Sanamu la Farao wa Misri Linalofanana na Michael Jackson Lawa Gumzo Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sanamu la Farao wa Misri Linalofanana na Michael Jackson Lawa Gumzo Marekani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Sanamu la Farao lilichongwa miaka 3,000 iliyopita ambalo linafanana sana na Michael Jackson Saturday, August 08, 2009 5:21 AM
  Sanamu la kale la mafarao wa Misri ambalo lilichongwa miaka 3,000 iliyopita limekuwa kivutio kikubwa sana nchini Marekani kutokana na jinsi linavyofanana kwa asilimia kubwa sana na mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson.
  Je Michael Jackson alikuwa akijaribu kuwa "Farao wa muziki wa Pop?" badala ya "Mfalme wa Muziki wa Pop".

  Maonyesho ya masanamu ya Mafarao wa Misri yanayoendelea nchini Marekani kwenye ukumbi wa makumbusho wa Field Museum, Chicago, kwa zaidi ya miaka 20 sasa, yamekuwa gumzo ghafla baada ya kugundulika kuwa kuna sanamu la farao linalofanana kwa asilimia kubwa na Michael Jackson.

  Mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kwenye jumba hilo la makumbusho kujionea sanamu hilo linalofanana na Michael Jackson.

  Sanamu hilo linaonyesha kipande cha kuanzia kifuani kwenda juu cha mmoja wa mafarao.

  Sanamu hilo lililotengenezwa miaka 3,000 iliyopita linafanana kwa asilimia kubwa sana na mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson ambaye alifariki juni 25 mwaka huu.

  Sanamu hilo ambalo linawakilisha sura ya mwanamke mmoja ambaye hajulikani alikuwa ni nani katika mafarao, liliingizwa kwenye maonyesho katika makumbusho hayo tangia mwaka 1988.

  Sanamu hilo lilichongwa kati ya mwaka 1550 BC na mwaka 1050 BC.

  Sanamu hilo linashabihiana kwa asilimia kubwa na sura ya Michael Jackson baada ya kufanyiwa operesheni za marekebisho ya sura yake.

  Sanamu hilo lina pua inayoshabihiana na ya Michael Jackson na lina macho ya duara kama ya Michael Jackson.

  Na kama uvumi uliozagaa kuhusiana na pua ya Michael Jackson kipande chake kunyofoka, sanamu hilo pia kipande cha pua yake kimenyofoka.

  Meneja wa jumba hilo la makumbusho, Jim Phillips alisema kuwa wafanyakazi wa jumba hilo la makumbusho wamekuwa wakisumbuliwa na maswali ya mashabiki wa Michael Jackson ambao wamekuwa wakimiminika kwenye jumba hilo tangia gazeti moja la Marekani liliposhtukia kufanana kwa sanamu hilo na Michael Jackson na kuirusha habari hiyo gazetini hivi karibuni.

  "Kuna watu wamekuwa wanakuja hapa na kutuuliza "Yuko wapi Michael Jackson?" na huwa tunawaambia Michael Jackson hapa hayupo, lakini kuna sanamu linalofanana sana naye" alisema Phillips akiongea na shirika la habari la AFP.

  Phillips alisema kuwa ingawa kuna utata kuwa huenda Michael Jackson alivutiwa na sura ya sanamu hilo na kujaribu kujibadilisha kufanana nalo, lakini ukweli ni kwamba Michael Jackson hakuwahi kwenda kwenye jumba hilo la makumbusho.

  "Kwa jinsi Michael Jackson anavyofanana na sanamu hili hakuna mtu anayeweza kukanusha " alisema Phillips.

  Michael Jackson alifariki juni 25 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 50 kutokana na shambulio la moyo.

  Ingawa mashabiki wake walishapata fursa ya kuuaga mwili wake tangia mwanzoni mwa mwezi uliopita, hadi leo mwili wake bado haujazikwa.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2759934&&Cat=2
   
Loading...