"Sanduku la Maoni". Je maoni yanafanyiwa kazi?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,453
3,203
Kuna utamaduni mzuri (sijui kama upo kwa sababu za miongozo), na uliozoeleka katika taasisi, hususani, za umma wa kuchukua maoni kutoka kwa watu wanaopata huduma au wadau kwa ujumla.
Kwa kawaida kuna sanduku linalowekwa eneo la wazi ili kurahisisha ukusanyaji wa maoni kwa njia ya maandishi.
Binafsi napata kujiuliza; je maoni yanayokusanywa yanafanyiwa kazi?; je wanaotarajiwa kutoa maoni wanatoa maoni?
Najiuiliza hivyo kwa kuwa, katika taasisi karibu zote za umma kumekuwa, na naamini kutaendelea, na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wanaopata huduma na wadu wengine.
Ikiwa kama maoni hayafanyiwi kazi, badala yake yanachomwa jalalani, hakuna haja ya kutoa maoni.
Wengi ni mashahidi, tumeshuhudia watu wanaopata huduma wakidiriki kwenda kwa mamlaka za juu ili kupeleka vilio vyao vya muda mrefu juu ya uduni wa huduma katika taasisi fulani fulani, wakiamini suluhu itapatikana.
Tunakoelekea tunaimarisha utamaduni sugu wa kutofanyia kazi maoni ya wadau, kitu ambacho ni hatari sana.
Ikiwa kama umewahi kutoa maoni juu ya uduni wa huduma au chochote kutoka kwa taasisi ya umama na yakafanyiwa kazi, naomba utujulishe Watanzania wenzako; ni maoni gani, yalifanyiwa kazi baada ya muda gani?
Ahsante kwa mchango utakaotoa.
 
Kuna sehem ina hiko kisanduku cha maoni na ilibaki kidogo niweke maoni yangu na mimi baada ya kukereka na huduma zao mbovu...kun siku nikamuuliza jamaa mmoja anafanya kazi hapo kuhusu hiko kisanduku akaniambia : "hiko kisanduku funguo zake zilipoteaga tangu mwaka juzi, mpaka leo bado tunasubiri fungu kutoka ofisini tuite fundi aje atubadilishie kitasa chake"...

basi kikaratasi changu cha maoni nikatia mfukoni nakatambaa zangu..
 
hizo formality za ofisi tu. Usipoteze muda kuandika chochote na kutumbukiza humo. Rubbish
 
Back
Top Bottom