Samwel Sitta: Sina muda wa kulumbana na UKAWA

Lipumba alipowatapeli kuwatoa Bungeni aliwalipa Tsh ngapi? Tunampongeza sana Mh. Mbowe kwa Uzalendo wake wa kuhakikisha Sitta anakuwa Mwenyekiti wa Bunge kabla hajaingizwa Mkenge na yule Professa Mseja.

SALOME SICHWALE acha kuongelea ndoa za watu, unaweza nitajia mke au mtoto wa Kinana?
 
Last edited by a moderator:
Jamani hao ndo maelfu ya wananchi? mi ninavyoona ni watu 20 wa ccm walioalikwa kuja kumpa ndumikuwili kampani. Jamaa anatia huruma ata suru yake yenyewe hapo inajieleza. IF EYES CAN NOT SEE MIND IS BLIND
 
MwanaDiwani, post #79 :

Huko nyuma nilishakueleza Kwamba - tume ya jaji warioba ilipendekeza rais mmoja wa muungano na viongozi Wengine wawili wa kuongoza pande Mbili za muungano bila ya kujalisha Viongozi hawa watapewa majina gani ya kiutawala. Pahala ambapo palitarajiwa kuwa suala la title za viongozi wa nchi washirika lingejadiliwa lakini bila ya kuathiri Roho ya rasimu ya wananchi (serikali Tatu) ilikuuwa ni ndani ya bunge maalum la katiba. Lakini tofauti na tume ya warioba, na katiba inayopendekezwa sasa imebariki gharama kubwa zaidi kwa wananchi, hasa watanganyika. Tofauti na rasimu ya tume ya jaji warioba, rasimu ya mafichoni ya CCM Sasa imeweka wazi Kwamba Jamhuri ya muungano wa Tanzania itakuwa na viongozi SABA wenye hadhi ya URAIS. Tukianza na Upande wa Zanzibar, wao watakuwa na viongozi WATANO wenye hadhi ya urais, Kama ifuatavyo:

1. Rais wa Zanzibar (anayepigiwa kura na wazanzibari tu lakini Ana Nguvu hadi kwa wananchi ambao Hawakushirikishwa kumchagua - watanganyika).

2. Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar ambae ni msaidizi wa rais wa Zanzibar, hivyo kuwa na mamlaka ya kukaimu mamlaka juu ya watanganyika.

3. Makamu wa pili wa rais Zanzibar (mamlaka sawa na makamu wa kwanza wa rais Zanzibar).

4. Makamu wa kwanza wa rais wa JMT (mgombea mwenza kutoka Zanzibar (Huyu yupo kuwakilisha maslahi ya wazanzibari, sio watanganyika).

5. Makamu wa pili wa rais wa JMT (ambae pia Ana kofia nyingine ya urais wa Zanzibar).

Hapa tusisahau Kwamba katiba ya Zanzibar (2010) imepora mamlaka ya katiba ya JMT.

Kwa Upande wa Tanganyika, wao watakuwa na viongozi WAWILi tu kati ya marais Saba wanaoridhiwa na katiba inayopendekezwa:

1. Rais wa JMT - Huyu tumeshaona jinsi gani katiba ya Zanzibar (2010) ilivyompora mamlaka. Kwa maana nyingine, rais wa JMT chini ya katiba inayopendekezwa atakuwa ni rais wa Muungano kinadharia tu, huku akiwa sio lolote kivitendo. Kwa maana nyngine Rahisi, rais wa muungano will become "a toothless dog" Katika uongozi wake wa jamhuri ya "muungano". Ukweli huu utazidi kujitokeza siku sio nyingi kwani Zanzibar hawawezi kurudi nyuma na kubadili katiba Yao kwa manufaa ya Tanganyika iliyovaa koti la muungano.

2. Rais wa pili kutoka wa Tanganyika atakuwa ni waziri mkuu wa JMT ambae vituko vya katiba inayopendekezwa vimempa wadhifa wa "makamu wa TATU" wa rais! Hata hivi tunavyozungumza, waziri mkuu wa JMT Hana mamlaka Zanzibar, mamlaka yake ni ndani ya Tanganyika tu, ukipenda, call it "Tanzania Bara". Isitoshe, mipaka ya Tanzania bara ni Ile Ile ya Tanganyika.

Hii inafanya uwepo wa viongozi SABA wenye hadhi ya urais Katika mazingira ya katiba inayopendekezwa - Zanzibar ikitoa watano, Tanganyika ikitoa wawili, huku marais wa upande wa Zanzibar wakiwa Ndio wenye mamlaka makubwa zaidi kiutawala (rejea mgongano wa kikatiba) lakini pia kirasilimali (kwani chochote cha Tanganyika ni cha muungano kwa vile haina serikali yake). Hali hii inafanya cha Zanzibar Kiwe cha Kwao, na cha Tanganyika Kiwe cha wote - watanzania. Licha ya soko moto kote hili, bado Gharama zote za kuhudumia marais hawa Saba wakiwa madarakani na wakienda kustaafu zitakuwa ni za mtanganyika. Mwezi Aprili mwaka huu, Hamad rashid alipinga sana rasimu ya tume Kwamba itapelekea uwepo wa marais watatu ambao watakuwa ni mzigo kwa walipa kodi. Huu pia ulikuwa ni upande wenu a hoja ndani ya CCM. Hamad Rashid akatoboa Siri Kwamba namnukuu, "Leo rais akisafiri, anatumia sio chini ya shillingi milioni 500 (Mia Tano), Mara nyingine hadi shillingi bilioni moja. Hizo ni akiwa tu madarakani." Akaendelea kusema Kwamba: " viongozi hao wakistaafu zaidi ya watatu kwa Wakati mmoja, utakuwa ni mzigo mkubwa wanabebeshwa wananchi".

Mbali ya haya, taarifa zilizopo ni Kwamba mshahara wa waziri mkuu kwa mwezi ni shillingi milioni 25, hapo hajaongezewa hadhi ya urais, je akiongezewa utakuwa ni shillingi Ngapi zaidi? Na jumla ya mishahara na posho kwa viongozi hawa itakuwa ni kiasi gani kwa mwezi? Kumbuka hawalipi kodi, na Wala hawalipii wakata nyasi, na hata miswaki Yao inabynuliwa na fedha za walipa kodi, nje ya posho na mishahara Yao.


Kama alivyojadili Nguruvi3 elsewhere, muungano umefikia Katika hatua ya hatari kuliko kipindi chochote Kile. Kwa mfano Katika suala jamhuri ya muungano, miaka 50 baadae, JMT imekuwa ni nchi Mbili Zenye serikali Mbili, na kofia Saba za urais,lakini bado Mmejaa matongo tongo kuona athari ya suala hili kiutawala, let alone maumivu kwa walipa kodi wa Tanganyika.

Chini ya Katiba inayopendekezwa, CCM inapendekeza kwamba – Rais wa Zanzibar afanywe kuwa Makamu wa Rais wa Muungano bila ya kujalisha Rais wa Muungano anatokea upande upi wa Muungano. Kwa kufanya hivyo, CCM inadai kwamba – hali hii itamwongezea Rais wa Zanzibar - “madaraka na hadhi” ndani ya serikali ya Muungano na pia nje ya nchi. Huku ni kupandikiza mbegu ya machafuko na hatimaye kuvunjika kwa muungano kwa sababu:

Mkataba wa Muungano (1964) uliweka utaratibu ambao – Rais wa Muungano wa NCHI Moja, alikuwa na wasaidi wake wakuu wawili – Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar (Marehemu Karume), na Makamu wa Pili wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika (Marehemu Kawawa).

LAKINI chini ya katiba inayopendekezwa, CCM haisemi iwapo Rais ni MMOJA wa nchi MOJA, badala yake Inasema tu kutakuwa na rais wa JMT, na hao Wengine Sita.

Katiba inayopendekezwa haisemi ni kiongozi gani ndiye atakayesimamia Mawaziri watakaokuwa wanasimamia mambo ya Tanzania Bara katika mfumo huu wa serikali mbili “ulioboreshwa”. Katika mikakati yake ya kuuza kwa umma katiba inayopendekezwa, CCM haina Maelezo juu ya ufafanuzi wa masuala muhimu (kiutekelezaji), kwa mfano, - katika mazingira ya Zanzibar kuwa ni “nchi” kamili, yenye “mamlaka” kamili, katiba, amiri jeshi mkuu, Wimbo wa taifa, ikitokea kwamba Rais wa Muungano anatokea upande wa pili wa muungano (Zanzibar), JE:

· Rais huyu kutoka nchi jirani ya “Zanzibar” atasimamia masuala yasiyo ya muungano - ya upande unaoitwa “Tanzania Bara”, ndani ya Jamhuri ya Muungano, kwa mamlaka yepi?

· Iwapo Rais wa Muungano atatokea panapoitwa “Tanzania Bara”, Rais huyu wa Muungano atakuwa na mamlaka yepi ya kusimamia mambo ya “Tanzania Bara” wakati yeye atakuwa amechaguliwa na wananchi wa pande zote mbili za muungano - Tanganyika na Zanzibar?

· Zipo wapi ‘pande mbili’ za muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika?

Katika haya, CCM haina uwezo wa kufafanua Hali ambayo itazidi kuudhoofisha muungano. Kwa vyovyote vile, Katiba inayopendekezwa haitaboresha muungano bali itajenga mazingira ya kuvunja muungano. Tuendelee kufafanua hili:

Kwa mfano, iwapo Rais wa Muungano atatokea upande wa nchi jirani ya “Zanzibar”, ambaye kwa Mujibu wa katiba inayopendekezwa, Rais wa Zanzibar pia atakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM inapendekeza kuwa rais wa nchi Jirani ya Zanzibar moja kwa moja awe ni makamu wa rais wa muungano (Tanganyika) hata Kama hakuna mtanganyika hata mmoja aliyempigia kura. Kwa maana nyingine, rais wa Zanzibar pia atakuwa ni rais wa watanganyika kwa njia ya uteuzi. Hiki ni kituko cha mwaka - watanganyika kuwa na marais wawili, mmoja waliyempigia kura, mwingine aliyepigiwa kura nchi Jirani (Zanzibar) kisha kuteuliwa kuwa rais wao watanganyika, Tena akiwa na katiba (ya Zanzibar)ambayo Ipo juu kimamlaka kuliko Ile ya watanganyika/muungano.

Mbali ya athari hizi, Ipo nyingine kubwa. kwa mfano, Kitendo cha rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa muungano bila kujalisha Rais wa Muungano atatokea upande upi wa Muungano kitatupeleka Katika Hali ifuatayo:

• Siku moja, Rais wa Muungano na Makamu Wa Rais Wa Muungano, wote watakuwa wametokea nchi jirani ya “Zanzibar”. Kwa maana hii, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, CCM inajenga mazingira ambayo Zanzibar hawataweza tena kutoa Rais wa Muungano. Hii ni kwa sababu:

Hali hii itaamsha watanganyika kwani kwa maana ya Kwamba - Kama tulivyoona, chini ya rasimu inayopendekezwa na CCM, Rais wa Zanzibar “automatically”, atakuwa pia ni Makamu wa Rais wa Muungano. Sasa ikitokea Siku CCM ikasimamisha mgombea Urais wa Muungano kutokea nchi jirani ya “Zanzibar”, nchi ambayo pia automatically itatoa makamu wa Rais wa Muungano, chini ya mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, wapiga kura kutoka upande wa inayoitwa “Tanzania Bara”, upande ambao una wapiga kura zaidi ya 90% ya wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano, HAKIKA, wengi ya wapiga kura hawa kutoka “Tanzania Bara”, hawatakubali kumchagua mgombea wa urais (CCM) kutokea nchi ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake pia anatokea huko huko “nchini” Zanzibar. Kwa maana nyingine, wananchi wa tangangika siku moja watakataa mgombea wa aina hii atakayependekezwa na CCM.

Je athari yake ni nini?

