Sarafu mpya yazinduliwa Kenya! Ipo sarafu ya shilingi moja

Kumbe hawana 200 na 500 za sarafu alafu noti yao kubwa ndo hiyo 1000?
Pesa yao iko juu ya ya kwetu sisi tunakaribiana na Uganda. Pesa ikiwa kwenye sarafu maana yake thamani yake ni ndogo kuliko noti
 
unajua yote Haya ni majina tu
Ukichunguza kwa Sana utagundua thamani ni moja kwa mfano kiatu utachonunua tz kwa 25,000 Kenya ukakipata kwa 1100 Na Washington ukakipata kwa dola 10 Na India ukakipata kwa rupia 700 utagundua kuwa ni sawa kwa thamani wala hakuna tofauti
 
Uzuri wa sarafu yoyote ile ni kwenye thamani yake tu, hongera zao naona wenzetu noti kubwa ni 1000, sijui sawa na shilingi ngapi za Tanzania kwa mnaojua.
Je thamani ya ksh ni uthibitisho wa uimara wa uchumi wa Kenya?
 
Je thamani ya ksh ni uthibitisho wa uimara wa uchumi wa Kenya?
Ngoja waje wataalamu wa uchumi, ila naamini nguvu ya sarafu inachangiwa na uchumi wa nchi husika ndio maana unavyoporomoka na sarafu ya nchi husika lazima iporomoke......sijawahi kusikia nchi inaporomoka uchumi halafu sarafu yake inapanda.
 
unajua yote Haya ni majina tu
Ukichunguza kwa Sana utagundua thamani ni moja kwa mfano kiatu utachonunua tz kwa 25,000 Kenya ukakipata kwa 1100 Na Washington ukakipata kwa dola 10 Na India ukakipata kwa rupia 700 utagundua kuwa ni sawa kwa thamani wala hakuna tofauti


Muhimu zaidi ni kuhakikisha sarafu inabaki imara, kitu ambacho US wamefanikiwa kwa decades sasa,
kushuka kwa thamani ya sarafu kunaathiri sana uchumi, hasa kwa nchi kama Tanzania ..
Kitu serikali yetu imefeli kwa miaka mingi ni kushuka kwa thamani ya shiling progressively, hii inashusha exchange rate na gdp kwa ujumla, chumi zilizokomaa kama Japan ama China zinaweza control hii kitu, zinaweza shusha na kupandisha thamani na uchumi hauyumbi..
 
sisi zetu ziko makumbusho Hongereni sana nguvu ya pesa yenu inajulikana miaka yote , nitawatania mengine sio kwenye nguvu ya pesa yenu.View attachment 964324
1985-88 nikiwa sm nilikuwa maarufu Sana shuleni kuwa na hela. Nilikuwa nikifanya vibarua vya kubeba tofali, mchanga na kuosha magari. Hiyo thumni unanunua andazi la kutengenezwa kwa mchanganyo wa ndizi mbivu na unga aka vimbama na viazi vitamu kwa sent 10@. Ilikuwa Poa Sana. Ukipewa gwala umenunua dagaa, mafuta, kitunguu na mafuta ya taa 1986. Siku hz hatareeee
 
Back
Top Bottom