Sanaa Ni ufundi wa kuwasilisha mawazo ya mtunzi husika

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Kiswahili zamani kidogo ila Sijasahau maana ya Sanaa Ikiwa na maana ya kuwasilisha mawazo ya mtunzi husika.

Ikiwa na Vipengele vyake kama Ususi,muziki,Ufinyanzi,Uchongaji na kadhalika.Ukiwa Msusi,Mwanamziki,Mfinyanzi,mchongaji uwe wa Vinyago wewe unawakilisha Kazi za Sanaa unahaki ya kuitwa Msanaa/Msanii.

Ukija kazi za Sanaa ni Kuelimisha,Kuburudisha,kufurahisha, ni Chanzo Cha Ajira Kwa Wasanaa na pia Kufikisha Ujumbe Sahihi kwa wakati Sahihi.

Kila Nchi Inachombo kinachosimamia Kazi za Sanaa Kwa Wanasanaa/Wasanii wake ikiwa ni Pamoja na kuhakikisha Wasanaa/Wasanii wanakuwa na uhuru wa kuwasilisha kazi zao za Kisanii bila kuvunja Sheria Wala taratibu za Nchi.

Nchi Mwetu kuna Chombo Kinaitwa Basata(Baraza la Sanaa Tanzania),Chombo hiki ndiyo chenye Mamlaka ya kuhakikisha Sheria na Taratibu zote za Sanaa zinafuatwa hasa Tamaduni zetu za Kitanzania.

Niwapongeze kwa Kusimamia Sheria na Taratibu zao vizuri Tumesikia Wasanii wengi Wakifungiwa Kwa kuimba Nyimbo zilizo kinyume na Maadili ya Mtanzania.

USHAURI KWa BASATA...Ninaimani Wanawataalamu Mbalimbali Ni Bora Wakawa Wanasikiliza Nyimbo zote zinazotoka kabla ya kwenda Kwenye Vituo vya Radio ili Kufanya Marekebisho na Msanii husika Au hata kama ni kuupiga Stop basi waupige Stop kabla hujatoka.

Unakuta Wimbo ushatoka unazaidi ya wiki Tayari kila mtu keshausikiliza wao ndo wanakuja kuufungia.

Kingine..Wanaweza pia kuwa na Miongozo yao kwamba Msanii aimbe nini Labda kuhusu Magonjwa,Kilimo,Kupongeza jambo lolote zuri lile...nk.

Kuna wimbo ulitungwa Sijui Mwaka gani "UNASEMA MAKAO MAKUU YA NCHI SASA YAMEKUA DODOMA" na kweli leo yametimia kutaka kujua zaidi Nasikia Kuanzia Miaka ya Zamani huko Wafanyakazi walikua wanakatwa Pesa kwa Ajili ya Kuchangia Makao Makuu na kuiwezesha Serikali kuhamia Dodoma.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom