimu Mwandamizi, Mh JOSEPH MANGO na kisha maombi hayo yakaanza kusikilizwa.

Tarehe 29.11.1987, mahakama hiyo ikatoa uamuzi kuwa, kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, SARAH arudishwe Tanzania kujibu mashtaka lakini ikamuachia huru TOROHA. Baada tu ya kuachiwa, mbio alizotimua TOROHA, hata USAIN BOLT angesubiri!. Siku ya jumanne, saa 6 mchana, tarehe 2.2.1988, SARAH alikabidhiwa kwa maafisa wa Tanzania mpakani Namanga na kukimbizwa "wanguwangu" na magari 5 ya polisi hadi Dar Es Salaam.

SARAH alifikishwa mahakama ya Kisutu saa tatu asubuhi, siku ya Jumatano, tarehe 10.2.1988 chini ya ulinzi mkali. Mahakama hiyo ilikuwa imefurika mno huku barabara ya Bibi Titi ikifungwa kwa muda kwani wananchi wengi walitoroka makazini kwenda kumuona SARAH anafananaje na kusikia aliwezaje kuiba kitita chote hicho!.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi JOSEPH MASANCHE, Bi. SARAH alisomewa mashtaka 5 na SSP EDWIN ABRAHAM MAN. Bi. SARAH alikuwa akitetewa na Dr. MASUMBUKO ROMAN LAMWAI, mmoja wa mawakili bora kabisa kuwahi kutokea nchini.

Bi. SARAH aliushangaza umati uliofurika, pale bila kupepesa macho, kutingisha pua wala kutikisa maskio, alipokiri mashtaka yote 5! Hakimu MASANCHE nae pia alipigwa butwaa na ikabidi amuulize kama ameelewa vizuri mashtaka ambapo "alikomaa" na kusema anaelewa na anakiri ni kweli alienda makosa hayo!.

MASANCHE, baada ya kusikiliza pande zote 2 kuhusu adhabu, akasoma hukumu iliyochukua robo saa tu ambapo alimuhukumu SARAH kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa na makosa yote kwenda pamoja hivyo angetumikia miaka 7 tu na pia akamuamuru arudishe fedha hizo mara moja. Mh MASANCHE alin'gaka- *"Hakuna kitu kibaya kama wizi wa fedha za kigeni ambazo Taifa linazihitaji sana"*.

Upande wa mashtaka hakuridhika na adhabu hiyo "kiduchu" hivyo ukakata rufaa Mahakama Kuu kuomba adhabu hiyo iwe kwa kufuatana na sio kwa pamoja. Aliyekuwa Jaji Kiongozi, Mh. NASSOR MZAVAS ndiye aliyesikiliza rufaa hiyo huku jamhuri ikiwakilishwa na Bw. KULWA SATO MASSABA na Dr. LAMWAI akimuwakilisha SARAH.

Saa 4 asubuhi, Ijumaa ya tarehe 19.2.1988, Mh MZAVAS alitoa hukumu. Baada ya kuisoma hukumu hiyo kwa dakika 45, huku umati ukisubiri kwa hamu, Mh. MZAVAS "aliinama na kujifanya kama anajikuna" kisha "akampiga SARAH mvua 28"! SARAH hakuamini macho yake na kubaki amebun'gaa! Mh. MZAVAS akamalizia- *"Hii ni hasara ya kiuchumi ambayo inaiathiri nchi.

Fedha hizo kidogo za kigeni nchi ilizofaulu kujiwekea akiba kwa kujikidhi sana, ndio inalolifanya kosa la kuiba fedha za kigeni kutisha. Wizi huu ulipotangazwa na RTD, Mahakama pia ilisononeka na kufadhaika sana kwa kuibwa kwa fedha hizo za kigeni kwani Mahakama nayo ni sehemu ya jamii"*.

"Upigaji" huu wa ulikuwa umepangwa na wapenzi hao wawili, SARAH na TOROHA. TOROHA alikuwa ni kijana mtanashati aliyezaliwa Mbegani, Bwagamoyo mwaka 1948. Baba yake aliwahi kufanya kazi Ikulu na kisha akawa Afisa wa ubalozi Japan na Uholanzi miaka ya mwanzoni ya Uhuru na alikuwa na uwezo wa kifedha. Mwaka 1967, baada ya kuzinguliwa na siasa ya Ujamaa ambapo nyumba yake ilitaifishwa, aliacha kazi na kutimkia Ujerumani na kufanya biashara ya mkahawa na duka la vinyago.

Mwaka 1979, Bw. TOROHA, akiwa kijana wa miaka 31, alimuoa Mkenya, Bi. ELIZABETH WANJIRU na wakaishi Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Kenya.

TOROHA alikuwa akija nchini mara mojamoja hivyo akaanza urafiki na Bi. SARAH aliyekuwa binti mdogo mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Zanaki jijini. SARAH, baadaye, aliajiriwa NBC na kupanda vyeo hadi kuwa Msimamizi, Idara ya Fedha za Kigeni.

TOROHA aliingia nchini tarehe 11.10.1987 na kufanya "mchongo wa upigaji" na "Mpango wa kando" wake, Bi. SARAH. Ili kufanikisha dili la upigaji na kusepa nje ya nchi bila kushtukiwa, Bi. SARAH alishirikiana na maafisa wasio waaminifu wa "Immigration" na kubadili majina yake na ya wanawe na kupata "passports" mpya tarehe 28.10.1987.

"Passport" ya SARAH yenye Na. 220130 ikawa na jina KHADIJA ALI MKIMBAU. "Passports" za wanawe zikawa na majina mapya 1.HAPPINESS SIMBAULANGA-(JAMILA ISMAEL HASSAN), 2. SIMBA SIMBAULANGA- (HALFAN ISMAIL HASSAN), 3. BLANDINA SIMBAULANGA-(JENIPHER ISMAEL HASSAN).

Kisha, SARAH "akapiga" hundi za kusafiria 1,100 zenye thamani ya $ 390.000 na hundi 200 zenye thamani ya £ 20.000. Fedha hizo 'alizipiga' mara 3 kati ya tarehe 19.10.1987 na 29.10.1987. Kwa wakati huo, hizo zilikuwa ni fedha nyingi sana. Baada ya mchongo kukamilika, SARAH na TOROHA walichukua vyumba 2 katika hotel maarufu sana ya Skyway iliyokuwa makutano ya Ohio na Samora.

Chumba kimoja kilikuwa chao na kingine cha watoto wa SARAH ambako walilala kwa usiku mmoja wa Ijumaa, tarehe 30.10.1987. Usiku wa Ijumaa hiyo, SARAH na TOROHA walienda ukumbi wa White House "kushangilia ushindi" ambako bendi ya Marquis du Zaire chini ya Babu Seya iliwapagawisha vilivyo!.

Tarehe 31.10.1987, TOROHA, kin'gast chake SARAH na watoto wake 3 walikwea pipa la ATC kwenda Kenya. Walipotua tu Jomo Kenyata International Airport, wakatumia hundi zenye thamani ya $ 2700 kununua tiketi 5 za KLM na wakaenda Amsterdam na kisha London. Wakiwa London UK, waliofanya "transactions" nyingi "Baclays bank" na tarehe 2.11.1988 wakanunua tiketi 5 za KLM ili waondoke kuelekea Kenya tarehe 5.11.1987. Tarehe 3 na 4 ilikuwa ni "kujirusha" tu nchi ya Malkia ie *Kazi na Bata*!.

Tarehe 5.11.1987 walikwea KLM na kufika Kenya tarehe 6.11.1987. Nchini Kenya walifanya matanuzi na manunuzi ambapo TOROHA alitumia $ 260,000 kununua magari (mini-bus 4 na pick up 1) na yote akayasajiri kwa jina la SARAH. TOROHA, alipokuwa akitaka kununua magari mengine ndipo aliponyakwa na mamwela katika ofisi za Toyota tarehe 13.11.1987! .

Huu ndio mkasa wa Bi. SARAH MARTIN SIMBAULANGA
 
Huu Ni uzi maalum wa kukushana uhalifu mbalimbali uliotokea Tanzania 🇹🇿 kwa nyakati mbalimbali.
Matukio haya hayako kwenye mtiririko maalum wa kikalenda.
SARAH SIMBAULANGA NA WIZI MKUBWA NBC 1987

Mkuu Bujibuji nafikiri ingependeza hata ungeelezea kwa ufupi ilikuwaje na hitimisho lake kwenye kila tukio na naamini wengine watafata.
 
Napia link za hayo matukio zinge wekwa kama kulishawahi kuwa na mabandiko yake humu JF
 
Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40).

Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha!.

Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, makambini, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha hizo. Kwa wengi, ilikuwa ni simanzi kubwa sana na haikushangaza basi pale Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la Vijana uliokuwa ukifanyika Singida kutoa wito kuwa uongozi wote wa juu wa NBC "Ufyekelewe mbali"!.

Ofisi ya DCI, mara moja, ilituma taarifa (Interpol) nchi mbalimbali ili zisaidie kuwakamata "mabandido" hao.

Hatimaye, majira ya saa 9 alasiri, siku ya Ijumaa, tarehe 13.11.1987, Bw. TOROHA akabambwa kwenye ofisi ya magari ya Toyota jijini Nairobi, Kenya akiwa kwenye mishemishe ya ununuzi wa magari.
"Mandata" walipombana aeleze kuhusu aliko Bi. SARAH, Bw. TOROHA hakuwa na namna zaidi ya kuwapeleka chumba na. 322 cha hotel maarufu ya Jacaranda. "Mandata" hao, wakiwa na TOROHA, waliingia chumba hicho kininja na kumkamata Bi. SARAH kiulaiiini!.

Jijini Dar Es Salaam, NBC ilimfukuza kazi Bi. SARAH kwa kutoonekana kazini kwa siku 5 mfululizi. Aidha, kamatakamata ilianza ambapo wafuatao walikamatwa na kuhusishwa na wizi huo: Bw. ROMANIUS PETER NDANZI(43), Mdhibiti wa Fedha za Kigeni, NBC "Foreign Branch", Bw. ERNEST JOHN MWENEWANDA(40), Meneja mauzo KLM, HAROON DAUD(35), Mfanyabiashara. Washtakiwa hawa, tarehe 19.11.1987, walifikishwa Kisutu kwa "Pilato" Mh. JUMA MUSTAPHA JIBREA. Waliomba dhamana wakanyimwa. Wakakata rufaa Mahakama Kuu. Tarehe 5.1.1987, Jaji LUHEKELO KYANDO, aliwanyima dhamana na kueleza, kwa uchungu na uzalendo, kwamba:

*"Kiini cha kesi hii ni moja ya matukio ambayo yameshtua sana umma kuona kwamba mamilioni ya fedha yanaibwa. Ni maoni yangu kuwa itakuwa kinyume na hisia za jamii ikiwa mahakama itachukua msimamo tofauti na usiokuwa na mwelekeo wa hisia sahihi kuhusu vitendo hivi"*.
Msimamo huu uliakisi kilichoelezwa na aliyekuwa Waziri wa sheria, Mama JULLIE MANNING, tarehe 17.1.1976, kwamba: *"Ingawa Mahakama hazipendelei upande wowote, hiyo haina maana kwamba zisijali nini kinatokea nchini"*.

Serikali ilituma Kenya Hati ya kuomba SARAH na TOROHA warudishwe nchini(Extradition) kwani nchi hizi zina makubaliano hayo ya aina hiyo. Hati hiyo iliwasilishwa na SP PETER MWANGI mahakamani saa 2.30 asubuhi ijumaa, tarehe 15.1.1988 mbele ya Hakimu Mwandamizi, Mh JOSEPH MANGO na kisha maombi hayo yakaanza kusikilizwa.

Tarehe 29.11.1987, mahakama hiyo ikatoa uamuzi kuwa, kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, SARAH arudishwe Tanzania kujibu mashtaka lakini ikamuachia huru TOROHA. Baada tu ya kuachiwa, mbio alizotimua TOROHA, hata USAIN BOLT angesubiri!.

Siku ya jumanne, saa 6 mchana, tarehe 2.2.1988, SARAH alikabidhiwa kwa maafisa wa Tanzania mpakani Namanga na kukimbizwa "wanguwangu" na magari 5 ya polisi hadi Dar Es Salaam.
SARAH alifikishwa mahakama ya Kisutu saa tatu asubuhi, siku ya Jumatano, tarehe 10.2.1988 chini ya ulinzi mkali. Mahakama hiyo ilikuwa imefurika mno huku barabara ya Bibi Titi ikifungwa kwa muda kwani wananchi wengi walitoroka makazini kwenda kumuona SARAH anafananaje na kusikia aliwezaje kuiba kitita chote hicho!.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mh. JOSEPH MASANCHE, Bi. SARAH alisomewa mashtaka 5 na SSP EDWIN ABRAHAM MAN. Bi. SARAH alikuwa akitetewa na Dr. MASUMBUKO ROMAN LAMWAI, mmoja wa mawakili bora kabisa kuwahi kutokea nchini.

Bi. SARAH aliushangaza umati uliofurika, pale bila kupepesa macho, kutingisha pua wala kutikisa maskio, alipokiri mashtaka yote 5! Hakimu MASANCHE nae pia alipigwa butwaa na ikabidi amuulize kama ameelewa vizuri mashtaka ambapo "alikomaa" na kusema anaelewa na anakiri ni kweli alienda makosa hayo!.

Mh MASANCHE, baada ya kusikiliza pande zote 2 kuhusu adhabu, akasoma hukumu iliyochukua robo saa tu ambapo alimuhukumu SARAH kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa na makosa yote kwenda pamoja hivyo angetumikia miaka 7 tu na pia akamuamuru arudishe fedha hizo mara moja. Mh MASANCHE alin'gaka- *"Hakuna kitu kibaya kama wizi wa fedha za kigeni ambazo Taifa linazihitaji sana"*.

Upande wa mashtaka hakuridhika na adhabu hiyo "kiduchu" hivyo ukakata rufaa Mahakama Kuu kuomba adhabu hiyo iwe kwa kufuatana na sio kwa pamoja. Aliyekuwa Jaji Kiongozi, Mh. NASSOR MZAVAS ndiye aliyesikiliza rufaa hiyo huku jamhuri ikiwakilishwa na Bw. KULWA SATO MASSABA na Dr. LAMWAI akimuwakilisha SARAH.

Saa 4 asubuhi, Ijumaa ya tarehe 19.2.1988, Mh MZAVAS alitoa hukumu. Baada ya kuisoma hukumu hiyo kwa dakika 45, huku umati ukisubiri kwa hamu, Mh. MZAVAS "aliinama na kujifanya kama anajikuna" kisha "akampiga SARAH mvua 28"! SARAH hakuamini macho yake na kubaki amebun'gaa! Mh. MZAVAS akamalizia- *"Hii ni hasara ya kiuchumi ambayo inaiathiri nchi. Fedha hizo kidogo za kigeni nchi ilizofaulu kujiwekea akiba kwa kujikidhi sana, ndio inalolifanya kosa la kuiba fedha za kigeni kutisha. Wizi huu ulipotangazwa na RTD, Mahakama pia ilisononeka na kufadhaika sana kwa kuibwa kwa fedha hizo za kigeni kwani Mahakama nayo ni sehemu ya jamii"*.

"Upigaji" huu wa ulikuwa umepangwa na wapenzi hao wawili, SARAH na TOROHA. TOROHA alikuwa ni kijana mtanashati aliyezaliwa Mbegani, Bwagamoyo mwaka 1948. Baba yake aliwahi kufanya kazi Ikulu na kisha akawa Afisa wa ubalozi Japan na Uholanzi miaka ya mwanzoni ya Uhuru na alikuwa na uwezo wa kifedha. Mwaka 1967, baada ya kuzinguliwa na siasa ya Ujamaa ambapo nyumba yake ilitaifishwa, aliacha kazi na kutimkia Ujerumani na kufanya biashara ya mkahawa na duka la vinyago.

Mwaka 1979, Bw. TOROHA, akiwa kijana wa miaka 31, alimuoa Mkenya, Bi. ELIZABETH WANJIRU na wakaishi Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Kenya. TOROHA alikuwa akija nchini mara mojamoja hivyo akaanza urafiki na Bi. SARAH aliyekuwa binti mdogo mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Zanaki jijini. SARAH, baadaye, aliajiriwa NBC na kupanda vyeo hadi kuwa Msimamizi, Idara ya Fedha za Kigeni.

TOROHA aliingia nchini tarehe 11.10.1987 na kufanya "mchongo wa upigaji" na "Mpango wa kando" wake, Bi. SARAH. Ili kufanikisha dili la upigaji na kusepa nje ya nchi bila kushtukiwa, Bi. SARAH alishirikiana na maafisa wasio waaminifu wa "Immigration" na kubadili majina yake na ya wanawe na kupata "passports" mpya tarehe 28.10.1987. "Passport" ya SARAH yenye Na. 220130 ikawa na jina KHADIJA ALI MKIMBAU. "Passports" za wanawe zikawa na majina mapya 1.HAPPINESS SIMBAULANGA-(JAMILA ISMAEL HASSAN), 2. SIMBA SIMBAULANGA- (HALFAN ISMAIL HASSAN), 3. BLANDINA SIMBAULANGA-(JENIPHER ISMAEL HASSAN).

