Sanamu la Yesu Mweusi Lasababisha Watu 708 Wajeruhiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sanamu la Yesu Mweusi Lasababisha Watu 708 Wajeruhiwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Watu 708 wamejeruhiwa nchini Philippines wakati mamilioni ya watu walipopigania kuligusa sanamu la Yesu mweusi ambalo linaaminika kuwa lina nguvu za miujiza.
  Tamasha la kila mwaka la waumini wa kanisa katoliki nchini Phillippines kuligusa sanamu la Yesu mweusi limeacha watu 708 wakipatiwa matibabu kutokana na majeraha mbalimbali.

  Kwa mujibu wa televisheni ya Philippines kati ya watu milioni 7 na 10 walikusanyika kwenye mitaa ya Manila ili kupata nafasi ya kuliona na kuligusa sanamu la Yesu Mweusi ambalo linaaminika lina miujiza mingi.

  Baadhi ya waumini walisema kuwa matatizo yao na magonjwa waliyokuwa nayo yaliondoka baada ya kuligusa sanamu hilo.

  Sanamu hilo linalojulikana kama "Black Nazarene" kila mwaka hupitishwa mitaani ambapo maelfu ya watu hujipanga kulishuhudia likipita, wengine wakisali na wengine wakitafuta nafasi ya angalau kuligusa.

  Wengine walikusanyika mitaani mbele ya luninga kubwa kushudia tukio hilo ambapo misa maalumu zilifanyika.

  Kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu, watu 708 walipatiwa matibabu kutokana na majeraha mbalimbali kutokana na kukanyagana na wengine kushindwa kupumua vizuri au presha kupanda.

  Tamasha hili limekuwa likifanyika januari 9 kila mwaka kwa miaka zaidi ya 100 tangu sanamu hilo lilipoingizwa nchini Philippines mwaka 1607.

  Sanamu la Yesu mweusi lilitengenezwa nchini Mexico likiwa halina tofauti yoyote na masanamu mengine ya Yesu.

  Wakati likisafirishwa, liliungua na moto ndani ya boti ambayo ilitumika kulisafirisha na ndipo likageuka kuwa na rangi nyeusi.

  Sanamu hilo lilihafidhiwa katika kanisa moja nchini Philippines lakini imeelezwa kuwa limeweza kunusurika matukio mawili makubwa ya moto, matetemeko mawili makubwa ya ardhi na mabomu ya Wajapan mjini Manila wakati wa vita vya pili vya dunia mwaka 1945.

  Watu wengi wanaamini kuwa kunusurika kwa sanamu hilo katika matukio hayo makubwa ni miongoni mwa ishara za nguvu za miujiza za sanamu hilo.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...