Ni kwamba – chini ya katiba inayopendekezwa na CCM, ni muhimu sasa waZanzibari waanze kujiandaa kisaokolojia Kwamba watanganyika Kamwe hawatomchagua kwenye Sanduku la kura mgombea urais mzanzibari kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanganyika watakuwa wamefanya uamuzi sahihi lakini Kitachofuatia kwa upande wa Zanzibar ni Kwamba wazanzibari wataanza kulalamika kwamba wanabaguliwa, wanaonewa, wananyimwa haki ndani ya Jamhuri ya muungano, kwahiyo waachwe “Wapumue”. And interestingly enough, watakaongoza katika kutoa hoja hizi ni wale wale wazanzibari ambao Islaml Jusa alisema kwamba walipofika Dodoma “Waliufyata”. Ni wale wale ambao leo wanapinga kwamba wao sio “wasaka tonge”. Katika kundi hili, hatutashangaa kuja kuona viongozi kama Balozi Seif Iddi, Mohamed Seif Khatib, nahodha, kificho,Hamad Rashid Mohamed, na wengine wakija kugeuka na kusema Kwamba Tanganyika inafanya Zanzibar kuwa koloni. Baadae tutaona jinsi gani ruksa kwa Zanzibar kukopa, kuwa na uhusiano wa kimataifa n.k bado hayatamaliza Dhana ya ukoloni.Hakuna mamlaka kamili kwa Zanzibar kwa Jambo lolote bila ya uwepo wa Tanganyika.

• Je kwa upande wa viongozi wa CCM bara, watakuja Lamba matapishi yao?

Kwa upande wa inayoitwa “Tanzania Bara”, iwapo Mgombea Urais wa Muungano atatokea nchi jirani ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake “automatically” pia atatokea Zanzibar, watakaoongoza katika kupinga hali hii haitakuwa watu wengine bali wale wale makada wa CCM ambao ndani ya bunge la katiba walijiita kwa majigambo Kwamba wao Ndio wenye “Maoni ya Walio Wengi”, ambao wamepitisha katiba inayopendekezwa kwa vigele gele na
Vifijo. Fitina zilizomkumba Dr. Salim Ahmed Salim alipokuwa anawania urais hazitafua dafu kwa fitina zitakazojitokeza katika mazingira tunayojadili hapa. Wana CCM ambao watakuwa katika makundi ya kutafuta Rais wa Muungano wataendesha kampeni kubwa kupinga uongozi wa Muungano kwenda kwa “nchi jirani katika kofia zote mbili za juu – Rais wa Muungano na Makamu wa Rais wa Muungano.

Kuna haja ya wazanzibari na watanganyika kuungana kuzuia hatari iliyopo Mbeleni. Ujumbe muhimu kwa wazanzibari ni Kwamba wanachoambiwa na CCM ndani ya rasimu inayopendekezwa ni kwamba:

• "Kuanzia sasa, wazanzibari wajiandae tu kisaikolojia kuwa ni “wasindikizaji” tu wa Uongozi" katika Jamhuri ya Muungano."

Pia CCM nayo ijiandae kutupiwa lawama na malalamiko mapya juu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar. Mbegu ya kuvunjika kwa muungano sio tu imeshapandwa, Bali pia imeanza kuchepuka.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Sitta ameleta mikosi Urambo. Baada ya mkutano huo ambao alikusanya watu kutoka pande zote za Urambo kwa malori, usiku wake soko limeteketea huku akishuhudia. Sitta ni mkosi kwa wana-Urambo
 
naona kavaa sendo na ameanza kuchechemea tayari sala za wananchi zimefika tutaona mengi sana mpaka mwaka ujao halafu mnakaa na kumsingizia mzee wetu Lowasa ni mgonjwa wakati yeye ndiye tunamtegemea kuwa raisi wa nchi yetu mwaka ujao.Mungu amlinde Lowasa
 
anagalia hali ya wananchi wake dah inasikitisha kweli hawajui hata jua linatokea wapi na kuzama wapi
 
anagalia hali ya wananchi wake dah inasikitisha kweli hawajui hata jua linatokea wapi na kuzama wapi

Ndugu,
Umetumia kipimio gani kinachotambulika kimataifa kuwafahamu hao wananchi wote kama hawafahamu mawio na machweo.

Inawezekana wewe ndiyo UKAWA una matatizo!
 
Hoja yangu ilikuwa hii:
quote_icon.png
By Lukansola

Kuhusu ubora wa katiba naunga mkono 100/100, maana nasikia kuna mpaka marehemu waliipigia kura ya ndio!


Comment yako:

Medula Oblangata yako ilifungwa Sikioni? Kichwa ni kwa ajili ya kufikiri sio kusokotea Dred.

