Samwel Sitta asisitiza: Dkt. Mwakyembe kalishwa sumu, asema kuna polisi majambazi

wewe mtanzania au mkenya? Huwajui mafisadi

Kwa jinsi hatutakaa tuikomboe nchi yetu kutoka kwenye udhalimu unapotamka mafisadi unagenelize na wataendelea kufanya huo ufisadi. Inatakiwa itamkwe wazi pamoja na majina yao kama ni Lowasa atamkwe kwa jina lake kama ni Chenge atamkwe kwa jina.
Uoga wa nini watajwe kwa majina watanzania wawajue
 
Hao Police wanaosema hakulishwa Sumu, Sasa waseme anaumwa nini Mwakiembe, Itakuwa wanajua nini kilichomsibu na wao wanahusika??
DON'T PROTECT WHILE YOU DO NOT HAVE PROTECTION
 
Kinachonishtua mimi ni hizi dalili za organized crimes zinazojitokeza! Halafu, watazamaji tukazoea tu!
 
Alafu kumbe hata uchimbaji wa uranium watu washavuta zao,maana nasikia ni madini hatari sana na hayapaswi kuchimbwa kiholela,usa wanayo lakini wanaogopa kuyachimba ili kuwanusuru wananchi wao,vp sisi waswahili tumekubali kirahisi namna hii????????????,
 
Hii series ya conspirancy tz ndio ipo season 1 episod....... Ni tamu never miss it.
 
ukimnyoshea kidole mwenzako, wewe unajinyoshea vidole vinne. wakati sita na mwakyembe wanawanyoshea wenzao, wao wanajinyoshea vidole vingi zaidi, kwani nao ni wezi tu wa mda mrefu. Kama wao wenyewe wameshiriki wizi, unadhani watamtaja nani?

"....... mheshimiwa spika, mengine nimeamua nisiyaseme hapa, kwani nikisema kila kitu serikali itaanguka....." unakumbuka ni maneno ya nani?

kama aliwahifadhi wezi wasianguke, kwa nini yeye asiitwe mwizi? Na kwa nini spika asingemtaka aseme yorte kwani wametumia kodi za watatnzania kuwafichua wezi? si wanatakiwa kuja na ripoti kamili ya nani mwizi? kwa nini walificha?

hata wao ni wezi, tena nataman sumu ya mwakyembe ihamie kwa sita kama adhabu ya kutumia madaraka yake vibaya kushiriki kuficha ukweli wa tume ya mwakyembe
 
jeshi la polisi limekuwa ni jeshi la kuwalinda watu wachache wanaoharibu hii nchi,huku wakiwa wanacheza mchezo wa kupotosha umma,yan as if wanatugonganisha vichwa sisi kwa sisi wakati wao wanacheza madili na mafisadi
 
Hivi hawa mafisadi wanaosemwa kila siku hawana majina? Maana kila siku tunamsikia mafisadi wanaimaliza nchi ni akina nani hao. Kufichaficha kwao kutawafanya nao waonekane kuwa nao ni mafisadi.

.
Ref. Mkutano wa Dr Slaa Mwembe yanga woote wametajwa kwa majina.
.
 
KIKWETE na LOWASSA WANAMKONO KATIKA KUMPA SUMU MWAKYEMBE.. KwANI RICHMOND INAWAHUSU SANA HAO MAFISADI WAWILI
 
jeshi la polisi limekuwa ni jeshi la kuwalinda watu wachache wanaoharibu hii nchi,huku wakiwa wanacheza mchezo wa kupotosha umma,yan as if wanatugonganisha vichwa sisi kwa sisi wakati wao wanacheza madili na mafisadi

Kwani nani anawalipa police mishahara?
Kesi ya nyani unampelekea sokwe?
 
Mwenzao Satta wa Zambia alianzisha chama huwezi kupigana vita ukiwa humo na mafisadi huku ukiwa unfaidi viposho pamoja nao.....mnafiki tu. aondoke CCM! au ashiriki kwa namna yoyote ile kuia CCM maana ndiyo hasa nyumba ya mafisadi.
 
Hii sasa ni hatari wenye maghala ya silaha wanaanza kutuonyesha jeuri na kutuambia wazi kwamba hako pale kwa ajili yetu bali kwa ajili ya Mafisadi.Hii maana yake kwangu ni kwamba sasa Watanzania na Uhuru wao waliojitwalia mnamo miaka ya 1960 chini ya Nyerere haupo tena mikononi mwao bali nchi sasa imechukuliwa na Mafisadi wa nje na ndani.
Swali kwa Watanzania wenzangu tutafanyaje ili kurejesha uhuru wetu kama Taifa?.
 
Back
Top Bottom