Sangara na wachina

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
4,134
3,757
Hivi karibuni biasharz ya sangara imekuwa kubwa sana mpaka bei ya kilomoja imefikia Tsh 5000 huku mawenzi mkoani Morogoro.

Nimedadisi nimeambiwa ni kutokana na mautumbo ya koromeo (Bondo) ni dili na wachina wananunua kilomoja kwa Tsh 200,000.

Wanadai ukinunua kilo miamoja unapata gram chahche za hicho koromeo na hivyo kuwafanya wanaponunua samaki hubaki wakiwa hawana thamani tena.

Kwa mnaouza tujuzeni kuna fursa tujiunge pamoja na kilo moja ya bondo i ahitaji kilo ngapi za sangara?
 
Bondo. kwanza unaposema kilo moja ya samaki sangara sawa na tsh 5000 hapo ni bei ya beach na nibei isiyorafiki kwa wavuvi. Sangara ameshuka bei kiasi kwamba hata wavuvi wanatamani kuachana nae. Watakaobaki wanamvua sangara kwa hizi bei zilizosawa na sigara ni wale wa uvuvi haram usiohitaji mtaji mkubwa. Swala la bondo hiyo ni mfumo mrefu sana kuuelezea. Mimi na mfanya kazi katika vyombo vya uvuvi labda nitakuelezea machache ninayoyajua kuhusu bondo. Kwa mujibu wa bei za sangara mwaka 2017 kuna sangara alikuwa anauzwa mpaka tsh 12,000 kwa kilo ama zaidi ya hapo. Ila toka selikari ipige marufuku uvuaji wa sangara wenye urefu wa zaidi ya sentimita85 ndipo bei ya sangara ikaporomoka kufikia hizo bei ulizoorodhesha hapo juu
 
Bei za bondo zinatokana na ukubwa wa bondo. Zinaanzia tsh 150 kwa gram mpaka tsh 1700 kwa gram. kwa lugha nyingine ni kwamba kilo moja ya bondo yaweza kukupa zaidi ya milion moja kutokanna na ukubwa wa bondo lenyewe
 
sangara wa mwanza au wa wapi maans huku nauziwa kilo 8000 kila siku na nimeshazoea
 
Back
Top Bottom