Samuel sitta, nisingeshiriki karamu ya wenye dhambi

sitta anawajua vizuri wenzake lakini kwa hili kachemka ccm ni kama mtumiaji wa mpira wa kiume mpira ukitumika tu unatupwa ,hakika watamtupa kazi yake imekwisha,huyu yupo tayari kufanya lolote kutimiza azma yake ndio maana ccm walisema wanataka spika mwanamke wakijua huo ni mtihani kwake hawezi kubadili jinsia
 
Hakuna jina limfaalo Sita kwa sasa maana tukimwita mhuni, wahuni wengi madhara yao huwa si kama ya Sita. Tukimwita mwizi, wevi wa kawaida huwa hawaibi pesa nyingi kama hizi alizoiba Sita na wenzake. Tukimwita mhaini, wahaini hupindua serikali, lakini Sita amepindua mamlaka ya wananchi.

Huyu Sita hakuna hata adhabu imfaayo. Akigombea tukamnyima kura, hata watu wema kuna wakati wanakosa kura. Akiwekwa jela, hata wevi wa kuku wapo jela. Tukiamua anyongwe, kuna walionyongwa kwa kuua hata mtu mmoja tu lakini Sita ameua Taifa lililotarajiwa. Sita anafaa kupewa adhabu gani? Mungu ndiye ajuaye.

......FARAO WA URAMBO....angalau itapoza kidogo hasira za wananchi
 
Nyerere alikua ana jeuri sana lakini kwa viongozi wa dini alikua mtiifu ajabu.Aliwahi kuchukuliwa na mashehe kwenda bagamoyo kufunga kwa maombi wakati wa kudai uhuru. Aliwahi kukataa wito wa watu wa kumwachilia Fisadi wa kigiriki lakini Kwa askofu MAKARIOS Nyerere alikua mpole.Sasa sijui huyu kijana wa kinyamwezi asie na hadhi ndani wala nje anajivunia nini kudharirirsha viongozi wa dini kwa ajili ya kikundi CCM. nashauri huyu bwana akifa azikwe bila kusaliwa.
 
Kikwete licha ya udhaifu wake lakini Ni mjanja wa mjini. Alijua fika kuwa mzigo mzito wa kubebeshwa Ni mnyamwezi, akaamua kumbebesha Sitta. Sasa Sitta ndio amepotea kwenye ulingo wa siasa za Tanzania kama alivyopotezwa Mwakyembe kwa kupewa uwaziri.
 
.... Kwakweli Mr Six Amelaaniwa Yeye Na Ukoo Wake Wote. Mi Nina Hasira Nae Sana, Sitaki Hata Kumuona
 
sitta anawajua vizuri wenzake lakini kwa hili kachemka ccm ni kama mtumiaji wa mpira wa kiume mpira ukitumika tu unatupwa ,hakika watamtupa kazi yake imekwisha,huyu yupo tayari kufanya lolote kutimiza azma yake ndio maana ccm walisema wanataka spika mwanamke wakijua huo ni mtihani kwake hawezi kubadili jinsia

.... Siyo Mpira Wa Kiume, Ni Kondomu Mkuu, Acha Kuzunguka
 
sitta anawajua vizuri wenzake lakini kwa hili kachemka ccm ni kama mtumiaji wa mpira wa kiume mpira ukitumika tu unatupwa ,hakika watamtupa kazi yake imekwisha,huyu yupo tayari kufanya lolote kutimiza azma yake ndio maana ccm walisema wanataka spika mwanamke wakijua huo ni mtihani kwake hawezi kubadili jinsia

Waswahili wanasema "mzigo mzito mpatie Mnyamwezi" sijui walikuwa wanamaanisha nini! Ila naona kwa Sitta kama msemo huo unalipa.
 
Tarehe 02/10/2014 ilikuwa ni siku ya maumivu kwa watz wengi. SITTA atakuja kuhukumiwa kwa jinsi alivyonyonga kwa kufanya uharamia dhidi ya haki, malipo ni hapahapa duniani.
 
sitta anawajua vizuri wenzake lakini kwa hili kachemka ccm ni kama mtumiaji wa mpira wa kiume mpira ukitumika tu unatupwa ,hakika watamtupa kazi yake imekwisha,huyu yupo tayari kufanya lolote kutimiza azma yake ndio maana ccm walisema wanataka spika mwanamke wakijua huo ni mtihani kwake hawezi kubadili jinsia

Umenifanya nicheke aiseee,eti walijua hawezi jigeuza kuwa mwanamke.
 
hata kama sita alifikiri kuondoa vipengele vyote vilivyo pendekezwa na wananchi kungemsaidia yeye kupitishwa na ccm kugombea urais naona hapa kafanya kosa kubwa kwani tuliokuwa tunamwona anafaa tumetumedhihirisha bila shaka kuwa hafai kabisa kwani maslahi ya nchi hii kwake si kitu isipokuwa urais tu.

