Samwel Sitta asisitiza: Dr. Mwakyembe kalishwa sumu, asema kuna polisi majambazi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samwel Sitta asisitiza: Dr. Mwakyembe kalishwa sumu, asema kuna polisi majambazi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Feb 20, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameendelea kusisitiza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu.

  Kauli yake imekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini kueleza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri huyo hausababishwi na kula chakula chenye sumu; kauli iliyomuibua Dk. Mwakyembe na kudai Jeshi hilo halikumtendea haki akisema si lazima unyeshwe sumu ili ikudhuru.

  Sitta amesema, hoja ya Jeshi la Polisi kueleza kuwa suala hilo linahitaji ushahidi ni kuupotosha umma ili usielewe nini kinachomsumbua Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Asasi ya Kiraia ya Vijana wa Kanisa Katoliki mkoani Tabora (VITAL) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Askofu Mkuu Marco Mihayo, Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo mkoani hapa, alisema yeye kama Waziri hawezi kusema uongo kuhusu jambo hilo.

  Alisema Jeshi la Polisi limekuwa likipotosha umma kukanusha kwamba Dk. Mwakyembe hajalishwa sumu ingawa Naibu Waziri huyo ana ushahidi wa kutosha kuhusu jambo hilo.

  "Mimi nitapigana hadi siku ya mwisho kutetea wanyonge na ninashangaa kuelezwa kwamba mimi nimeshitakiwa na Polisi kwamba nimepotosha umma kusema kwamba Dk. Mwakyembe amelishwa sumu. Na kwa taarifa yako Baba Askofu nimeelezwa jalada langu limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ili nishitakiwe," alisema Sitta.

  Alilishutumu Jeshi la Polisi kutokana na tabia ya kuhujumu watu na kusisitiza kuwa tabia hizo ni za kijambazi zinazoweza kuhatarisha hali ya usalama na maisha ya watu wanaozuliwa mashitaka kama hayo yanayomkabili.

  Akizungumza ufisadi, alisema amekuwa mstari wa mbele kupinga suala hilo kwa nguvu zote na atahakikisha anapigana kufa au kupona kupambana na watu wanaojilimbikizia mali kwa kutumia madaraka yao.

  Alisema jambo hilo halikubaliki na kwamba kwa sababu yupo hai, ataendelea kupambana nalo hadi hapo litakapoleta tija na hatimaye kuwawezesha wananchi wanufaike na rasilimali za nchi yao.

  Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, lilieleza kuwa kwa taarifa ilizopewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hospitali ya Apollo nchini India, ni kwamba ugonjwa wa Dk. Mwakyembe haukutokana na kulishwa kitu chenye sumu.


  Source:
  Habari leo
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Sema...sema...baba!! Hawa si wa kuwachekea hata kidogo!! Majambazi wakubwa.
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa mafisadi wanaosemwa kila siku hawana majina? Maana kila siku tunamsikia mafisadi wanaimaliza nchi ni akina nani hao. Kufichaficha kwao kutawafanya nao waonekane kuwa nao ni mafisadi.
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mafumbo mafumbo yamezidi hebu semeni yote na mtuambie wenyenchi tufanyeje?!!!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nimependa habari kama hii kuandikwa na Habari Leo!
   
 6. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,929
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  Hili sakata mpaka kieleweke...Sita baba,twende kazi.
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda hii kwa kuwa sasa kwangu mimi naona aina ya pili ya Mzee Sitta kwa mara ya kwanza ilikuwa kawe jijini Dar es Salaam na ya pili ulingo wa nyumbani kwao pale Tabora.

  Ameanzisha aina nzuri ya machakato anapotumia nyumba ya Mungu kuwakumbusha wananchi kuhusu mapambano na ufisadi kwa kusema hadharani.

  Sasa natamani kuona upande wa pili nao usichangishe pesa huku tukia hatuoni hata press image yake tusikie nao wakikemea ufisadi ili kesho na kesho kutwa tujue mkweli ni nani.Tumesikia Sita sasa tunawsubilia wengine nao!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. n

  nicksemu Senior Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe mtanzania au mkenya? Huwajui mafisadi
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Ni nani alaumiwe pale Taasisi ama wawakilishi wa Serikali wanapokwaruzana hadharani? Yet, wanataka tuwe na imani na Serikali?
   
 10. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Penye moshi kuna moto ndani.Hakuna kuaminiana ndani ya serikali hi ni zaidi ya hatari.Mungu okoa taifa lako Tanzania
   
 11. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii game sasa inaelekea pazuri! mengi tunayasubiri! wandani wakigombana tarajia ya chumbani kuwekwa hadharani!!
   
 12. S

  Sambuka JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ni magum, kwanin wanalazmisha kua hajalishwa, wakt ye mwenyewe ndiye ajuae afya yake... TUE MAKINI HAPA OHOOO,
   
 13. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  kAMA HADI LEO HUWAJUI MAFISADI UNAITAJI KWENDA KUPIMWA AKILI,HAKIKA WEWE UTAKUA TAAHIRA HALAFU HUJITAMBUI.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo kanjanja mwingine, hakuna hata kipengele kimoja kinacho mnukuu Sitta katika uandishi wake, hayo ni maoni ya huyu tu, hawa waandishi makanjanja wanatupeleka wapi?
   
 15. S

  Shembago JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni hatari kwa taifa tene ni aibu kubwa kama Taasisi nyeti kama Jeshi la Polisi amabalo tumelipa dhamana ya kulinda raia wa TZ,wanatoa taarifa zisizo na mshiko,Hii Inatisha sana.Wananchi wenzangu,2015 tafakari,Chukua hatua
   
 16. a

  adobe JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  na mimi nasisitiza samwel sita kamnywesha sumu mwakyembe maana ndo mtu pekee anaeweza kumfikia na rahisi kupewa sumu akampa
   
 17. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Nakutajia wachache wengine malizia wewe.

  (1)E. LOWASA
  (2)J. KIWETE
  (3) Rostam Aziz
  (4) Waliokunywa maji ya Bendera ya CCM

  Wengine Malizia wewe......................
  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 18. N

  Nipe tano Senior Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kulikuwa na haraka gani kwa jeshi la polisi kutoa taarifa yao?
   
 19. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  umemsahau na"RIZ 1"teh teh!
   
 20. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Tena nasikia anataka kugombea na ubunge ktk kajimbo flani hv,anasema babu zake walitokea huko na ameshajenga na jumba la kufa mtu kwenye kakiwanja(mahame ya babu zake)
   
Loading...