Samwel Sitta asisitiza: Dkt. Mwakyembe kalishwa sumu, asema kuna polisi majambazi

Kwa jinsi hatutakaa tuikomboe nchi yetu kutoka kwenye udhalimu unapotamka mafisadi unagenelize na wataendelea kufanya huo ufisadi. Inatakiwa itamkwe wazi pamoja na majina yao kama ni Lowasa atamkwe kwa jina lake kama ni Chenge atamkwe kwa jina.
Uoga wa nini watajwe kwa majina watanzania wawajue
yaap nimekupata, uwoga unatucost sana watanzania
 
Sam 6 USITUBABAISHE hapa! Kama UNAWAjUA si uwataje? Naona una ushahidi wa kile usemacho. Kwa nini usikiseme wazi? Mwandishi mmoja alishaandika: TUPENI HABARI ZA UKWELI KUHUSU AFYA YA MWAKYEAMA MNYAMAZE MILELE"! Mie nakubaliana naye 100%. Kusemana kwa kufichana haisaidii. Ndo sababu kama Spika, 6 alijua wahusika wa Ricmond LAKINI HAKUWATAJA! Ushujaa wa kupingana na ufisadi uko wapi hapa?
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameendelea kusisitiza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu.

Kauli yake imekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini kueleza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri huyo hausababishwi na kula chakula chenye sumu; kauli iliyomuibua Dk. Mwakyembe na kudai Jeshi hilo halikumtendea haki akisema si lazima unyeshwe sumu ili ikudhuru.

Sitta amesema, hoja ya Jeshi la Polisi kueleza kuwa suala hilo linahitaji ushahidi ni kuupotosha umma ili usielewe nini kinachomsumbua Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya.

Akizungumza katika uzinduzi wa Asasi ya Kiraia ya Vijana wa Kanisa Katoliki mkoani Tabora (VITAL) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Askofu Mkuu Marco Mihayo, Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo mkoani hapa, alisema yeye kama Waziri hawezi kusema uongo kuhusu jambo hilo.

Alisema Jeshi la Polisi limekuwa likipotosha umma kukanusha kwamba Dk. Mwakyembe hajalishwa sumu ingawa Naibu Waziri huyo ana ushahidi wa kutosha kuhusu jambo hilo.

“Mimi nitapigana hadi siku ya mwisho kutetea wanyonge na ninashangaa kuelezwa kwamba mimi nimeshitakiwa na Polisi kwamba nimepotosha umma kusema kwamba Dk. Mwakyembe amelishwa sumu. Na kwa taarifa yako Baba Askofu nimeelezwa jalada langu limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ili nishitakiwe,” alisema Sitta.

Alilishutumu Jeshi la Polisi kutokana na tabia ya kuhujumu watu na kusisitiza kuwa tabia hizo ni za kijambazi zinazoweza kuhatarisha hali ya usalama na maisha ya watu wanaozuliwa mashitaka kama hayo yanayomkabili.

Akizungumza ufisadi, alisema amekuwa mstari wa mbele kupinga suala hilo kwa nguvu zote na atahakikisha anapigana kufa au kupona kupambana na watu wanaojilimbikizia mali kwa kutumia madaraka yao.

Alisema jambo hilo halikubaliki na kwamba kwa sababu yupo hai, ataendelea kupambana nalo hadi hapo litakapoleta tija na hatimaye kuwawezesha wananchi wanufaike na rasilimali za nchi yao.

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, lilieleza kuwa kwa taarifa ilizopewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hospitali ya Apollo nchini India, ni kwamba ugonjwa wa Dk. Mwakyembe haukutokana na kulishwa kitu chenye sumu.


Source:
Habari leo
Kweli Mkuu hao si wakucheka nao, badala ya kutafuta mtu aliyempa sumu Mwakyembe wao wanatafuta kuzima ukweli, hiyo ndiyo kazi tuliyowatuma hao Polisi????????
 
Hivi hawa mafisadi wanaosemwa kila siku hawana majina? Maana kila siku tunamsikia mafisadi wanaimaliza nchi ni akina nani hao. Kufichaficha kwao kutawafanya nao waonekane kuwa nao ni mafisadi.

.
Ref. Mkutano wa Dr Slaa Mwembe yanga woote wametajwa kwa majina.
.
 
Penye moshi kuna moto ndani.Hakuna kuaminiana ndani ya serikali hi ni zaidi ya hatari.Mungu okoa taifa lako Tanzania
Wacha ndani ya serikali hata ndani ya chama ndio usiseme, kuna hatari mbele yetu Watanzania!!!!!! Maghamba hayavuliki ni taabu tupu!!!!!

 
Hivi hawa mafisadi wanaosemwa kila siku hawana majina? Maana kila siku tunamsikia mafisadi wanaimaliza nchi ni akina nani hao. Kufichaficha kwao kutawafanya nao waonekane kuwa nao ni mafisadi.

Unataka list ngapi za mafisadi mbona wengi walitangazwa na Slaa pale mwembe Yanga? Tafuta uzi humu wenye majina yao utawafahamu.
 
Hata mimi naungana na Mh. Sitta. Swala la Mwakyembe linafanana kabisa na la yule mpelelezi wa KGB aliyeasi (Livinyenko) na kupewa sumu akiwa uingereza,alinyonyoka nywele zote mwilini na hatimae kufariki.
 
Alafu kumbe hata uchimbaji wa uranium watu washavuta zao,maana nasikia ni madini hatari sana na hayapaswi kuchimbwa kiholela,usa wanayo lakini wanaogopa kuyachimba ili kuwanusuru wananchi wao,vp sisi waswahili tumekubali kirahisi namna hii????????????,

Mkuu taratibu bana,,"waswahili ni JK na ccm/serikali yake" waliokubali mikataba hiyo. mie akaaaaa! sio mswahili
 
Kinachonishtua mimi ni hizi dalili za organized crimes zinazojitokeza! Halafu, watazamaji tukazoea tu!

Petu Hapa, usishtuke, hii siyo 'organised crime' ila sema 'it is the piper who calls the tune' we have a functioning presidential institution, but it's too lame to even point an accusing finger to the thief. Anaishia kuwafunga anaohisi wametembea na mahawara zake.
 
Back
Top Bottom