Samsung yatengeneza binadamu wasio halisi wenye uwezo wa kufanya kazi kama binadamu wa kawaida

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
d7b049fd941722930372497531589484


Kampuni ya Samsung kushirikiana na Advanced Research Lab (Star Lab) wamefanikiwa kutengeneza watu wasioasilia ambao watakuwa wanafanana na binadamu katika maeneo mbalimbali ya miili yao kama sura na muonekano, kuonyesha hisia, tabia na akili na pia wana uwezo wa kuzungumza na kubadilishana nae maongezi kama binadamu wa kawaida.

d7b049fd941722930372497531589484-1


Watu hao sio roboti kwa sababu roboti huwa anamilikiwa kila kitu na binadamu (kwamba bila kupata msaada wa binadamu hawezi kufanya kazi).

d7b049fd941722930372497531589484-2

Lakini watu hao waliopewa majina ya NEON wataweza kujisimamia wenyewe kwa kila kitu pia wanaweza kufanya kazi mbali mbali kama vile kusoma taarifa ya habari, anaweza kuwa mwalimu, mshauri wa masuala ya fedha, na hata msimamizi wa mazoezi (gym master). Pia, wanaweza kuwa wasemaji wa mtu au kampuni lakini pia wanaweza kuwa waigizaji.
d7b049fd941722930372497531589484-3

Mtaalamu kutoka Star lab amesema hawana lengo la kuondoa ajira za binadamu wa kawaida (Sisi) ila lengo lao ni kuboresha zaidi maingiliano ya kibiashara baina ya mtoa huduma na mteja.
d7b049fd941722930372497531589484-4

Watu hao waliotambulishwa jumatatu ya wiki hii watapatikana dunia nzima kwa ajil ya huduma mbali mbali. Samsung ndio wamekuwa Kampuni ya kwanza kutengeneza watu sio asilia (Artificial Human).
 
Baada ya miaka 30 ukoloni utarudi upya sababu hatuendani na kasi ya maendeleo ya dunia.

Mfano, wakati sisi tunapambana na kujenga barabara za lami, wenzetu wako kwenye mikakati ya kujenga frictionless roads. So baada ya miaka 10 hizi tarmac roads zitakuwa useless.



Unforgetable
Unahisi friction haina kazi??friction ndo kila kitu Kwenye barabara...huwezi kukunja kona bila friction
 
Najiuliza maswali hapa sipati jibu

Wanaweza kuumwa kama mimi?

Wanahisi njaa kama mimi?

Au Wanaenda haja kama nyinyi?
Kuumwa si sehemu ya maisha halisi ya watu maana watu tunaweza kuishi bila kuumwa tukifuata utaratibu wa asili wa jinsi ya kula.

Majibu kwa maswali mengine ni kutumia akili tuu.
 
Baada ya miaka 30 ukoloni utarudi upya sababu hatuendani na kasi ya maendeleo ya dunia.

Mfano, wakati sisi tunapambana na kujenga barabara za lami, wenzetu wako kwenye mikakati ya kujenga frictionless roads. So baada ya miaka 10 hizi tarmac roads zitakuwa useless.



Unforgetable
Bado kuna watu watasema sisi tuna akili kuliko wasungu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom