Samweli Sitta, fanya mdahalo na wafanyakazi wa TAZARA kwanza

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Hivi karibuni waziri wa uchukuzi, Bw, Samuel Sitta ameomba mjadala/mdahalo na mgombea wa CHADEMA Bw. Edward Ngoyai Lowassa kuhusu swala la Richimond.

Mimi namuomba Bw. Samuel Sitta kabla ya kufanya mdahalo wa Richmond na Bw. Lowassa, ningeomba aje hapa TAZARA tujadili kutopewa mishahara kwa muda wa miezi sita, kwa watumishi zaidi ya 200000,wa Taasisi anayoisimimamia , kwa upande wangu naona kama utu na ubinadamu unakosekana inakuwaje Waziri unashindwa kufuatilia mishahara na stahiki zetu, halafu ukafuatilia suala la RICHMOND kama kipaumbele chako.

Hatukuzuii kufanya hilo lakini hilo si kipaumbele kwako kwani katika jiji hili la Dar Es Salaam na maeneo mengine tunaishije na hatuoni kauli kwako ya kufuatilia zaidi ya RICHMOND.

Kama swala la Richmond ni muhimu katika kampeni ili kupunguza kura za mahasimu wenu, huoni kuwa Swala la mishahara kwa wafanyakazi wa TAZARA ni muhimu zaidi kwa upande wako hasa ukizingatia kura wafanyakazi za ya 200000 wa TAZARA ni nyingi sana ? Ukiachilia mbali kura za wake au waume zao na jamaa zao ?

Je, haikuwa busara kwako kulishughulikia hili ili uokoe kura za wafanyakazi hao kwenda kwa mahasimu wenu?

Basi nakushauri kabla ya kuomba mdahalo na mgombea wa UKAWA basi wafanyakazi wanaomba ufanyike mdahalo nawe.
 
Sitta kama sijakosea ni mwanasheria aliehitimu kutoka Chuo kikuu huria cha Tanzania, Ni lini mtuhumiwa akatakiwa kufanya mdahalo? Mahakama ni za kazi gani? Hawa watu wamefika mahali wanatuona waTanzania ni mazuzu ee? aliezima mjadala wa richmond ni yeye kipindi akiwa spika wa bunge leo anasema anataka mdahalo? Hawa jamaa wanatuona sisi hamnazo!
 
naona mnaanza kumkingia kifua fisad wenu coz mnajua hawez chomoka ha ha haaa endeleen mnaweza mnusuru!
 
Ni kweli na haki! mdahalo na ENL kuhusu Richmond hauwezekani; kama wanasema ile ni jinai kama Mwakyembe anavyouita; Lowassa keshasema mwenye ushahidi sisisi; aende mahakamani! period.
Sitta ashughulikie maswala ya wizara anayoiongoza asitupotezee muda hapa na ngonjera za mdahalo; Richmond ni mahakamani tu! nendeni
 
mimi namtaka aeleze kwanini wafanyakazi wa TAZARA hawajalipwa miezi sita
 
Back
Top Bottom