Samsung yaipiku Apple kwa mauzo ya simu robo ya kwanza ya mwaka

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
117
500
1619940814493.png

Uamuzi wa kampuni ya simu ya Samsung kushusha bei ya simu zake aina ya Galaxy S21 unaonekana kuipa faida kampuni hiyo baada ya kumpiku mpinzani wake wa karibu, Apple katika mauzo ya simu duniani kwa robo ya kwanza ya mwaka huu.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini imeonekana kufanya vizuri katika mauzo ya simu kwa kuteka soko kwa asilimia 22, ikiuza takriban simu milioni 76.5, ikilinganishwa na Apple iliyouza simu milioni 52.4 na kuambulia asilimia 15 tu ya soko kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

Samsung iliamua kushusha bei ya simu zake za Galaxy S21 kufikia dola 200 (sawa na sh 466,000). Licha ya kushuka kwa mauzo, Apple imeendelea kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, ikijitapa kuongezeka kwa mauzo ya iPhone kwa asilimia 65.

Tofauti na matarajio, iPhone 12 Mini imeuza chini ya kiwango, lakini aina zingine za simu kama iPhone 12 na iPhone 11 zimeifanya Apple kuendelea kubaki sokoni ndani ya robo hii ya kwanza ya mwaka.

Anayefuata kwa karibu ni Xiaomi ya China, ambayo imeuza simu milioni 49 na kufanikiwa kuteka asilimia 14 ya soko. Oppo na Vivo zimebaki katika nafasi tano za juu kwa kuuza simu milioni 37.6 na milioni 36 kila mmoja, wakati Huawei ikiporomoka hadi nafasi ya 7.

Kwa ujumla, soko la simu janja limekua kwa asilimia 27 katika robo ya kwanza ya mwaka, ikiuza jumla ya simu milioni 347, ukilinganisha na mwaka jana.

Chanzo: CNet
 
At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,602
2,000
Mimi naona aliefaidi hapo ni apple. Maana device zake ni premium zote na bei iko juu.

Samsung wana simu mpaka chini ya laki 2
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
12,254
2,000
Apple angekuwa na bugdet phone za laki 3-6 nyingi basi angeongoza kwa kishindo..maana kama premium zake anauza hizo copy 50m,za bei ya chini nazo angeuza sana
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,097
2,000
Apple angekuwa na bugdet phone za laki 3-6 nyingi basi angeongoza kwa kishindo..maana kama premium zake anauza hizo copy 50m,za bei ya chini nazo angeuza sana
apple anauza nchi kubwa na simu zake zinafanyiwa ruzuku unafikiri wananunua unlocked kama huku?
hio iphone se bei yake ni dola 400 hapo inauzwa dola 50 tu,

kote USA, China, Japan, Uk etc zinauzwa kwa mikataba na mitandao ya simu, wewe unaenunua Samsung ya laki 2 umelipa hela nyingi pengine alienunua iphone se,

ndio maana wachina wakienda hizo nchi wanekewa figisu hawauzi kwenye mitandao, wanaishia tu masoko ya unlocked.
Mimi naona aliefaidi hapo ni apple. Maana device zake ni premium zote na bei iko juu.

Samsung wana simu mpaka chini ya laki 2
 
mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
852
500
Hivi kati ya iPhone 12 mini na iPhone 12 ipi unashauri kununua
 
At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,602
2,000
apple anauza nchi kubwa na simu zake zinafanyiwa ruzuku unafikiri wananunua unlocked kama huku?
hio iphone se bei yake ni dola 400 hapo inauzwa dola 50 tu,

kote USA, China, Japan, Uk etc zinauzwa kwa mikataba na mitandao ya simu, wewe unaenunua Samsung ya laki 2 umelipa hela nyingi pengine alienunua iphone se,

ndio maana wachina wakienda hizo nchi wanekewa figisu hawauzi kwenye mitandao, wanaishia tu masoko ya unlocked.
Alaa nilikuwa sijui.
Sasa kwa nini huku bei iko juu hivyo..!? Hakuna Hasara.. Au mitandao ya simu inapeleka gawio. Kila baada ya muda fulani..!
 
Otterhound

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
1,777
2,000
Samsung Galaxy is my favorite phone. Apple wakasome ❌

Mchina nae anakuja juu, apple ana hali mbaya
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
22,603
2,000
Samsung Galaxy is my favorite phone. Apple wakasome

Mchina nae anakuja juu, apple ana hali mbaya
s 20 ultra mpaka s21,s21 plus ni masimu kweli kweli.

kuna ndugu yangu ni mnazi wa apple kufaa,juzi amenunua note 20 akabaki haamini macho yake.

hayo madude ni majini.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
22,603
2,000
Apple angekuwa na bugdet phone za laki 3-6 nyingi basi angeongoza kwa kishindo..maana kama premium zake anauza hizo copy 50m,za bei ya chini nazo angeuza sana
hana namna atakuja huku tu.

mwaka jana katoa simu 4 kwa pamoja.kwa ripoti hizi usishangae mwaka huu akaja na simu 6 sokoni.

watu wa kipato cha chini tukitaka simu za apple basi tunakwenda kununua simu za miaka minne nyuma huko,ambazo nyingi zimeshapoteza ubora wa betri nk.wakati wenzake wameshtuka kwamba siku hizi simu za kiwango cha kati zinauzika sana.maana zina betri imara,storage,na ni za kisasa ingawa nyingi hazina feature premium,kitu ambacho sio hitaji la walio wengi maana hawana matumizi nazo.

samsungu kajigawa hivyo,ukitaka simu zenye kila sifa kuna za mamilioni huko juu,ukitaka ubora wa kati kuna za milioni,na ukitaka za ubora wa chini zipo za malaki.apple wao wana simu za mamilioni tu.wanadai wana wateja watiifu.
 
Otterhound

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
1,777
2,000
s 20 ultra mpaka s21,s21 plus ni masimu kweli kweli.

kuna ndugu yangu ni mnazi wa apple kufaa,juzi amenunua note 20 akabaki haamini macho yake.

hayo madude ni majini.

Aise, alichelewa sana mkuu mkorinto. Wengine wanazisifia iphone kwa sababu tu ya mapenzi yao kwa marekani, lakini hapo hapo anatumia Samsung n.k. akili zingine bwana!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom