Samuel Sitta amsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Madeni Kipande

Malalamiko kwa Mhandisi Kipande yalianza siku nyingi ila wakubwa waliamua kuweka pamba masikioni mwao.
 

Attachments

  • Mapendekezo TPA.pdf
    1.4 MB · Views: 743
Ndiyo ukweli halisi mwakyembe aliteleza kabisa.
Pigo la pili kwa mwakyembe alitegemea albaki hapa kwa Kipande kutokana na kumlinda muda wote huu aliokuwa akifanya udhalimu. sauti ya wengi ni sauti ya mungu. Umejidhalilisha sana mkuu na hakika mtalipa kwa uonevu wote mliofanya
 
Wadau salama....

Katika kile kinachoonekana mbio za urais kushika moto, Leo waziri wa uchukuzi Samwel Sitta bila kupepesa macho wala kutikisa masikio amemshughulikia aliyekuwa mshirika wake wa muda mrefu. Akiwa anaongea kwa ujasiri na kwa dharau Sitta amewasimamisha kazi mara moja aliyekuwa mpambe mkubwa wa Mwakyembe Bwana Madeni Kipande (kaimu DG wa Bandari). katika hatua nyingine Sitta amemsimamisha kazi pia ndugu yake Mwakyembe ambaye ni kaimu mkurugenzi wa ATC Bwana Kapten Lazaro.

Ni jambo la wazi Mwakyembe alitumia gharama kubwa sana kulinda uozo uliokuwa unafanya na Kipande pamoja na huyo ndugu yake wa ATC. kwa haraka haraka tafsiri ya hili jambo ni kwamba Sitta na Mwakyembe wamefungua ukurasa mpya wa kushughulikiana. Muda sii mrefu tutasikia pia Mwakyembe kuwafukuza kazi watu wa Sitta katika wizara ya Africa Mashariki.

Hotuba ya Nyerere

kwa haya yanaoendelea kati ya Sitta na Mwakyembe nakifananisha na maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, pale aliposema kwamba dhambi ya usaliti ni sawasawa na kula nyama ya mtu.... ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha, ina maana kwamba ukiwa na damu ya usaliti utazidi kuwa msaliti daima. Leo hii Sitta na MWAKYEMBE wameanza kusalitiana na kurogana wenyewe baada ya kumaliza wote. Sitta na Mwakyembe wa 2008 siyo wa leo, Sitta na Mwakyembe waliopika majungu na fitina dhidi ya kampuni ya Richmond leo hii hawako wamoja tena, ni wazi Mungu ni mkubwa..... wananchi tupo mkao wa kusikia yatakayojiri

Mytake: Ukiwa msaliti utazidi kuwa msaliti daima, ukiwa mnafiki utazidi kuwa mnafiki daima, ukiwa mtu wa majungu utazidi kuwa mtu wa majungu daima na ukiwa mzandiki utazidi kuwa mzandiki daima...

Asanteni
Agwambo
kilichobaki sasa wataanza kurogana wenyewe kwa wenyewe... kazi kweli kweli
 
Sita na Mwakyembe ni wanafiki wakubwa sana....... Dhambi ya usaliti inawasuta

unafika wa sitta unatoka wapi na wewe kijana wa Lowasa,acha kusingizia watu bana sitta hana kosa hata chembe kipande alikuwa hovyo hafai kuwa kiongozi.
 
Mh Sitta naomba ushikirie uzi huo huo kwani Kipande kawa mbabe mno na kudharau hadi Ofisi ya Rais Secretariate ya Ajira kwani kazi mbali mbali zilitangazwa na short list kufanyika lakini akakaidi na kuingiza watu wake....huyo mtu ni hatari mno na vema kuangalia pamoja na visingizio vya kulindwa na ofisi kubwa kwa madai yake..

Keep it up mkuu viwango na speed .
 
HII MBINU YA KIKWETE KUHAKIKISHA KUWA AKIONDOKA YEYE ANAACHA VUMBI

HAO MAJAMAA MWAKYEMBE NA SITTA SI NDO WALIKUWA KITU KIMOJA KATIKA KUMSHUGHULIKIA MH LOWASSA,

sasa unafiki wao unaanza kuwa wazi.

WAACHE WACHAMBANE WAKICHOKA LOWASSA IKULU ANAANZA KUWASHUGHULIKIA WOTE WAWILI KWA PAMOJA
 
Malalamiko kwa Mhandisi Kipande yalianza siku nyingi ila wakubwa waliamua kuweka pamba masikioni mwao.

I have read this report written by John Ulanga the retired board member, this shows the height of Kipande's arrogance, I mean he was a semi-God at TPA it was either his way or the highway ! na aliyempa kibri ni huyu huyu Mwakyembe, kwakweli they need to readvertise all those top management positions with immediate effect !!! all those jobs were placed without any valid interviews ni kujuana tu, the board had best interest za TPA lakini wakaishia kufukuzwa kwa makeke tu, kweli, mwezi mmoja wa Sita ni zaidi ya miaka 2 ya Mwakyembe....its always outcome of your actions that counts really
 
Ni kweli Mkuu. Sitta amemsimamisha kazi Madeni Kipande na nafasi yake imechukuliwa na Awadhi Massawe. Huko Bandari ni chereko, vifijo na nderemo.
Bila shaka watakuwa wanashangilia kurudishwa tena kwa mabonanza pale harbours club .
 
Bila shaka watakuwa wanashangilia kurudishwa tena kwa mabonanza pale harbours club .

bila shaka wamefurahia kuondoka kwa huyo aliyejiona yuko juu ya Board na aliyemkingia kifua naye kashatoka, JK kumweka six pale hakukosea walahi
 
Inaonekana bandari ni rahisi sana kuwang'oa watendaji.Maana kila waziri anayekuja inaonekana mkurugenzi aliepo
hafai anaondolewa,mbona hatusikii hatua kama hizo kwenye Mashirka yetu ya Reli na Ndege!.Ina maana huko hakuna uozo?.Mnasemaje Huyo Kipande hafai, wakati kwenye bunge bandari imekuwa ikisifiwa urasimu umepungua ,utoaji wa mizigo umeongezeka kwa kasi.Inaa maana Mwakyembe alikuwa hajui kama huyo madeni Kipande mnyayasaji.Vitu vingine vya ajabu kweli.Wengine tunatia shaka isije kuwa kila waziri anaingia na Mtu wake bandarini.
 
Kwa hiyo mwakyembe alikuwa anafukia madudu? au sitta anataka aanzishe yake na mtu wake.

ma CCM ni ya kufukuza kama nguruwe pori?
 
  • Thanks
Reactions: 999
Kipande deserves it. Every woman employee who refused to sleep with him was hunted down and dismissed on fabricated charges in a kangaroo court.
 
Back
Top Bottom