Sanga one atangaza nia ya kugombea uwenyekiti ccm

Mar 23, 2012
64
13
<p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal">
<p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">Na Stephano Mango, Songea</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">KADA wa Chama cha Mapinduzi(Ccm) Halmashauri ya Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma Golden Sanga (Sanga One) ametangaza nia ya kugombea Uwenyekiti wa
chama hicho Wilaya ya Songea katika uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika mapema
mwezi Septemba mwaka huu</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya
Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea Golden Sanga alisema kuwa ameamua
kugombea nafasi hiyo ili kuweza kurudisha heshima ya Chama cha Mapinduzi mjini
hapa</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">Sanga alisema kuwa kila kukicha mvuto wa Ccm miongoni mwa jamii
umekuwa ukipungua kutokana na matendo maovu yasiyokuwa ya kimaadili yanayofanywa
na Viongozi wa chama hicho ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wananchi na
wanachama wa chama hicho</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">Alieleza kuwa kutokana na hali hiyo kumesababisha kata 6 kati ya 21
kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu
wa madiwani, wabunge na Urais wa mwaka 2010</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">Alieleza zaidi kuwa amejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na
viongozi wenzake watakaochaguliwa kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama
katika uchaguzi unaoendelea kufanyika mwaka huu ili kuweza kukijenga chama na
kuleta ushindi stahiki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa
2015</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri" _yuid="yui_3_1_1_3_134476522972885">Kwa mujibu wa taarifa ya Chama
cha Mapinduzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuwa wagombea wana haki ya
kutangaza nia za kugombea nafasi wanazozitaka ndani ya chama ambapo kwa nafasi
ya uwenyekiti wa Wilaya fomu zinatolewa kuanzia agosti&nbsp;22 hadi 30 ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi septemba mwaka huu</font>&nbsp;
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri" _yuid="yui_3_1_1_3_134476522972883">Uchunguzi uliofanywa na gazeti
hili umebaini kuwa waliotangaza nia hadi sasa ni Gerald Mhenga ambaye ni Katibu
wa mipango na uchumi wa Ccm Wilaya ya Songea na Golden Sanga ambaye amewahi
kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwemo udiwani wa kata ya
Bombambili katika halmashauri hiyo</font>
</font><p style="margin: 0in 0in 10pt;" class="yiv78724396MsoNormal"><font size="4"><font face="Calibri">MWISHO</font> </font></p>
 
Back
Top Bottom