Kisha, SARAH "akapiga" hundi za kusafiria 1,100 zenye thamani ya $ 390.000 na hundi 200 zenye thamani ya £ 20.000. Fedha hizo 'alizipiga' mara 3 kati ya tarehe 19.10.1987 na 29.10.1987. Kwa wakati huo, hizo zilikuwa ni fedha nyingi sana. Baada ya mchongo kukamilika, SARAH na TOROHA walichukua vyumba 2 katika hotel maarufu sana ya Skyway iliyokuwa makutano ya Ohio na Samora.

Chumba kimoja kilikuwa chao na kingine cha watoto wa SARAH ambako walilala kwa usiku mmoja wa Ijumaa, tarehe 30.10.1987. Usiku wa Ijumaa hiyo, SARAH na TOROHA walienda ukumbi wa White House "kushangilia ushindi" ambako bendi ya Marquis du Zaire chini ya Babu Seya iliwapagawisha vilivyo!.

Tarehe 31.10.1987, TOROHA, kin'gast chake SARAH na watoto wake 3 walikwea pipa la ATC kwenda Kenya. Walipotua tu Jomo Kenyata International Airport, wakatumia hundi zenye thamani ya $ 2700 kununua tiketi 5 za KLM na wakaenda Amsterdam na kisha London. Wakiwa London UK, waliofanya "transactions" nyingi "Baclays bank" na tarehe 2.11.1988 wakanunua tiketi 5 za KLM ili waondoke kuelekea Kenya tarehe 5.11.1987. Tarehe 3 na 4 ilikuwa ni "kujirusha" tu nchi ya Malkia ie *Kazi na Bata*!.

Tarehe 5.11.1987 walikwea KLM na kufika Kenya tarehe 6.11.1987. Nchini Kenya walifanya matanuzi na manunuzi ambapo TOROHA alitumia $ 260,000 kununua magari (mini-bus 4 na pick up 1) na yote akayasajiri kwa jina la SARAH. TOROHA, alipokuwa akitaka kununua magari mengine ndipo aliponyakwa na mamwela katika ofisi za Toyota tarehe 13.11.1987! .

Huu ndio mkasa wa Bi. SARAH MARTIN SIMBAULANGA
 
Ushimen Asante kwa mchango maridhawa.
Je unayakumbuka matukio ya uchunaji ngozi kule MBOZI enzi hizo MBOZI ikiwa ni moja ya wilaya za mkoa wa Mbeya?
Mkasa mzima unafuata
 
Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40).

Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha nyingi kiasi kile!.

Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha nyingi kiasi hicho. Kwa wengi, ilikuwa ni simanzi kubwa sana na haikushangaza basi pale Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la vijana uliokuwa ukifanyika Singida kutoa wito kuwa uongozi wote wa juu wa NBC "Ufyekelewe mbali"!.

Ofisi ya DCI, mara moja, ilituma taarifa (Interpol) nchi mbalimbali ili zisaidie kuwakamata "mabandido" hao.

Hatimaye, majira ya saa 9 alasiri, siku ya Ijumaa, tarehe 13.11.1987, Bw. TOROHA akabambwa kwenye ofisi ya magari ya Toyota jijini Nairobi, Kenya akiwa kwenye mishemishe ya ununuzi wa magari.

"Mandata" walipombana aeleze kuhusu aliko Bi. SARAH, Bw. TOROHA hakuwa na namna zaidi ya kuwapeleka chumba na. 322 cha hotel maarufu ya Jacaranda. "Mandata" hao, wakiwa na TOROHA, waliingia chumba hicho na kumkamata Bi. SARAH kiulaiiini!.

Jijini Dar Es Salaam, NBC ilimfukuza kazi Bi. SARAH kwa kutoonekana kazini kwa siku 5 mfululizo. Aidha, kamatakamata ilianza ambapo wafuatao walikamatwa na kuhusishwa na wizi huo: Bw. ROMANIUS PETER NDANZI(43), Mdhibiti wa Fedha za Kigeni, NBC "Foreign Branch", Bw. ERNEST JOHN MWENEWANDA(40), Meneja mauzo KLM, HAROON DAUD(35), Mfanyabiashara. Washtakiwa hawa, tarehe 19.11.1987, walifikishwa Kisutu kwa "Pilato" Mh. JUMA MUSTAPHA JIBREA. Waliomba dhamana wakanyimwa. Wakakata rufaa Mahakama Kuu. Tarehe 5.1.1988, Jaji LUHEKELO KYANDO, aliwanyima dhamana na kueleza, kwa uchungu na uzalendo, kwamba:
"Kiini cha kesi hii ni moja ya matukio ambayo yameshtua sana umma kuona kwamba mamilioni ya fedha yanaibwa. Ni maoni yangu kuwa itakuwa kinyume na hisia za jamii ikiwa mahakama itachukua msimamo tofauti na usiokuwa na mwelekeo wa hisia sahihi kuhusu vitendo hivi".