Post ya mwenyewe unaichakachua!... mazoea mabaya
 
binafsi nilikuwa simkubali kabisa mh. Samwel sitta hasa jinsi alivoendesha bunge la tissa kwa kulifanya jukwaa la kusakama wapinzani wake wa kisiasa lakini baada ya kupumzishwa na kuona jinsi nguli wa siasa, mwanamke wa karne anne makinda akiongoza bunge kwa kanuni na sheria bila ya ushabiki nae kajifunza na hatimae kafanikiwa kutuletea katiba pendekezwa bora kabisa kusini mwa jangwa la sahara kama alivoahidi. Hongera sitta hongera comrade andrew chenge
..koooonyoooo koya
 
mbunge wa jimbo la urambo mashariki samwel sitta, amepokelewa kwa kishindo jimboni kwake urambo na kuhutubia katika viwanja vya mwananchi square.

Sitta akihutubia wapigakura wake alielezea jinsi mchakato wa bunge maalum la katiba ulivyokwenda hadi alipokabidhi katiba inayopendekezwa kwa rais dkt.jakaya kikwete.

Katika hotuba yake hiyo, sitta ambaye alikuwa mwenyekiti wa bunge hilo, alielezea jinsi katiba ilivyotoa haki za wakulima, wafugaji, haki za watoto, baraza la vijana la taifa, hamsini kwa hamsini kwa wanawake katika nafasi za uongozi na mengineyo.

Aidha, amewataka wana urambo na watanzania kuipitia katiba inayopendekezwa kwa kina na ufasaha kwani imekidhi vigezo na matakwa ya wananchi yenye maslahi mapana ya vizazi kwa vizazi.
===================


10418983_802870006443650_17526327949523614_n.jpg

samwel sitta wakati wa shughuri ya kumsimika.
10704076_802869316443719_2623104900641162220_n.jpg

mhe. Samwel sitta akihutubia wananchi wake katika mkutano wa kumpongeza kwa kazi ngumu ya kuliongoza bunge maalum
10710696_802870223110295_8112502459661380857_n.jpg

10365728_802870863110231_469350024327703825_n.jpg
mbona hawaambii wapitie na kuzisoma rasimu zote yake yeye na ya maoni ya wananchi iliyowakilishwa na tume ya jaji warioba?
 
SUALA JE ZNZ katiba yake inaweza kura za ndio kukidhi haja ya matakwa ya sharia yaani 2/3 za ndio ili ikubarike?

Bara naona hakuna mushkirah ila Znz mmh!

Ndg yangu kila kitu kimeshamalizwa Dodoma, Tanganyika bado inaitaka zanzibar kama koloni lake,hivi kama wameweza kuchakachua kura za wabunge toka zanzibar, hazikutosha lakini wamezitosheleza, unadhani watashindwa kuchakachua kura ya maoni? Sijui wenzetu Zanzibar mtatumia mbinu gani
 
Kama ni huo Uchifu mbona hata E. Lowasa alishasimikwa kama Mtemi/Chifu wa Urambo?Hii ni propaganda ya kijinga
 
SUALA JE ZNZ katiba yake inaweza kura za ndio kukidhi haja ya matakwa ya sharia yaani 2/3 za ndio ili ikubarike?

Bara naona hakuna mushkirah ila Znz mmh!

Ndg yangu kila kitu kimeshamalizwa Dodoma, Tanganyika bado inaitaka zanzibar kama koloni lake,hivi kama wameweza kuchakachua kura za wabunge toka zanzibar, hazikutosha lakini wamezitosheleza, unadhani watashindwa kuchakachua kura ya maoni? Sijui wenzetu Zanzibar mtatumia mbinu gani
Noboko,

Kwa upande wa Znz kuna mambo mawili muhimu yatakayotakiwa kufuatwa ili katiba hiyo ya Sitta iweze kutumika.

1. Hatua ya kura ya maoni ya wananchi.
2. Mabadiliko ya katiba ya Znz ili yaendane na katiba ya JMTz. hapa ndipo pazito zaidi kwani inahusisha wawakilishi tu.

Ok all in all kwa upande wa Znz itakuwa mbombo ngafu.




 
Back
Top Bottom