Sanga mbunge wa Makete ni Mwalimu wa wale Wabunge wa kipindi kimoja

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MHE SANGA ANAJARIBU KUWAFUNDISHA WABUNGE WA MUDA MFUPI.

Na Elius Ndabila

Ninawasalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni muda muda kidogo sijaandika kama nilivyokuwa nafanya mwanzo. Yapo majukumu ambayo yamenibana nakosa nafasi nzuri ya kuwa kwenye social network kama hizi.

Festo Sanga ni Mbunge wa Jimbo la Makete aliyeshinda kwenye Uchaguzi wa 2020. Ni Mbunge kijana, Mkalimu, Mwenye maono na Mcheshi. Lakini ninamtazama kama sehemu ndogo ya Wabunge wachache waliokuja kuwafundisha Wabunge wanaokaa Bungeni kipindi kimoja.

Niliwahi kuandika sifa za Mbunge anayekaa muda mrefu madarakani na sifa za Mbunge anayekaa muda mfupi madarakani. Lakini sifa Kuu ya Mbunge anayekaa miaka mitano tu madarakani ni yule anayejua Ubunge ni wa Kwake, ni yule anayezugukwa na Watengeneza Majungu na tatu ni yule ambaye hata Ubunge wake aliupata kwa Bahati nasibu. Hawa hukaa muda mfupi.

Mhe Festo Sanga toka ameanza Ubunge amekuwa ni Mbunge aliyeutafsiri Ubunge kuwa si wa Kwake, bali ni wa Wananchi wa Makete. Kiufupi ni Mbunge ambaye kila mwanamakete anamfikia.

Shughuli za Bunge zikiisha Utamkuta Sanga Jimboni akifanya shughuli zote wanazofanya Wananchi. Anapoenda Vijijini kwenye ziara havai suti, anavaa nguo za KAZI kwa kuwa anatamani kufanya kile ambacho anawakuta watu wanafanya. Hataki kuwa boss wa kuelekeza. Ziara zake hachagui Wananchi wa kuwafikia anaenda hata Vijiji ambavyo watsngulizi wake hawakuwahi kufika. Hivyo si sehemu ya Wabunge wa mabega na Cheo, ni Mbunge wa watu.

Simuoni kama Mhe Sanga kama Mungu atampa afya njema iwapo ndani ya CCM atapata Upinzani mkali. Ninamuona kama Mbunge ambaye atateleza tu kwa kuwa ameshajipambanua kwenye uwakilishi wa watu.

Wale Wabunge wa miaka mitano mitano ninadhani chukueni darasa kwa Mhe Sanga. Elimu haina mwisho. Hata kama Ubunge si Mwanasiasa mzuri na Ubunge ulikuja tu by emergency, lakini bado unaweza kupindua matokeo endapo utachukua hata mbinu mbili za Mhe Sanga.

Nimemchukua Sanga kama sample ya Damu Mpya zilizoingia Bungeni na wanaonyesha mfano bora na dhana halisi ya Uwakilishi. Ningeweza hata kuchukua mfano wa Mhe Masache Mbunge wa Lupa mkimya, mpole lakini mtu wa vitendo. Mhe Kwagilwa kule Tanga ni mifano ya Vijana utawaona wanavyopambana, Mhe Condesta Mbunge wa Momba Moja ya Wabunge wazungumzaji wakubwa Bungeni, Mhe Gulamali few to mention.

Orodha ya Wabunge hawa wapya bila shaka nao walichukua mifano kwa kaka zao kama vile Mhe Mulugo, Mhe Bashe, Mhe Rizione n.k ambao majimboni mwao Wana technic nyingi za kushinda ikiwepo namna ya kuutafsiri Ubunge wao.

Mbunge sahihi ni yule ambaye anaamini kuwa Wananchi ndio Mabosi wake, si yule anayejua kuwa yeye ni boss wa Wananchi. Mbunge bora ni yule baada ya Uchaguzi anahakikisha anawaunganisha watu wote, na si kuwagawa na kubaki na kakundi anakokaamini. Mbunge bora na sahihi ni yule ambaye baada ya Bunge anaenda kuwapa mrejesho Wananchi na kuchukua kero Mpya na si Mbunge ambaye anatumia uzoefu wake kuzungumza hoja za Wilayani kwake. Lakini Mbunge bora ni yule anawaheshimu viongozi wa Chama kilichompa Ubunge na si yule ambaye anataka Viongozi wamheshimu.
 
Hata Filikunjombe alikuwa mbunge wa wanaludewa,CCM hatukumpenda kasi yake yakuwakomboa wananchi.Mtaji wa siasa ni umasikini wa wananchi.
 
Mzee wa kujipendekeza kwa kiwango cha Lami mpaka kukaa bungeni alikuwa anasumbua awekwe seat za mbele
 
Back
Top Bottom