Msimamo huu uliakisi kilichoelezwa na aliyekuwa Waziri wa sheria, Mama JULLIE MANNING, tarehe 17.1.1988, kwamba: "Ingawa Mahakama hazipendelei upande wowote, hiyo haina maana kwamba zisijali nini kinatokea nchini".

Serikali ilituma Kenya Hati ya kuomba SARAH na TOROHA warudishwe nchini(Extradition) kwani nchi hizi zina makubaliano hayo ya aina hiyo. Hati hiyo iliwasilishwa na SP PETER MWANGI mahakamani saa 2.30 asubuhi ijumaa, tarehe 15.1.1988 mbele ya Hakimu Mwandamizi, Mh JOSEPH MANGO na kisha maombi hayo yakaanza kusikilizwa.

Tarehe 29.11.1987, mahakama hiyo ikatoa uamuzi kuwa, kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, SARAH arudishwe Tanzania kujibu mashtaka lakini ikamuachia huru TOROHA. Baada tu ya kuachiwa, mbio alizotimua TOROHA, hata USAIN BOLT angesubiri!.

Siku ya jumanne, saa 6 mchana, tarehe 2.2.1988, SARAH alikabidhiwa kwa maafisa wa Tanzania mpakani Namanga na kukimbizwa "wanguwangu" na magari 5 ya polisi hadi Dar Es Salaam.

SARAH alifikishwa mahakama ya Kisutu saa tatu asubuhi, siku ya Jumatano, tarehe 10.2.1988 chini ya ulinzi mkali. Mahakama hiyo ilikuwa imefurika mno huku barabara ya Bibi Titi ikifungwa kwa muda kwani wananchi wengi walitoroka makazini kwenda kumuona SARAH anafananaje na kusikia aliwezaje kuiba kitita chote hicho!.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mh. JOSEPH MASANCHE, Bi. SARAH alisomewa mashtaka 5 na SSP EDWIN ABRAHAM MAN. Bi. SARAH alikuwa akitetewa na Dr. MASUMBUKO ROMAN LAMWAI, mmoja wa mawakili bora kabisa kuwahi kutokea nchini.

Bi. SARAH aliushangaza umati uliofurika, pale bila kupepesa macho, kutingisha pua wala kutikisa maskio, alipokiri mashtaka yote 5! Hakimu MASANCHE nae pia alipigwa butwaa na ikabidi amuulize kama ameelewa vizuri mashtaka ambapo "alikomaa" na kusema anaelewa na anakiri ni kweli alienda makosa hayo!.

Mh MASANCHE, baada ya kusikiliza pande zote 2 kuhusu adhabu, akasoma hukumu iliyochukua robo saa tu ambapo alimuhukumu SARAH kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa na makosa yote kwenda pamoja hivyo angetumikia miaka 7 tu na pia akamuamuru arudishe fedha hizo mara moja. Mh MASANCHE alin'gaka- "Hakuna kitu kibaya kama wizi wa fedha za kigeni ambazo Taifa linazihitaji sana".

Upande wa mashtaka hakuridhika na adhabu hiyo "kiduchu" hivyo ukakata rufaa Mahakama Kuu kuomba adhabu hiyo iwe kwa kufuatana na sio kwa pamoja. Aliyekuwa Jaji Kiongozi, Mh. NASSOR MZAVAS ndiye aliyesikiliza rufaa hiyo huku jamhuri ikiwakilishwa na Bw. KULWA SATO MASSABA na Dr. LAMWAI akimuwakilisha SARAH.