nadhani aliingizwa katika mtego ambao hakujua kwamba yupo mtegoni..
Wajanja wamecheza vizuri karata yao..
Wamempoteza ktk njia...
Ajiandae tu Kupumzika au kubaki Urambo, ila si ktk Kuongoza nchi.
 
sitta jina lake litasahaulika kuliko hata marehemu aliyezikwa mm sikuamini kama sitta angebadilika na kuwa dickteta hivyo pia kuwatukana viongozi wa dini ndo laana ambayo itamamuliza kabisa huyu hafai msikitini wala makanisani MUNGU atamuhukumu mwenyewe mm sina mamlaka
 
Kunzia sasa hadi umauti utakapomfika six aitwe Condom na sio mpira wa kiume
 
Mungu kwa tafsiri ya Anthropologists ni Unversal power. Pale uwezo wa binadamu unapokoma kuweza kutenda lolote ndipo anakuja Mungu. Hitimisho la kusema 'Mungu mwenyewe ndie ajuaye' ni hitimisho la kukata tamaa. Ni hitimisho linalompa ukuu mkubwa mno Samwel Sita. Ni sawa na kusema Watanzania wote kwa umoja wetu ( ukiwaondoa wale wanaokubaliana na mawazo ya Sita pamoja na CCM yake) tumeshindwa kumkabili hivyo anayeweza kukabiliana naye ni Mungu peke yake. Mawazo yako ni mawazo ya mtu mwepesi wa kukata tamaa, mtu mwoga na anayesubiri nguvu kutoka nje yake yeye mwenyewe. Sikubaliani na hitimisho lako. Naamini bado watanzania wanayonafasi ya kukataa kulishwa chakula wasichokipenda. Mapinduzi (revolution is a continuous process) na ni sehemu ya maisha. Tawala zote zilizoingia madarakani kwa kauli ya kutetea wanyonge baadaye hugeuka na kuwa kandamizi. Jamii husika zisizokata tamaa kama wewe usemavyo huziondoa kwa mbinu zozote zile zinazowezekana. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni moja ya kupigiwa mfano.
Wakati wa utawala wa Sultani wa Zanzibar Afroshiraz Party ilikuwa ikishinda chaguzi mbali mbali, lakini utawala dhalimu wa Sultani uliwapora ushindi wao. Kitendo hiki cha kuto heshimu kura halali za wananchi wa Zanzibar kiliwafikisha Wanzibar Kuipindua Serikali iliyokuwa madarakani. Mwl Nyerere katika Kitabu chake cha 'Tujisahihishe' ameutaja uoga kama kizuizi kikubwa cha mapinduzi. Anasema, namnukuu. ' kama sisi tungalikuwa waoga, tusingapata uhuru' Uhuru huu tulio nao sasa ni matokeo ya watu wasiokata tamaa, kama wewe kupinga bila kuchoka ukandamizaji, uonevu, unyanyasaji na udhalilshaji uliokuwa ukifanywa na serikali ya wakati huo. Kama kweli jamii ya watanzania wanaona haki yao imeporwa na Samweli Sita kama mwewe anavyopora vifaranga vya kuku ni lazima haki hiyo idaiwe kwa njia yoyote ile. Haki haitolewi bure kwenye kisahani, inadaiwa tena kwa gharama. Ndiyo maana mahakama zote hutoza gharama za uendeshaji wa kesi. Siamini kama akija mtu nyumbani kwako akakupora mkeo kwa hila au kwa nguvu , utasema Mungu ndiye ajuaye. Utakuwa mwanaume wa ajabu. Wakurya wana usemi unaosema ' Mwanaume hufia nje, hafii ndani' ikiwa na maana kuwa mwanaume wa kweli hufia kwenye mapambano. Watala wote duniani hufanana na simba anayekula na kufuahia mawindo yake, siyo rahisi kumwondoa simba kwenye mawindo yake.
Hakuna jina limfaalo Sita kwa sasa maana tukimwita mhuni, wahuni wengi madhara yao huwa si kama ya Sita. Tukimwita mwizi, wevi wa kawaida huwa hawaibi pesa nyingi kama hizi alizoiba Sita na wenzake. Tukimwita mhaini, wahaini hupindua serikali, lakini Sita amepindua mamlaka ya wananchi.

Huyu Sita hakuna hata adhabu imfaayo. Akigombea tukamnyima kura, hata watu wema kuna wakati wanakosa kura. Akiwekwa jela, hata wevi wa kuku wapo jela. Tukiamua anyongwe, kuna walionyongwa kwa kuua hata mtu mmoja tu lakini Sita ameua Taifa lililotarajiwa. Sita anafaa kupewa adhabu gani? Mungu ndiye ajuaye.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom