Samwel Sitta alijenga bunge imara. Sijui sasa wanakosea wapi!

Kujibu swali lako unaonaje tuanze na haya mawili
1) ulikuwa upande gani wakati bunge live likiondolewa?
2)Una amini kuwa Magufuli anaingilia bunge?
1.Wakati Nape anaondoa bunge live sikukubaliana naye

2.Rais Magufuli haingilii bunge ila wabunge wengi wanatamani kufanya kazi serikalini kama mawaziri so wanajitahidi kujiweka jirani na Rais!
 
1.Wakati Nape anaondoa bunge live sikukubaliana naye

2.Rais Magufuli haingilii bunge ila wabunge wengi wanatamani kufanya kazi serikalini kama mawaziri so wanajitahidi kujiweka jirani na Rais!
Hapo no 2.nionavyo Magufuli analiingilia bunge pia
 
Nikumbukavyo mimi Sita alichukiwa na chadema klk hata Ndugai, alivyofariki walisherehekea hapa JF, tafuta huo uzi usome, isitoshe walimpiga chini Mafisadi yaliyokimbilia chadema na kumuweka Mama Makinda.
Sitta alichukiwa zaidi baada ya kuvurunda katika bunge la katiba! Kwa miaka yake 5 ya kuliongoza bunge alijitahidi sana kujenga bunge imara! Job anazidiwa kwa mbali kabisa hata na mama Makinda!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lile bunge la Kasi na Viwango la mzee Sitta (rip) kiukweli lilikuwa imara hata kwa kuliangalia tu kwa macho.
Ninakumbuka namna walivyoshughulikia issue ya Richmond na hatimaye Lowassa kubwaga manyanga, hakika ilikuwa si mchezo.
Nakumbuka pia namna Dr Slaa, Zitto Kabwe na Hamad Rashid walivyokuwa wanautendea haki upinzani ndani ya bunge.
Lakini nakumbuka jinsi mbunge Ally Kessy wa CCM alivyokuwa akiwasilisha michango yake bila kujali itikadi ya vyama.

Lakini zaidi nakumbuka namna Spika Sitta alivyokuwa anatoa maamuzi bila kuyumba wala kuyumbishwa. Hata pale mzee Lowassa alipotaka kutema nyongo na kujiuzulu alipewa fursa ya kufanya hivyo.

Imekwenda wapi ile speed na standards?!
Maendeleo hayana vyama!
Ivi ile ofisi ya Spika aliyojenga urambo,Ndugai anaitumia?
 
Nikumbukavyo mimi Sita alichukiwa na chadema klk hata Ndugai, alivyofariki walisherehekea hapa JF, tafuta huo uzi usome, isitoshe walimpiga chini Mafisadi yaliyokimbilia chadema na kumuweka Mama Makinda.
Acha kupotosha sita ailikuja kujiharibia kwenye bunge la katiba baada ya kuweka ccm mbele na kuweka maslahi ya taifa nyuma ..hata chadema walifurahi alipoteuliwa kuwa spika wa bunge la katiba wakitegemea atafanya kama alivyofanya akiwa spika wa bunge la jamuhuri, lakini alochokifanya haakuna aliyetegemea mwanakwenda yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bunge bovu kupata kutokea tangu tupate uhuru. Sababu ya ubovu huu wa bunge letu ni udhaifu wa Spika na Naibu wake.
 
Ni bunge bovu kupata kutokea tangu tupate uhuru. Sababu ya ubovu huu wa bunge letu ni udhaifu wa Spika na Naibu wake.
 
Back
Top Bottom