Saa 4 asubuhi, Ijumaa ya tarehe 19.2.1988, Mh MZAVAS alitoa hukumu. Baada ya kuisoma hukumu hiyo kwa dakika 45, huku umati ukisubiri kwa hamu, Mh. MZAVAS "aliinama na kujifanya kama anajikuna" kisha "akampiga SARAH mvua 28"! SARAH hakuamini macho yake na kubaki amebun'gaa! Mh. MZAVAS akamalizia- "Hii ni hasara ya kiuchumi ambayo inaiathiri nchi. Fedha hizo kidogo za kigeni nchi ilizofaulu kujiwekea akiba kwa kujikidhi sana, ndio inalolifanya kosa la kuiba fedha za kigeni kutisha. Wizi huu ulipotangazwa na RTD, Mahakama pia ilisononeka na kufadhaika sana kwa kuibwa kwa fedha hizo za kigeni kwani Mahakama nayo ni sehemu ya jamii".

"Upigaji" huu wa ulikuwa umepangwa na wapenzi hao wawili, SARAH na TOROHA. TOROHA alikuwa ni kijana mtanashati aliyezaliwa Mbegani, Bwagamoyo mwaka 1948. Baba yake aliwahi kufanya kazi Ikulu na kisha akawa Afisa wa ubalozi Japan na Uholanzi miaka ya mwanzoni ya Uhuru na alikuwa na uwezo wa kifedha. Mwaka 1967, baada ya kuzinguliwa na siasa ya Ujamaa ambapo nyumba yake ilitaifishwa, aliacha kazi na kutimkia Ujerumani na kufanya biashara ya mkahawa na duka la vinyago.

Mwaka 1979, Bw. TOROHA, akiwa kijana wa miaka 31, alimuoa Mkenya, Bi. ELIZABETH WANJIRU na wakaishi Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Kenya.

TOROHA alikuwa akija nchini mara mojamoja hivyo akaanza urafiki na Bi. SARAH aliyekuwa binti mdogo mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Zanaki jijini. SARAH, baadaye, aliajiriwa NBC na kupanda vyeo hadi kuwa Msimamizi, Idara ya Fedha za Kigeni.

TOROHA aliingia nchini tarehe 11.10.1987 na kufanya "mchongo wa upigaji" na "Mpango wa kando" wake, Bi. SARAH. Ili kufanikisha dili la upigaji na kusepa nje ya nchi bila kushtukiwa, Bi. SARAH alishirikiana na maafisa wasio waaminifu wa "Immigration" na kubadili majina yake na ya wanawe na kupata "passports" mpya tarehe 28.10.1987. "Passport" ya SARAH yenye Na. 220130 ikawa na jina KHADIJA ALI MKIMBAU. "Passports" za wanawe zikawa na majina mapya 1.HAPPINESS SIMBAULANGA-(JAMILA ISMAEL HASSAN), 2. SIMBA SIMBAULANGA- (HALFAN ISMAIL HASSAN), 3. BLANDINA SIMBAULANGA-(JENIPHER ISMAEL HASSAN).

Kisha, SARAH "akapiga" hundi za kusafiria 1,100 zenye thamani ya $ 390.000 na hundi 200 zenye thamani ya £ 20.000. Fedha hizo 'alizipiga' mara 3 kati ya tarehe 19.10.1987 na 29.10.1987. Kwa wakati huo, hizo zilikuwa ni fedha nyingi sana. Baada ya mchongo kukamilika, SARAH na TOROHA walichukua vyumba 2 katika hotel maarufu sana ya Skyway iliyokuwa makutano ya Ohio na Samora. Chumba kimoja kilikuwa chao na kingine cha watoto wa SARAH ambako walilala kwa usiku mmoja wa Ijumaa, tarehe 30.10.1987. Usiku wa Ijumaa hiyo, SARAH na TOROHA walienda ukumbi wa White House "kushangilia ushindi" ambako bendi ya Marquis du Zaire chini ya Babu Seya iliwapagawisha vilivyo!.

Tarehe 31.10.1987, TOROHA, kin'gast chake SARAH na watoto wake 3 walikwea pipa la ATC kwenda Kenya. Walipotua tu Jomo Kenyata International Airport, wakatumia hundi zenye thamani ya $ 2700 kununua tiketi 5 za KLM na wakaenda Amsterdam na kisha London. Wakiwa London UK, waliofanya "transactions" nyingi "Baclays bank" na tarehe 2.11.1988 wakanunua tiketi 5 za KLM ili waondoke kuelekea Kenya tarehe 5.11.1987. Tarehe 3 na 4 ilikuwa ni "kujirusha" tu nchi ya Malkia ie Kazi na Bata!.

Tarehe 5.11.1987 walikwea KLM na kufika Kenya tarehe 6.11.1987. Nchini Kenya walifanya matanuzi na manunuzi ambapo TOROHA alitumia $ 260,000 kununua magari (mini-bus 4 na pick up 1) na yote akayasajiri kwa jina la SARAH. TOROHA, alipokuwa akitaka kununua magari mengine ndipo aliponyakwa na mamwela katika ofisi za Toyota tarehe 13.11.1987! .
 
Huyu hapa
1604671364815.png
 
Kuna kipindi miaka ya 80 walitoroka majambazi kama 21 hivyo waliokuwa gerezani, sikumbuki kama ni ukonga au keko.

Tukio hilo lilizua taharuki kubwa sana katika jiji la Dsm na kusababisha kuwepo kwa msako mkali wa Polisi/Jkt/Mgambo na road blocks ktk maeneo mengi.

Kati ya majambazi waliotoroka ambao picha zao zilichapishwa ktk magazeti, nawakumbuka wawili ambao walijulikana kwa majina ya Leloo, na mwingine Hamisi Shija "nyau." nadhani walikuja kupatikana na kuuwawa na polisi.

Wazee wangu wa jiji la Dsm wanaweza kutukumbusha tukio hilo.

cc Mohamed Said, Pascal Mayalla, Nguruvi3, Kichuguu, Kiranga
 
Hivi alishamaliza miaka yake 28, na kutoka jela?
 
Pascal Mayalla, Kiranga, Mohamed Said, Nguruvi3, Richard,

..tukio la miaka ya 80 la majambazi kutoroka gerezani Dsm haumna kumbukumbu nalo?
Mkuu JokaKuu , kumbukumbu zipo, mimi nilikuwa darasa la 6, na tayari ni mzoefu wa kusoma magazeti na kusikiliza habari, kufuatia kufuatilia kesi ya Mauaji Mwanza, ambapo Mzee wangu, Andrew Mayalla, ndiye alikuwa RSO wa Mwanza, kesi ili drag toka 1979 hadi 1980 na Jaji akiwa huyu huyo Jaji Mzavas, PP alikuwa ni Kulwa Satto Masaba, Mzee alitetewa na wakili Murtaza Lakha, na ndio the one and only aliyenusurika!.

Enzi hizo tukiisha Drive In flats, nex door kwetu ni nyumba ya Banyikwa, kulikofanyikia vikao vya mambo mambo!.

Watuhumiwa kadhaa wa kesi ya uhaini kutaka kumpindua Nyerere, walitoroka Ukonga maximum prison, akiwemo Pius Lugangira, alias Father Tom, Hatibu Maghee, Capt. Eugene Maganga na wajeshi wengine wawili, sikumbuki majina yao, lakini nadhani kuna Capt. Kadege na Ngalomba, wakatorokea Kenya.

Kule Kenya, Uncle Tom, machale yakamcheza, akatimkia UK.

Huku Kenya jeshi likakiwasha, Staff Sergeant Hezekia Ochuka, na Private Pancras Oteyo Okumu, wakatorokea Tanzania.

Kufuatia Tanzania na Kenya kuwa na mkataba wa kubadilishana wahalifu, kina Maganga wakaletwa na sisi tukawapo Wakenya jamaa zao, ambao kule walipokelewa kwa hukumu za kifo, na kuwa executed immediately!. Hawa wa kwetu, walipigwa mvua kadhaa, Ben alipoingia, akawasamehe.

Story zao ziko kwenye mabandiko kibao humu.

P
 
..shukrani.

..kuna matukio mawili ya wafungwa / mahabusu kutoroka gereza la Keko au Ukonga.

..wako waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za uhaini ambao umewaelezea hapa.

..halafu wapo wengine walitoroka ambao walikuwa ni majambazi sugu.

..ninaowakumbuka mimi ni Leloo, na Hamisi Shija "nyau". Nadhani idadi ya majambazi waliotoroka ilikuwa kati ya 10 na 20.

..nafahamu habari za kesi ya uhaini ya kina Hatty Maghee na wenzake iko ktk mabandiko mbalimbali hapa JF. Lakini sina kumbukumbu ya yeyote kuandika kuhusu majambazi waliotoroka gerezani na kutishia usalama wa jiji la Dsm miaka ya 80.

NB:

..nadhani Jaji Kiongozi Nassoro Mzavas alihukumu kesi nyingi nzito. Nilibahatika kumuona nje ya mahakama.
 
Back
Top Bottom